Kusimama kwa maamuma pamoja na Ima...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusimama kwa maamuma pamoja na Imamu

Question

Kama akiwepo maamuma mmoja tu anasimama namna gani pamoja na Imamu?

Answer

Kwa mujibu wa Sunna kwa maamuma mmoja asimame upande wa kulia wa Imamu, na inapendekezwa awe nyuma yake kidogo ili Imamu apambanuliwe na yule maamuma. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abbas, (R.A), amesema: “Nililala katika nyumba ya Shangazi yangu Mama Maymunah (R.A) Mtume (S.A.W) Akaswali Ishaa kisha Akaswali Rakaa nne (4), kisha Akalala,kisha akainuka, nikasimama kushotoni kwa Mtume (S.A.W), kisha Mtume (S.A.W),  akaniweka upande wa kuliani kwake. (Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Mashiekh wawili Bukhari na Muslim).

Akisimama kushoto kwake au nyuma yake, inapendekezwa kuwa kisimamo hiki kirekebishwe, ni sawa sawa na maamuma au na Imamu, ikiwa Swala imekamilika kwa namna hii, pia ni sahihi na haibatiliki hata kidogo. Ingawa hali hii ni kinyume na iliyo sahihi zaidi.

Share this:

Related Fatwas