12 Mfunguo Nne 1440
Utafutaji wa Kina
Skip Navigation Links

Kususia Bidhaa ya Kimarekani na Kiyahudi

الســؤال

Nini Hukumu ya kisheria ya kugomea bidhaa za kimarekani na kiyahudi?

الجـــواب

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ipo tofauti baina ya (Kususia) mgomo wa kimataifa na ambao unaweza kuathiri katika siasa za kimataifa, na baina ya migomo binafsi ambayo haiathiri siasa, lakini lengo lake ni kumlea mwanadamu kinafsi na kuihisisha juu ya wajibu wa kuwanusuru waislamu wanaodhulumiwa Duniani.
Na maamuzi ya migomo ya kimataifa lazima yatolewe na Mamlaka kuu za kutoa maamuzi zenye uzito mkubwa kisiasa na kiuchumi, kama vile serikali zinazoelekeza sera za uchumi za nje na mashirika makuu ambayo yana athari kubwa katika kuagiza bidhaa nje ya nchi, ili yalete tija inayotakiwa kwa maamuzi hayo, katika kusimamisha mashambulizi dhidi ya waislamu na kushinikiza ili kukomesha mzingiro wa kiuchumi au ugaidi au njaa. Na ni lazima hapa yatafitiwe na kujulikana madhara na faida za uamuzi wa kufanya mgomo, pamoja na kulinganisha baina ya faida na hasara zake.
Na kutokana na hayo, hakuna kizuizi chochote cha wewe kununua unachokihitaji katika bidhaa za mashirika ya nchi hizo, na wala kufanya hivyo hakuzingatiwi kuwa ni kuyasaidia mashirika hayo au nchi husika kuwashambulia waislamu, na wala huna dhambi yoyote kwa kitendo hicho cha wewe kununua bidhaa hizo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote.

Ukurasa wa Kwanza Utambulisho wa Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri Ombi la Fatwa خريطة الموقع آراء ومـقـتـرحــات Wasiliana Nasi