Kufanya Umra Zaidi ya Mara Moja kwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufanya Umra Zaidi ya Mara Moja kwa Mwenye Kujistarehesha Kati ya Umra na Hija.

Question

Swali linahusu kuitekeleza Ibada ya Umra zaidi ya mara moja kwa mwenye kujistarehesha kati ya Umra na Hija, baada ya kuifuta Ihramu yake ya Umra ya kwanza, ambao aliinuia kwa ajili ya kujistarehesha kati ya Umra na Hija? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Inajuzu kwa uwazi kurudiarudia Umra zaidi ya mara moja, na kuitekeleza Ibada hii siku zote ni jambo lililosuniwa, na haya ni maoni ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy, Shafiy, na wanazuoni wengi waliotangulia na waliowafuatia.
Na miongoni mwa walionukulu hayo kutoka kwa wengi wa wanazuoni ni: Al-Mawardiy, As-Sarkhasiy, Al-A’abdariy, na An-Nawawiy. Na Ibn Al-Mundhir aliinukulu hayo kutoka kwa Ali ibn Abi Twalib, Ibn Omar, Ibn Abbas, Anas, Aisha, A’atwaa, na wengineo RA.
Na ni pokezi moja lililopokelewa na Ahamad na Is-haaq Ibn Rahawaih, pia ni kauli ya Mutarraf na Ibn Al-Mawwaz miongoni mwa wafuasi wa Madhehebu ya Malik.
Na mfano wa huyu mwenye kujistarehesha baada ya kuifuta ihramu ya Umra yake ya kwanza ambayo aliinuia kujistarehesha kati ya Umra na Hija, na kabla ya kuitekeleza Ihramu yake kwa ajili ya kufanya Hija.
Na Umra haikatazwi katu isipokuwa katika sura kadhaa maalumu ambazo maelezo yake yatatolewa baadaye. Na sura hii iliyotajwa katika swali hakika siyo miongoni mwa sura hizo. Kwa hiyo Umra kwa uwazi wake ni jambo linalopendeza, hivyo atakayeitekeleza basi atafanya ibada iliyosuniwa, na atapata thawabu zake, kwa mujibu wa rai ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy, Shafiy, na wengi miongoni mwa wanazuoni waliotangulia na waliowafuatia.
Na Umra inajuzu kutekelezwa wakati wowote, isipokuwa katika siku maalumu nazo ni Siku Tano za Hija: Siku ya A’rafah, Siku ya Idi Kubwa, na Siku Tatu baada ya Idi Kubwa (Siku za Tashriiq Siku za kusherehekea Sikukuu), na hii inatokana na Bi Aisha, Ibn Abbas, R.A. Na maana yake ni kwamba: inajuzu kutekeleza ibada ya Umra mara kwa mara kwa mwenye kujistarehesha na mwingine yoyote, katika siku zingine isipokuwa hizo tano zilizotajwa hapo juu. Na pia inajuzu pamoja na kuchukiza kwake kwa mujibu wa maoni ya wafuasi wa Madhehebu ya Malik ambao wao wanaona kuwa: ni jambo linalochukiza kutekeleza Ibada ya Umra zaidi ya mara moja kila mwaka.
Na maana ya kujistarehesha, kwa maoni ya wanazuoni ni: Mtu ambaye sio mkazi wa Makkah atatekeleza Umra, kisha akafuta Ihramu ya Umra hii, na akiwa ndani ya miezi ya Hija, kisha atatekeleza Hija bila ya kurudi mji wake au mfano wa mji wake, muda wa kati ya Hija na Umra. Na atakayekuwa na hali hii ataitwa: mwenye kujistarehesha, na atalazimika kuchinja kondoo. Na sababu ya jina hili ni kwamba, atajistarehesha kwa kufanya yaliyokatazwa yanayoambatana na kutekeleza Umra, wakati anapoifuta Ihramu ya Umra mpaka atakaponuia tena Ihramu yake kwa ajili ya kufanya Hija.
Na wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy wanasema kuwa: kurudiarudia Umra ni jambo la kupendeza, na siyo la kuchukiza, na inajuzu kuitekeleza wakati wowote ndani ya mwaka mzima, isipokuwa siku tano ambazo ni: Siku ya A’arafah, Siku ya Idi Kubwa, na siku tatu baada ya Idi Kubwa. Kwa hiyo inajuzu kwa maoni yao kurudiarudia Umra kwa mwenye kujistarehesha na mwingine yoyote asiyefanya hivyo, isipokuwa siku tano zilizotajwa. Na Mwanachuoni wa Madhehebu ya Hanafi Ibn A’abidiin katika kitabu cha [Raddul Muhtar; 2/585, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Inajuzu Kurudiarudia Umra ndani ya mwaka mmoja, kinyume na Hija, na kauli hii pia ni ya Mwandishi wa Al-Hindiyah”. Nae anasema pia [2/472]: “kurudiarudia Umra hakuchukizi, kinyume cha rai ya Imamu Malik, lakini rai ya wengi miongoni mwa wanazuoni, ni bora zaidi”.
