Ukosefu wa vitendo na fikra sahihi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukosefu wa vitendo na fikra sahihi kwa wenye msimamo mkali

Question

Nini mwisho wa matendo bila ya kuwa na elimu na ufahamu katika dini?

Answer

Wanachuoni wametahadharisha kufanya matendo bila ya kuwa na muono na elimu, kwa sababu hilo hupelekea kuyumba kwa mizani ya vipaombele, kwani Imamu Al-Hassan Al-Basry amesema: “mwenye kutenda bila ya elimu ni kama mwenye kutembea njia isiyo sahihi, na mwenye kutenda bila ya elimu anayoharibu ni mengi zaidi ya anayotengeneza”.

Miongoni mwa sura za kuyumba kwa mizani kwa baadhi ni kuyapa umuhimu zaidi mambo ya Sunna kuliko ya lazima, kutangaliza matawi juu ya mashine, kuzipa umuhimu ibada za mtu peke yake zaidi ya ibada za wengi na yasiyokuwa hayo katika aina za kuyumba, na hali hizi hupelekea kupoteza muda na nguvu pamoja na kutengeneza matatizo na kuvunja mahusiano, haya ni tofauti na mfumo ambao umewekwa na Maimamu Waislamu, tunakuta Imamu Bukhari anaweka mlango katika kitabu chake cha Sahihi wenye jina: “Mlango wa elimu kabla ya kauli na matendo” na akataja humo kauli ya Mwenyezi Mungu: {Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu} Muhammad: 19. Na kauli ya Mtume S.A.W: “Mwenyezi Mungu anapomtakia mja kheiri humzindua katika dini” ili kusisitiza kwetu kuwa ufahamu katika dini na matendo vinajenga ufahamu salama na bora zaidi ya kufanya matendo moja kwa moja, kwa sababu kilichobora kupewa umuhimu ni ufahamu salama kisha kufanya matendo kwa sheria zake.

Uislamu umeweka mfumo wa kwenda kwa hatua nao ni mfumo unaonesha katika hatua za utungaji Sharia mbali mbali kama vile kuharamisha pombe kwa hatua nne, kuthibiti katika Jihadi mtu mmoja kwa wawili mpaka kumi, na yasiyokuwa hayo ili kutuwekea wazi sisi umuhimu wa kufahamu hali za watu na asili ya nafsi zao mpaka katika masuala ya utunguji Sharia na hukumu.

Share this:

Related Fatwas