kuosha maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

kuosha maiti

Question

Ni ipi hukumu ya kisheria kwa wale wasiohitajika kuhudhuria kuosha maiti?

Answer

Inapendekezwa kuwekewa mipaka kwa wale wanaomuosha maiti na anayeteuliwa tu, na inachukiza kuhudhuria wale wasiohitajika katika kuosha.

Inapendekezwa kuwa mwenye kuhudhuria kuosha maiti ni yule tu anayemuosha, na anayemsaidia katika kuosha kwake, na inachukiza kuwepo kwa wale ambao kuwepo kwao sio lazima. Mtu, kwa tabia yake, hapendi mtu yeyote kuona sehemu zake za siri. Siku zote anapenda heshima yake kuhifadhiwa, awe yu hai au amekufa, na sharia ya Kiislamu imechunga kuhifadhi heshima ya maiti, na kuitilia mkazo na kuihimiza. Amesema Mtume (S.A.W):“Atakaemwosha maiti na akatimiza amana aliyopewa na wala asitoe siri ya aibu yake yoyote ile aliyonayo, yataondoka madhambi yake kama siku alivyozaliwa na mama yake.” Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad.

Share this:

Related Fatwas