Na katika kitabu cha [Al-Hidayah] moja ya vitabu vya wafuasi wa madhehebu ya Hanfiy, Mwenyezi Mungu awarehemu [1/178, Ch. ya dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] pamoja na maelezo zake, kama vile: [Al-I’inayah Sharh Al-Hidayah: 3/136-139, Ch. ya Dar Al-Fikr] na [Al-BinayahSharh Al-Hidayah: 4/460, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] na [Fat-hul Qadiir: 3/137, Ch. ya dar Al-Fikr] kuwa: “(Umra haipitwi na wakati) kwa sababu haina wakati maalumu (na inajuzu kutekelezwa wakati wowote ndani ya mwaka mzima), na mtu akinuia Umra ndani ya miezi ya Hija, kisha akafika Makkah Siku ya Idi Kubwa atamaliza Umra yake, na halazimiki kuchinja mnyama.
Kwa ujumla mwaka mzima ni wakati wa Ibada ya Umra, na dalili ya kuwa unajuzu kutekelezwa ndani ya miezi ya Hija bila kuchukiza ni ile Hadithi ilivyopokelewa na Imamu Bukhariy katika Sahih yake, kwa Isnadi yake kutoka kwa Mtume S.A.W., kuwa: “Yeye alitekeleza ibada ya Umra ndani ya Mfungo Pili mara nne, isipokuwa ile Umra aliyoitekeleza sambamba na Hija”.
(Isipokuwa kupitia siku tano, ambapo inachukiza kufanya Umra ndani yake, nazo ni: Siku ya A’arafah, Siku ya Idi Kubwa, na siku tatu baada ya Idi Kubwa. Kwa Hadithi iliyopokelewa na Aisha R.A, kuwa: Mtume alikuwa akichukia kufanya Umra ndani ya siku hizi tano.
Na Al-Baihaqiy amepokea kutoka kwa Aisha R.A, akisema: Umra inajuzu kutekelezwa ndani ya mwaka mzima isipokuwa ndani ya siku nne: Siku ya A’arafah, Siku ya Idi Kubwa, na Siku Mbili baada ya Idi Kubwa. Na Said Ibn Mansuur amepokea kutoka kwa Ibn Abbas R.A: Siku tano: A’arafah, Idi Kubwa, na Siku Tatu baada ya Siku ya Idi Kubwa, utekeleze umra kabla ya siku hizi au baada yake kama utakavyo. Na kwa sababu siku hizi ni za Hija, kwa hiyo zinahusu amali zake tu.
Na kutoka kwa Abu Yusuf, Mwenyezi Mungu amrehemu, anasema kuwa: Umra haikatazwi kutekelezwa siku ya A’arafah kwa sharti kwamba itekelezwe kabla ya wakati wa Adhuhuri, na kwa sababu wakati wa nguzo ya Hija huwa baada ya Adhuhuri na siyo kabla yake, na Madhehebu sahihi ni yale tuliyoyataja hapo juu, ambayo ni: kuchukiza utekelezaji wa Umra kabla na baada ya wakati wa Adhuhuri (lakini akiitekeleza ndani ya siku hizi tano basi Umra ni sahihi, na akaendelea na Ihramu ndani yake) yaani ndani ya Umra, na asipoitekeleza ndani ya siku hizi, kwa mfano wa kuitekeleza Swala baada ya kufikia wakati Kuchukiza (kwa sababu Kuchukiza kunatokana na sababu nyingine) yaani sababu isiyohusu Umra.
Hapo Mwanachuoni huyu anataka kusema kuwa Kuchukiza ni sababu inayohusu kitu kingine kisichokuwa Umra, na sio Umra yenyewe (nacho ni kutukuza jambo la Hija na kuainisha wakati maalumu kwa ajili ya kuitekeleza) na kutukuza jambo lake ni kwa kuainisha wakati maalumu ambao haushirikishwi na kitu chochote. Na kama chukizo hapo ni kwa ajili ya kitu kingine, basi (inasihi kuitekeleza Umra)”.
Kwa maoni ya wafuasi wa madhehebu ya Shafiy: Inajuzu kuitekeleza Umra katika wakati wowote wa mwaka, na haichukizi wakati wowote, pamoja na kutekelezwa ndani ya Miezi ya Hija na mingineyo bila ya kuchukiza. Vile vile haichukizi kutekelezwa Umra moja au zaidi ndani ya mwaka mmoja au siku moja, bali inatakiwa kutekelezwa zaidi na zaidi.
Na Umra haikatazwi, kwa maoni yao, isipokuwa kwa mwenye Ihramu kwa ajili ya kutekeleza Hija, hata akifuta Ihramu ya Hija mara mbili na akakaa Minaa kwa ajili ya kutupa mawe na kulala huko, basi Ihramu yake ya umra haifungwi, kwa sababu hawezi kushughulika kwa Umra, bali analazimika kumaliza kazi za Hija kwa kutupa mawe na kulala huko.
Na kama atafanya mwendo wa kwanza, baada ya kupiga mawe ndani ya siku ya Pili ya Tashriiq, kisha akafunga Ihramu ya Umra ndani ya Siku za Tashriiq zilizobakia, iwe usiku au mchana, basi Umra yake ni sahihi kwa maoni yao.
Na kwa mujibu wa hayo inajuzu kwa mwenye kujistarehesha, kwa maoni ya wafuasi wa madhehebu ya Shafiy, kufanya Umra zaidi ya mara moja, isipokuwa wakati wa Ihramu ya Hija, hadi mwendo wa kwanza baada ya kupiga mawe ndani ya Siku ya Pili ya Tashriiq.
Na Imamu Al-U’umraniy mfuasi wa madhehebu ya Shafiy katika kitabu cha: [Al-Bayan: 4/63-64, Ch. ya Dar Al-Minhaj] anasema: “Inajuzu kufanya Umra ndani ya mwaka mmoja, mara mbili, tatu, na zaidi, na inatakiwa kuifanya mara nyingi. Na rai hii ni ya Abu Hanifa; na Imamu Malik anasema: Haijuzu ndani ya mwaka mmoja isipokuwa Umra moja, na rai hii ni ya An Nakhi’iy na Ibn Siriin”.
Na Imamu Muhiy Diin An Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Majmuu’ Sharh Al-Muhadhab: 7/147-150, Ch. ya Dar Al-Fikr, kwa muhtasari] anasema: “Imamu Shafiy na wafuasi wake wanasema kuwa: Mwaka mzima ni wakati wa Umra, kwa hiyo inajuzu kuitekeleza Ihramu kwa ajili ya Umra katika wakati wowote wa mwaka, na haichukizi katika wakati wo wote, ndani ya Miezi ya Hija au mingineyo, kwa kujuzu kwake huko ni bila ya Kuchukiza; na haichukizi kufanywa Umra mara mbili au tatu au zaidi ndani ya mwaka mmoja, au ndani ya siku moja, bali inatakiwa kufanywa zaidi na zaidi, bila hitilafu kati yetu…
Na wanazuoni wenzetu wanasema: Huenda kukatazwa kufanywa Ihramu kwa ajili ya Umra ndani ya baadhi ya nyakati kunatokana na dharura, na siyo kwa wakati wenyewe, kama vile mwenye Ihramu ya Hija haijuzu kwake kuitekeleza Ihramu kwa ajili ya Umra baada ya kuanza kufuta Ihramu ya Hija, bila hitilafu, kwa hiyo Ihramu yake haijuzu kwa ajili ya Umra kabla ya kuanza kufuta Ihramu ya Hija, kwa mujibu wa Madhehebu…
Na wakasema pia kuwa: akifuta Ihramu mbili za Hija, na akakaa Minaa kwa ajili ya kutupa mawe na kulala usingizi huko, kisha akafunga Ihramu kwa ajili ya Umra, hapo Ihramu yake haifungiki bila hitilafu; na hii imetajwa na Imamu Shafiy, na wanazuoni wenzetu wameikubali; kwa sababu mtu huyu hana uwezo wa kushughulikia vitendo vya Umra, wakati analazimika kushughulikia kutimiza vitendo vya Hija kama kupiga mawe na kulala usingizi kuko.
Na wakasema pia: Mtu halazimiki kitu cho chote, lakini akienda mwendo wa kwanza baada ya kupiga mawe ndani ya Siku ya Pili ya Tashriiq, kisha akafunga Ihramu ya Umra ndani ya mabaki ya Siku za Tashriiq, iwe mchana au usiku, basi Umra yake ni sahihi, bila hitilafu.
Na Sheikh Abu Muhammad Al-Juwainiy katika kitabu cha [Al-Furuuq] na wengineo pia wanasema: Tofauti kati ya sura hizi mbili ni kuwa mkazi wa Minaa ndani ya siku ya mwendo, ingawa asipokuwa na Ihramu kwa mujibu wa kufuta Ihramu kwa mara mbili, isipokuwa yeye amekaa kwa ajili ya kutekeleza Ibada maalumu ambayo ameshughulika kuitimiza, nayo ni kupiga mawe na kulala huku, ni miongoni mwa yanayoikamilisha Hija, kwa hiyo Umra yake haihirimiwi kabla ya kumaliza Hija yake, kinyume na mwenye kuenda mwendo ambaye alimaliza Hija yake, na akawa mfano wa asiye na Hija.
Na Abu Muhammada anasema: Hakuna sura inayoonesha kuwa mtu anaweza kufunga Ihramu ya Umra wakati hajahirimia Umra yake isipokuwa katika sura hii, lakini inajadiliwa kuwa akitekeleza Ihramu wakati wa kujamiiana na mke wake, basi ni halali lakini Ihramu yake haifungika, kwa rai sahihi zaidi”.
Kisha Imamu An-Nawawiy katika: “Tawi la Madhehebu zao kuhusu kufanya Umra zaidi ya mara moja ndani ya mwaka mmoja anasema: “Madhehebu yetu kuwa: hivyo hakuchukizi, bali inatakiwa hivyo, na hii ni rai ya Abu Hanifa, Ahamd, na wengi wa wanazuoni miongoni mwa Salaf na waliowafuatia; miongoni mwa wengi wa wanazuoni ni: Al-Mawardiy, As-Sarkhasiy, na Al-A’abdariy; na Ibn Al-Mundhir aliipokea kutoka kwa Ali Ibn Abi Twalib, Ibn Umar, Ibn Abbas, Anas, Aisha, Atwaa, na wengineo R.A. Na Al-Hasan Al-Baswriy, Ibn Siriin, na Malik wanasema: Inachukiza kufanya Umra zaidi ya mara moja ndani ya mwaka mmoja, kwa sababu ni ibada inayokusanya Tawafu na Saiy, kwa hiyo haifanywi isipokuwa mara moja kila mwaka, mfano wa Hija… Kuna jibu kwa dalili ya Imamu malik ambapo kutumia Kipimo (Qiyasi) cha Hija kuwa: Hija ni ibada yenye wakati maalumu, kwa hiyo haiwezekani kutekelezwa zaidi ya mara moja kila mwaka, lakini Umra haina wakati maalumu, kwa hiyo inaweza kufanywa zaidi ya mara moja, mfano wa Sala”.
Na Sheikh wa Uislamu Zacharia Katika kitabu cha [Sharh Al-Bahjah Al-Wardiyah: 2/278, Ch. ya Al-Maimaniyah] anasema: “Wakati wowote ni wakati wa kufanya Umra kwa mtu ye yeote, isipokuwa Hujaji anayekaa Minaa kwa ajili ya kupiga mawe, huyu hakatazwi kutekeleza Ihramu ya Umra, na kabla ya kufuta Ihramu yake ya Hija ili kutokusanya Hija na Umra pamoja, kwa hiyo hakatazwi kutekeleza Ihramu ya Umra hata kama hatakuwepo Minaa, na baada ya hapo ili yeye ashughulikie ibada za kupiga mawe na kulala usingizi huku, na kwa hivyo yeye hawezi kushughulikia kazi za Umra wakati wa Hija, na haya maelezo yana mitazamo mbalimbali. Na inafahamika kutokana na hayo kuwa inakatazwa kuhiji Hija mbili ndani ya mwaka mmoja, kama alivyotaja katika kitabu cha [Al-Umm], na akathibitisha hivyo…
Naam, akiwa na haraka ndani ya siku ya pili ya Tatshriiq Ihramu yake ya Umra ni sahihi, hata akiwa katika wakati wa kupiga mawe, kwa sababu alipoenda mwendo akatoka katika Hija, na ikawa kama vile wakati wa kupiga mawe umeisha. Na kauli hii ameinukulu Kadhi Abu Attayib kutoka katika Matini ya Kitabu cha Al-Umm; na katika Kitabu cha Al-Majmuu anasema: haina hitilafu juu yake…
Na kuitekeleza ihramu ya Umra katika nyakati zote za kufanya hivyo haichukizi, bali ni Sunna ya kuitekeleza zaidi na zaidi, na haichukizi ndani ya mwaka mmoja kutekelezwa mara nyingi, kwa sababu Mtume SAW, “Alimuamrisha Bi Aisha mara atekeleze mbili ndani ya mwaka mmoja, na Aisha mwenyewe alifanya Umra mara mbili ndani ya mwaka mmoja, yaani baada kifo chake Mtume”. Na katika mapokezi mengine ni: mara tatu. Na Ibn umar alifanya Umra mara mbili ndani ya mwaka mmoja, kwa miaka mingi. Hadithi hii imepokelewa na Shafiy na Baihaqiy.
Na Sheikh wa Uislamu Ibn Hajar Al-Haitamiy, Mwenyezi Mungu amrehemu, katika kitabu cha [Al-Minhaj Al-qawiim Sharh Al-Muqadimah Al-Hadhramiyah: UK. 274] anasema: “(Inajuzu kutekelezwa Ihramu ya Umra katika wakati wowote) kwa sababu mwaka mzima ni wakati wa Umra. Ndio, hakatazwi Hujaji kutekeleza Ihramu ya Umra, kwa kuwa tu yeye anahusika na Ibada za Hija kama vile kupiga mawe, kwa sababu kuwepo kwa hukumu ya Ihramu ni kuwepo kwa Ihramu yenyewe, kwa hiyo kakuna Hija mbili ndani ya mwaka mmoja, kinyume na aliyedai hivyo. Na ni Sunna kufanya umra mara nyingi, hata ukiwa ndani ya siku moja, kwa sababu Umra ni bora zaidi kuliko Tawafu, kwa rai inayotambuliwa. Lakini kuna mjadala kuhusu wakati wa Umra na ule wa Tawafu”.
Na wafuasi wa Madhehebu ya Malik wanaona kuwa wakati wa Umra ni mwaka mzima, isipokuwa Siku za Minaa, pamoja na kuonesha chukizo la kufanya Umra mara nyingi, na ikiwa mtu atatekeleza Ihramu kwa ajili ya Umra nyingine, ihramu yake itakubalika, na zaidi ya hayo baadhi ya wanazuoni walinukulu kuwa itakubalika kwa kauli ya pamoja.
Na Imamu Ibn Al-Hajib mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha [Jamii Al-Ummahaat: Uk. 187, Ch. ya Al-Yamamah] anasema: “Umra inajuzu ndani ya mwaka mzima, isipokuwa siku za Minaa kwa Hujaji, na Ihramu haikubaliki isipokuwa baada ya kupiga mawe na kutoka katika Minaa, hapo itakubalika. Na kuhusu kufanya Umra zaidi ya mara moja ndani ya mwaka, kuna kauli mbili”.
Kauli hizi mbili zilielezwa na Mtaalamu Al-Hatwaab katika kitabu cha [Mawahib Al-Jaliil Fi Sharh Mukhtasar Khaliil: 2/467-468, Ch. ya Dar Al-Fikr] akisema: “Kauli mbili: mashuhuri kati yake inaonesha kuwa kufanya Umra zaidi ya mara moja kunachukua, nayo ni madhehebu ya Al-Mudawanah; na kauli isiyo ya kawaida ya Mutarraf inaonesha kuwa inajuzu kufanya umra zaidi ya mara moja, na mfano wake upo kwa Ibn Al-Mawwaz, kwa sababu yeye anasema: Nataraji kuwa sio kosa kufanya umra mara mbili kila mwaka. Na Aisha alifanya Umra mara mbili ndani ya mwaka mmoja, na Ibn Umar na Ibn Al-Munkadir wakafanya hivyo hivyo, na Aisha alichukizwa kufanya Umra mara mbili ndani ya mwezi mmoja, kama alivyochukizwa Al-Qasim Ibn Muhammad…
Na kwa kauli mashuhuri ni kuwa inachukiza kufanya Umra zaidi ya mara moja kila mwaka, hata kama mtu ataitekeleza Ihramu kwa Umra nyingine ihramu yake itafungika kwa kauli ya pamoja. Na katika Al-Mudawanah anasema: Umra ndani ya mwaka mmoja ni mara moja, na kama mtu ataitekeleza nyingine basi itasihi, ikiwa Umra ya kwanza ipo ndani ya Miezi ya Hija au haiko ndani ya miezi hiyo, na kama mtu anataka kuhiji ndani ya mwaka huu au siyo”. [Mwisho].
Na inajuzu kwenda Umra zaidi ya mara moja kwa mapokezi ya Imamu Ahmad na Is-ahaaq Ibn Rahawaih. Na katika [Masaail] ya Imamu Is-Haaq Ibn Mansuur Al-Kausaj kwa Maimamu Wawili: 5/227, Ch. ya Al-Jamia’ah Al-Islamiyah, Madina]: Nimesema: “Je, mtu anaweza kufanya Umra ndani ya mwezi mmoja atakavyo? Imamu Ahmad amesema: mtu atafanya kama atakavyo, kwani Umra haina wakati maalumu lakini hija ina wakati maalumu.
Na Is-haaq Ibn Rahawaih anasema: kama alivyosema lakini afadhali kufanya Umra mara moja kila mwezi; inafanyika hivyo kwa ajili ya kukusanya hitilafu, na kuwezesha kunyoa”. Hapo Maimamu Ahmad na Ibn Rahawaih – ndani ya mapokezi haya – walikubali kuwa inajuzu kwa Mtu kufanya Umra kama atakavyo, na hakuna kizuizi chochote cha kufanya zaidi ya mara moja. Bila shaka hili linaambatana na wakati ambao ndani yake ibada ya Umra inakatazwa, kwa sababu ya kushughulikia Ibada za Hija.
Na dalili ya kujuzu kufanya Umra zaidi ya mara moja ni kama ilivyopokelewa na Bukhariy na Muslim kutoka kwa Abu Huraira, kwa Isnadi Marfuu’: “Umra hadi Umra hufuta dhambi zilizotendwa baina yake” na hakutofautisha kati ya kuwepo kwake ndani ya mwaka mmoja au miaka miwili. Hivyo dalili hii imetolewa na Imamu Al-Umraniy na Sheikh Abu Is-haaq Ash-Shiraziy na Al-Baihaqiy na wengineo miongoni mwa wanazuoni wa Madhhebu ya Shafiy, lakini Imamu An-Nawawiy Sheikh wa Madhehebu haikubali, katika kitabu cha [Al-Majmuu’: 7/149, Ch. ya Dar Al-Fikr], akielekea kuwa hoja ya dalili hii haiko wazi.
Ni wazi kwamba ukweli ni wao, kwa sababu kufanya toba mara nyingi na Ibada za kufuta dhambi zinatakiwa kisheria, kwa hiyo dalili yao ni sahihi, na hili linaegemezwa katika Hadithi Sahihi iliyopokelewa na At-Tirmidhiy kutoka kwa Abdullahi Ibn masu’ud anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, amesema:”Endelezeni ibada kati ya Hija na Umra kwani Ibada hizo zinaondoa umaskini na dhambi, kama pampu inavyoondoa uchafu wa chuma, dhahabu na fedha, na hakuna malipo yoyote ya Hija iliyokubalika isipokuwa Pepo”. Kwa hivyo basi kuzifanya mara nyingi na kuzifuatanisha ni sehemu ya maana ya amri ya kuziendeleza kwa ujumla, kama ilivyo wazi.
Na Al-Hafidh katika kitabu cha: [Fat-hul Bariy: 3/598] kwenye Sharh yake ya Hadithi ya Abu Huraira, na baada ya kuashiria Hadithi ya Ibn Masu’ud, anasema: “Hadithi ya Mlango huu ina maana ya kuhimiza kufanya umra zaidi ya mara moja, na hii ni kinyume na alivyosema: inachukiza kufanywa umra zaidi ya mara moja kila mwaka, mfano wa wafuasi wa Madhehebu ya Maliki, na wengineo wanaosema: mara moja ndani ya mwezi mmoja.
Na dalili yao ni kwamba Mtume S.A.W., hakuitekeleza Ibada hii isipokuwa mwaka hadi mwaka, na matendo yake huonesha wajibu au kazi ya kupendeza, na kujibiwa kuwa: kazi ya kupendeza haihesabiki katika matendo yake, kwani yeye alikuwa akiacha kazi hali ya kupendeza kwake kwa ajili ya kuepushia ugumu Umma wake, na akahimiza hivyo kwa kauli yake, kwa hivyo basi inaonekana wazi kuwa ni kazi ya kupendeza.
Na wao walikubali kuwa inajuzu kufanya Umra ndani ya siku zote kwa asiyetekeleza Ibada za Hija, isipokuwa kwa mujibu wa ilivyopokelewa na wafuasi wa Madhehebu ya Hanafiy kuwa: ni inachukiza kutekelezwa ndani ya Siku ya A’arafa, Siku ya Idi Kubwa, na Siku Tatu za kusherehekea Iddi Kubwa. Na Al-Athram amepokea kutoka kwa Ahmad kwamba: Mtu akifanya Umra hapana budi anyoe au apunguze nywele zake, kwa hiyo hawezi kufanya Umra tena hadi siku kumi zipite, ili aweze kunyoa kichwa chake. Na Ibn Qudamah anasema: hii inaonesha kuwa Inachukiza kufanya Umra ndani ya muda usio wa siku kumi, kwa rai yake”.
Na miongoni mwa dalili pia ni ile iliyopokelewa kuwa: Aisha R.A, alifanya Umra mara mbili ndani ya mwezi mmoja kwa mujibu wa amri ya Mtume S.A.W.
Na imepokewa kutoka kwa Ali kuwa: Alikuwa akifanya Umra kila siku.
Na kutoka kwa Ibn Umar kuwa: Alikuwa akifanya Umra ndani ya kila siku za mwaka kwa maelezo ya Ibn Az-Zubair. Na Habari hizi zimepokelewa na Shafiy na Al-Baihaqiy kwa Isnadi zao.
Na kwa kuwa umra ni ibada isiyoambatana na wakati na haiainishwi kwa nyakati za mwaka, basi inalazimika iwe namna ya ibada inavyofanywa siku zote na kila wakati, kama vile: Saumu na Sala.
Na Umra imeitwa kwa jina hili kwa sababu inafanywa muda wa umri mzima. Na inasemwa: imeitwa hivyo kwa sababu ya kutekelezwa kwake katika mahali pa makazi, na pia inasemwa: Umra maana yake ya kilugha ni kusudio, kwa hiyo huonesha maana ile ile.
Na dalili ya kuwa Umra inajuzu kutekelezwa ndani ya muda wowote wa mwaka na kuwa haichukizi ndani ya nyakati zote – kama ilivtotajwa katika kitabu cha: [Al-Majmuu: 7/149] kuwa: Asili yake ni kutokuwepo chukizo lolote mpaka liwepo katazo la Kisheria, na katazo hilo halipo; na pia inajuzu kuunganisha kati ya Hija na Umra (Qiran) ndani ya siku ya A’arafa bila ya kuchukiza, hivyo haikuchukiza kufanya Umra peke yake (Ifrad) ndani yake mfano wa nyakati zote za mwaka.
Na kwa sababu wakati ambao haikuwa makuruhu ndani yake kuendeleza Umra, pia haikuwa makuruhu kuanza kwake, kama ilivyo kwa mwaka mzima. Na kuhusu kauli ya kuwa: umra inachukiza ndani ya Siku za Hija, ni kauli batili na haina dalili.
Kisha Imamu An Nawawiy katika kitabu cha [Al-Majmuu: 7/149-150] anasema: “Imamu Shafiy, wafuasi wake, Ibn Al-Mundhir na wengineo walitoa hoja iliyotajwa katika Vitabu Viwili vya Sahihi kuwa: “Aisha R.A, alitekeleza Ihramu ya Umra mwaka wa Hija ya Kuaga, akapata hedhi, na Mtume S.A.W, alimuamuru atekeleze Ihramu ya Hija, akafanya, akawa ni mwenye kuunganisha (Qiran), akasitisha Ibada kwa ujumla, na alipopata tahara ya hedhi akatekeleza Tawafu na Saiy, hapo Mtume S.A.W akamwambia: Umekwisha futa Ihramu yake ya Hija na Umra, hapo Aisha alimuomba Mtume S.A.W., ampe idhini ya kufanya Umra nyingine, na Mtume S.A.W., ampe idhini, akafanya umra nyingine kutoka katika mahali pa (Tani’im)”. Hadithi hii imepokelewa na Bukhariy na Muslim kwa urefu wake, na mimi niliinukulu kwa ufupisho wake.
Na Imamu Shafiy anasema: Umra hii ya kwanza ya Bi Aisha ilikuwa ndani ya Mfungo tatu, na wa pili pia ulikuwa ndani ya Mfungo tatu, yaani Umra hizi mbili zilikuwa ndani ya Mfungo tatu.
Pia kutoka kwa Bi Aisha kuwa yeye alifanya Umra mara mbili ndani ya mwaka mmoja, yaani baada ya kifo cha Mtume S.A.W, na katika mengine: Umra tatu. Na kutoka kwa Ibn Umar kuwa alifanya Umra kwa miaka mingi katika zama za Ibn Az-Zubair mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Na Imamu Shafiy na Al-Baihaqiy walizitaja Hadithi hizi zote kwa Isnadi zao”.
Na wafuasi wa Madhehebu ya Hanbal waliwapinga wanazuoni hawa, na wakajuzisha kufanya Umra zaidi ya mara moja, kisha wakazuia kuendeleza, na wakadai kuwa ni kwa kunukulu kutoka kwa Salaf. Na ni wazi kwamba hii siyo sahihi; kwa sababu wao wenyewe walinukulu kutoka kwa Masahaba wengi na Matabiin kujuzu kwa kuendeleza, na wanaojuzisha ni wengi sana kuliko wanaokataza, na kujuzisha kufanya zaidi ya mara moja kisha kukataza kuendeleza ni utata na madai yasiyo na dalili, na kudai kuwa Salaf walikataza kuendeleza ni marufuku.
Na miongoni mwa waliodai hili ni watunzi wa Kitabu cha [Al-mughniy: 3/220-221, Ch. ya Maktabat Al-Qahirah] na kitabu [Ash-Sharh Al-Kabiir: 3/500-501, Ch. ya Dar Al-kitab Al-Arabiy] wanasema: “Hakuna kosa kufanya Umra mara nyingi ndani ya mwaka mmoja, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Ali, Ibn Umar, Ibn Abbas, Anas, Aisha, Atwaa, Twawuus, Ikrimah, na Shafiy. Na walioona kuwa inachukiza kufanya Umra mara mbili kila mwaka: Al-hasan, Ibn Siriin, na Malik. Na An-Nakhi’iy anasema: Hawakufanya Umra kila mwaka isipokuwa mara moja, na Mtume S.A.W, hakufanya hivyo.
Lakini sisi tunaona kuwa: Bi Aisha alifanya Umra mara mbili ndani ya mwezi mmoja kwa mujibu wa amri ya Mtume S.A.W; Umra pamoja na Qiran, na Umra baada ya kumaliza Hija yake; na Mtume S.A.W, amesema: “Umra hadi Umra hufuta dhambi zilizotendwa baina yake”. Muttafaq. Na Ali R.A, alisema: mara moja ndani ya mwezi mmoja. Na Anas alikuwa akinyoa nywele za kichwa hutoka kwenda kufanya Umra. Na hayo yaliyopokelewa na Shafiy katika Musnad yake.
Na ikrimah amesema: Mtu atafanya Umra akiweza kuzikata nywele zake kwa wembe. Na Atwaa amesema: Mtu akitaka atatekeleza Umra mara mbili kila mwezi. Na kuhusu kufanya Umra zaidi ya mara moja na kuendeleza, hayo hayatakiwi kwa rai ya wazi tuliyoitaja kutoka kwa Wema waliotangulia. Hivyo Ahmad naye amesema: Iwapo Mtu atafanya umra, hana budi kunyoa au kupunguza nywele zake, na anaweza kunyoa kichwa chake ndani ya muda wa siku kumi. Na inafahamika kuwa haitakiwi kufanya Umra muda usio wa siku kumi.
Katika katika mapokezi ya Al-Athram anasema: Mtu akitaka atafanya umra kila mwezi. Na baadhi ya wenzetu wanasema: inatakiwa kufaya umra mara nyingi. Na kauli za Salaf na hali zao zinaonesha tulivyosema. Na kwa sababu haikunukuliwa na Mtume S.A.W., na Maswahaba zake kuendeleza kati yake, lakini kilichonukuliwa ni kuyakanusha hayo, na haki ni katika ufuasi. Na Twawuus anasema: Hao wanaotekeleza Ihramu katika (Tani’im), mimi sijui ikiwa watapata Ujira au wataadhibiwa? Na alipoulizwa: Kwa nini waadhibiwe?, akasema: kwa sababu waliacha Twawafu ya Kaaba, wakatoka umbali wa maili nne, wakarudi, na mpaka warudi masafa ya maili nne watakuwa na Twawafu mara mia mbili, na kila walipotufu Kaaba itakuwa bora zaidi kuliko kutembea bila faida”.
Na madai ya kutonukuliwa kuendeleza halifai iwe dalili ya kukataza; kwa sababu haimaanishi isipokuwa kutokuwepo dalili, na kutokuwepo dalili siyo dalili ya jambo la, kuwepo au kutokuwepo. Na miongoni mwa kanuni za kitaaluma zinazoamuliwa kuwa ni kitu muhali kuwepo Tawi pamoja na kutokuwepo Asili, na kuwepo hoja pamoja na kutokuwepo dalili; na kuwa pia kutonukuliwa siyo kutokuwepo, na hailazimiki kuwa kutonukulu ni kutokuwepo.
Na Ibn Al-Arabiy mfuasi wa Madhehebu ya Malik, kuhusu suala la kutonukulu kutoka kwa Mtume S.A.W, katika kitabu chake cha: [Ahkaam Al-Qura'an: 2/286, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] anasema: “uhakiki wake ni kutokuwepo dalili, na siyo kuwepo kwake”. Na kutokuwepo dalili kwa suala moja kunalifanya suala hili liwe na zuio la kiasili, na kuharamisha ni hukumu inayogeuza zaidi zuio hilo la kiasili, na kuhitaji dalili Maalumu, na kwa hivyo basi unaionaje dalili kwa ujumla inaonesha pia kwamba kujuzu kutakiwa, kama ilivyotangulia.
Na kudai kwamba alinukulu kutoka kwao kuwa wamekanusha, siyo sahihi, na kiko wapi hicho kilichonukuliwa? Hayo ni maneno matupu yasiyo na dalili, isipokuwa maneno ya Twawuus tu, yakilinganishwa na maneno ya waliojuzisha, mwanzoni mwa maneno yake. Na huu ni mwelekeo usio na uhakiki sahihi wa kitaaluma. Kwa sababu ikiwa inajuzu kufanya Ibada zaidi ya mara moja kwa uwazi, hivyo basi ni wazi kwamba inajuzu ifanywe Ibada hiyo mara nyingi na kuiendeleza, na tofauti kati ya hizi mbili inahitaji dalili ambayo haipo.
Vile vile, kazi inayotakiwa – kama ilivyotangulia kutajwa katika maneno ya Al-Hafidh – haikuainishwa katika matendo yake S.A.W.; kwa sababu Yeye S.A.W., alikuwa akiacha kutenda kitendo chochote alichotaka kukifanya kwa ajili ya kuepusha ugumu kwa Umma wake, na aliihimiza kwa tamko katika Hadithi zilizotangulia.
Na kwa mujibu wa maelezo hayo yaliyotangulia, na kuhusu uhalisia wa swali: Inajuzu na inatakiwa kwa mwenye kujistarehesha kabla ya kutekeleza Ihramu ya Hija, na kwa aliyemaliza mwendo wake wa kwanza, baada ya kurusha mawe, ndani ya Siku ya Pili ya Tashriiq, atekeleze Umra na anaweza kutekeleza Umra zaidi ya mara moja na kuendeleza kati ya masiku hayo. Na hii ni kwa mujibu wa Madhehebu ya wanazuoni wengi, miongoni mwa Salaf na waliowafuatia.
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas