Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa Pamoja.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa Pamoja.

Question

Nimesikia mtu anasema: “Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja ni uzushi”, na ushahidi wake ni kwamba haikupokelewa kuwa Mtume S.A.W kafanya hivyo, na kanuni inasema: kuacha kupokelewa ni kupokelewa kwa kuacha, na dalili yake pia ni hadithi ya Aisha: "Atakayezusha katika Dini yetu yasiyokuwemo basi kitarudishwa (hakitokubaliwa kitendo chake)", na athari ya Ibn Masoud kuhusu kukataza kwake aliyewaona wakifanya hivyo. Mwenyezi Mungu amesema: {Leo nimekukamiliishieni Dini yenu} [AL MAIDAH 3], basi kukizusha kitu baada ya ukamilifu wake si miongoni mwa dini. Ni nini ukweli wa mtazamo huo?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sala na amani ziwe juu ya Mtume wetu, familia yake na masahaba wake. Ama baada ya hayo:
Aya zinazothibitisha kumtaja Mwenyezi Mungu ni jambo linalopendeza ni nyingi, nazo ni jumuishi yaani zinaeleza namna au jinsi ya kumtaja Mwenyezi Mungu, ikiwemo kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja. Mwenyezi Mungu amesema: {Basi nikumbukeni nitakukumbukeni,} [AL BAQARAH: 152]. Mwenyezi Mungu anasema pia: {Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala,} [AALI IMRAAN: 191]. Mwenyezi Mungu amesema pia: {Na wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.} [AL AHZAAB: 35]. Mwenyezi Mungu alisema aidha: {Enyi mlioamini! mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru, Na mtakaseni asubuhi na jioni} [AL AHZAAB: 41-42].

Na miongoni mwa hadithi za Mtume zinazoruhusu kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja ni zilizopokelewa na Bukhari kutoka hadithi ya Abu Huraira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema: "Mwenyezi Mungu ana Malaika wanatembea njiani wakitafuta watu wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu, wanapowakuta watu wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu wanaitana Njooni kwa mahitaji yenu, akasema: wanawazunguka kwa mbawa zao mpaka mbinguni, akasema: Mola wao akawauliza, naye anajua zaidi kuliko wao: wanasema nini waja wangu? Malaika Wakasema, wanakusifu, wakushukuru na wanakutukuza".

Kauli ya Mtume S.A.W: "Watu wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu", iko katika hali ya wingi, huonyesha kwamba wao wanamkumbuka (wanamtaja) kwa pamoja.

- Imepokelewa na Al-Tirmidhi kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A kwamba Mtume amesema: "Mtakapopita peponi, basi kaeni. Wakasema: ni nini pepo? Akasema: vikao vya kumkumbuka Mwenyezi Mungu".

Na “vikao” ni wingi wa “kikao”, na kikao cha watu ni: watu ambao wanakusanyika kwa kukaa duara, na mfumo unaotumika kumkumbuka Mwenyezi Mungu hali ya kuwa watu wamekusanyika inakuwa kila mtu anakaa katika kikao kwa kumtaja Allah peke yake au wanamtaja Allah kwa pamoja kwa sauti moja kwa kukubaliana. Na kama wanaokusanyika wakikaa kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kudhihirisha bila ya kuafikiana kunasababisha kutokea usumbufu ambao unaharibu kumtaja Mwenyezi Mungu, kwa sababu usumbufu huo unaharibu utulivu.

Tirmidhiy amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Said Al-Khudari kwamba Mtume, S.A.W. amesema: "Hakuna watu wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu ila malaika huwazunguka na huruma huwafunika na utulivu huwashukia na Mwenyezi Mungu huwataja kwa wale alionao".

Na kauli ya Mtume S.A.W: "Hakuna watu ambao wanamkumbuka Mwenyezi Mungu", yaani: wanakutana kwa ajili ya kumkumbuka kwa kumsifu, kumshukuru, kusoma Qurani, na kutafuta elimu ya kisheria, Al-Minyawi alisema katika kitabu cha [Faidhu Lqadeer 5/494, Al-Maktabatu Ltujariya]: “Hadithi hiyo inaashiria ubora wa vikao vya elimu, wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu, kukutana kwa ajili ya vikao hivi, na upendo wa malaika kwa wanadamu”.

Sheikh Ssideek Hassan Khan alisema katika kitabu cha [Nuzulu Al-Brar, uk. 17, Dar Al Maarifa]: “Hadithi hiyo inapendezesha kukutana kwa ajili ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, basi sifa nne kila moja zinahimiza shime ya wanaotaka na inakuza azma ya watu wema kwa ajili ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu”.

Katika riwaya ya Imamu Muslim, Mtume, S.A.W amesema: "Hawakusanyiki watu katika nyumba ya Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakasomeshana pamoja ila utulivu huwashukia, na rehma huwafunika na Malaika huwazunguka na Allah Huwakumbuka kwa wale walioko pamoja Naye".

Katika Hadithi hiyo kuna dalili ya kujuzu kukusanyika kwa ajili ya kusoma Quraani, na kusoma Quraani ni aina ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Wanachuoni wa madhehebu ya Shaafiy na Hanbali wanasema kuwa kusoma Quraani kwa pamoja inajuzu, pia Imamu Al-Nawawi amesema katika kitabu chake kinachoitwa [Al-Tibian fii Hamalat Al- Quraani, Uk. 56- 57, Dar Ibn Hazm]: “Ujue kuwa kusoma kwa pamoja inajuzu kwa dalili za wazi, vitendo vya watu waliotangulia, na watu waliokuja baada yao ... Ibn Abi Daud amesema kwamba Abu Al-Darda (R.A) alikuwa anadurusu Quraani akiwa pamoja na kundi la watu, wote wanasoma. Ibn Abi Daud alisema kwamba walikuwa watu wema miongoni mwa waliotangulia, waliokuja baada yao, na pia majaji waliotangulia walikuwa wakisoma pamoja”.

Katika riwaya ya Imamu Ahmad alipoulizwa kuhusu kukutana kwa watu kwa ajili ya kusoma au kuomba dua au kumkumbuka Mwenyezi Mungu alisema: “Ni kitu gani bora zaidi ya hayo”. [Kashful Qinaa 1/432, Dar Al-Kutub Al-Ilmiya.

Sheikh Ibn Taymiyyah katika Al-fatawa Al-Kubra 5/342, Dar Al-Kutub Al-Ilmiya] amesema: “kusoma kwa pamoja ni nzuri kwa wanachuoni wengi, na miongoni mwa aina za kusoma kwa pamoja ni kusoma kwa sauti moja, ingawa wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Malik wana mitazamo miwili kuhusu hukumu ya Makruhu juu ya jambo hilo”.

Imepokelewa na Muslim kutoka kwa hadithi ya Abu Saeed Al-Khudri kwamba Mtume, S.A.W. alitoka nje akakuta baadhi ya masahaba wake wanakaa pamoja, akasema: "Kwanini mmekaa pamoja? Wakasema: tumeketi kwa ajili ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa sababu ametuongoza kwa Uislamu na ametuneemesha kwake, akasema: haki ya Mungu, mmeketi kwa ajili ya jambo hilo tu? Wakasema: haki ya Mungu, tumeketi kwa ajili ya jambo hilo tu. Akasema: Mimi siapi mbele yenu kwa kuwatuhuma, lakini Jibril alinijia na aliniambia kuwa Mwenyezi Mungu anajivunia kwa ajili yenu mbele ya malaika".

Imepokelewa na Imamu Al-Bukhari kutoka kwa Abu Huraira R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Mwenyezi Mungu anasema: “Mimi ninakuwa katika dhana ya mja wangu, na mimi niko pamoja naye pindi anaponitaja, atakaponitaja katika nafsi yake nitamtaja katika nafsi yangu, na akinitaja katika kundi la watu ninamtaja katika kundi bora kuliko la watu hao, na akinikaribia kwa shubiri moja ninamkaribia kwa dhiraa, na akinikaribia kwa dhiraa ninamkaribia zaidi ya dhiraa, na akinijia hali ya kuwa akitembea nitamwendea hali ya kuwa ninakimbia".

Muradi wa kauli ya Mtume S.A.W. “kumtaja mja hadharani” ni kuwa kwake pamoja na kundi la waumini, au hadharani, na anaekuwa hadharani hazungumzi ila kwa sauti kubwa, na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa sauti iwao hao wanaomtaja hawakufanya hivyo kwa sauti ya pamoja basi hali hiyo ingelisababisha ushawishi kati yao kama tulivyoeleza hapo juu.

Mwanachuoni mkubwa anayeitwa Ibn Abideen katika kitabu chake [Durru L-Mukhtar 6/398]: “Imamu Al-Ghazali alifananisha mtu anapomkumbuka Mwenyezi Mungu peke yake, na kundi la watu wanapomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa Adhana ya pekee na ya pamoja, alisema: sauti za waadhini wingi zinakata mbuga zaidi hewani kuliko sauti ya muadhini mmoja, hali kadhalika, kundi la watu wanapomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa sauti moja wanaathiri zaidi kuliko mtu mmoja”.

Katika swali la fatwa, muulizaji alitaja baadhi ya pingamizi, kwahivyo tunazijibu kama ifuatavyo:
Mtume S.A.W ameacha swala la kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa pamoja, na kuacha katika lugha maana yake ni: kuepusha kitu fulani, Ibn Faris amesema: “kuacha kitu: kukiepusha” [Mu’jam Maqaayiis Al-Lugha 1/345, Dar Al-Fikr].


Inasemekana: kuacha jambo fulani, yaani kujuepusha: na imepokelewa katika hadithi: "Wasiohudhuria Sala ya Ijumaa wabadilishe mtindo wao huo laa sivyo Allah S.W. Atawapiga mihuri katika nyoyo zao na watakuwa miongoni mwa walioghafilika." [Imepokelewa na Imam Muslim]. Na kauli yake: "na wabadilishe mtindo wao huo", yaani: waache ada mbaya hiyo.

Kuhusu maana ya kitenzi cha “kuacha” Sheikh Al-Attar alisema: “maana yake ni kuacha kufanya kwa makusudi yanayowezekana au bila ya makusudi, kama katika hali ya kughafilika au ya kulala, iwe mtu alikumbwa na kinyume chake au la. Ama kuhusu kutoyafanya yale tu asiyokuwa na uwezo nayo haimaanishi ni kuacha, kawa hivyo, hatuwezi kusema: mtu amecha kuumba miili”. [Hashiat Al-Attar ala sharhu ljawami’i Naklan an Sharhu lwaqfu 1/280, Dar Al-Baz].

Basi kitenzi cha kuacha kinamaanisha: kutofanya jambo fulani, yaani kuacha jambo fulani bila ya kukusudia, nalo halikusudiwa kuigwa, basi haimaanishi kujuzu wala kuchukiza wala kuharamisha.

Ama kutofanya jambo fulani baada ya nafsi kuielekeza, na haiwi ila kwa makusudi tu, na hali hiyo inaitwa kuacha jambo fulani kwa makusudi, ambayo ni kuepusha kitu fulani baada ya kuelekea kwake.

Al-Shbramalsy alisema katika [Hashiyatih ala nihaayatul muhtaj]: “Maana ya kuacha kitu fulani ni: kuizua nafsi siyo kutokifanya, kwa sababu kutofanya siyo hali ya kukalifishwa”. [1/390. Dar Al-Fikr].

Wasomi wa elimu ya Uswuul wanasema kwamba kuacha kitu fulani kwa makusudi ni kitendo miongoni mwa vitendo, lakini kuacha kitu hakuonekani kama kufanya kitu, kwani kuacha kitu ni jambo ambalo siyo la kuwepo, kinyume cha kufanya kitu fulani ambalo ni jambo la kuwepo, basi haisihi kuingia kuacha katika vitendo vya waziwazi kwa kufanya kama dalili.

Basi kuacha kitu kwa makusudi ikiwa hakuna dalili ya kwamba kitu hiki kinachoachwa ni haramu au Makruhu, basi haiwi hoja, bali lengo lake ni kuruhusu kuacha kufanya, ama kitendo kinachoachwa kinakuwa ni marufuku, basi kuacha peke yake hakunufaishi, lakini hunufaika kwa kutoka dalili inayoonyesha hivyo.

Imamu Al-Jassas anasema: “Kila tulipoona Mtume S.A.W. ameacha kufanya kitu, bila ya kujua kwa nini amekiacha, tulisema: kuacha kwake kunamaanisha ruhusa, si wajibu kwetu, lakini inapothibiti kwetu kwamba ameiacha kwa sababu kuifanya ni dhambi, basi inabidi tuiache kwa sababu hiyo hiyo, mpaka ielezwe dalili kwamba jambo hilo halituhusu sisi” [Al-Fusul fi Al-Usuul 3/228, Wizara ya waqfu ya Kuwait].

Imamu Ibn Daqeeq akichangia aliyoyapokea Bukhari na Muslim kutoka kwa Ibn Omar R.A. anasema: "Mtume S.A.W. alikuwa akisali katika safari yake juu ya ngamia ambapo popote anapoelekea alikuwa akisali sala ya sunna na sala ya witri isipokuwa sala za faradhi", katika riwaya nyingine: "Alikuwa akisali sala zote isipokuwa sala za faradhi tu" na kauli yake: "Alikuwa akisali sala zote isipokuwa sala za faradhi tu" inawezekana kuchukuliwa kwamba sala za faradhi hazisaliwi juu ya ngamia, lakini maoni hayo hayana nguvu kama ni dalili, kwa sababu hali hiyo haina isipokuwa kuacha kuifanya tu, siyo kuacha pamoja na dalili ambayo inathibitisha kukatazwa, na maoni hayo hayo katika kauli yake "isipokuwa sala za faradhi tu", yanaonyesha kuondoka kitendo hiki, na kuacha kitendo hakuonyeshi kukukatazwa kama tulivyotaja”. [Ihkam Al-Ahkam 1/211, Matbaat Al-Sunna Al-Muhamadiya].

Imamu Ibn Qudaamah Al-Hanbali ametaja kutoafikiana kwa wanavyoni kuhusu suala la kukausha viungo kwa kitambaa baada ya kutia udhu, au kuoga, ambapo wanavyuoni wametoa dalili inayothibitisha kukausha viungo ni Makruhu, iliyopokelewa katika sahihi ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Maimuna kuwa amempa Mtume S.A.W kitambaa baada ya kutia udhu, basi hakukirudisha lakini amekumuta maji kwa mkono wake, akawajibu kwa kusema: “Na kuacha Mtume S.A.W. hakumaanishi Makruhu, kwa sababu Mtume S.A.W. anaacha na anafanya jambo la Mubah”. [Al-Mughni 1/95, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi.]

Dalili ya kimsingi ya wale wanaoona kwamba kuacha kufanya kwa sababu ya uharamu au kuchukiza kwa kitendo ni kwamba: masahaba wa Mtume hawakupokea mambo ambayo kama Mtume aliyafanya, basi wangelikuwa na hamu ya kuyapokea, na hali hiyo ilivyo ni masahaba kupokea mambo yaliyoachwa na Mtume S.A.W. Na kwa kuwa hakuna hata mmoja wa masahaba aliepokea mambo hayo kabisa, wala kuyasema, basi inajulikana kwamba mambo hayo hayapo, na kutokana na hivyo, basi kila kinachokuwa hakikupokelewa kuwa Mtume alikifanya, basi amekiacha, na kitu hiki kinachukua nafasi ya matini katika hukumu yake.

Na matokeo ya mtazamo huo ni kuzuia kuchukua matini jumuishi kama zilivyo ili ziwe pamoja na mambo ambayo hayakupokelewa na Mtume S.A.W. pia ni pamoja na kuzuia kukisia katika hali hiyo, na kutokana na hayo, hairuhusiwi kuchukulia ujumla wa Quraani au hadithi mpaka itakapotufikia kwamba Mtume S.A.W. amelifanya jambo hilo.

Unaonekana ubatilifu wa muulizaji na mtu yeyote mwengine, kwa msingi wa: “kuacha mapokezi ni kupokea kuacha”. Na masharti matatu yaliyotajwa katika swali lile kwa kutaja tawi moja la kifiqhi, jamhuri ya wanazuoni haijaufuata msingi huu wala masharti haya yanayodaiwa kuwepo, nayo ni katika orodha ya vitu viotavyo ardhini ambavyo havina zaka

Mtume S.A.W. alikuwa akichukua Zaka ya vitu vinne tu miongoni mwa vitu vinavyotoka ardhini, navyo ni tende, zabibu, shairi, na ngano, na haikupokelewa kutoka kwa Mtume kwamba alichukua Zaka ya visivyokuwa hivyo. [Imepokewa na Al-Tabarani na Al-Hakim]. Kwa hivyo, ikiwa kuacha kupokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. ni kupokelewa kwa kuacha, basi itakuwa hakuna Zaka isipokuwa katika aina nne hizo tu; kwa sababu haikupokelewa kwamba Mtume S.A.W. amechukua kutoka vitu vingine zaidi ya hivyo. Pia kwa sababu masharti matatu yanakuwepo, na kwamba Mtume S.A.W. alikuwa ana uwezo wa kuchukua Zaka kutoka kwa wakulima wa matunda, mboga na vitu vingine kutoka wakulima wa Madina na jirani zake, lakini hakufanya hivyo, na hakuwauliza Zaka.

Pia haja ilikuwepo, kwani Mtume S.A.W aliubainishia Umma wake vinavyotakiwa kutolewa Zaka, na kama kuna jambo la maslahi ya kisheria angelifanya Mtume saw, kwahiyo kama hakulifanya na haikupokewa kauli yake katika jambo hilo hujuulisha kutojuzu. Pia hakujadhihiri kizuizi cha kuacha kwake.

Lakini wanavyuoni wengi pamoja na wenye madhehebu maarufu wamechukua yaliyomo katika ujumla wa kauli ya Mwenyezi Mungu: {na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi.} [ALBAQARAH: 267], na kauli ya Mtume S.A.W.: "Mimea inayonyeshewa na mvua na chemchem, Zaka yake ni sehemu moja katika kumi, na inayotiliwa maji mpaka ikamea Zaka yake ni nusu ya sehemu moja katika kumi". [Imepokelewa na Bukhari kutoka kwa Abdullah bin Omar, na wakafanya Zaka katika aina nyingine, sio tu katika zile zilizotajwa katika hadithi, licha ya hitilafu baina yao katika swala hilo.

Abu Hanifa anaona Zaka ni wajibu katika mimea yote inayotolewa ardhini kwa makusudi ya kustawi. [Tibiyan Al-Haqaiq 1/291, Dar Al-Kitabul Islamiy].

Na Imamu Malik: Zaka ni lazima katika ngano, shairi na nafaka nyingine zinazoliwa, lakini Zaka haichukuliwi katika matunda isipokuwa tende na zabibu. [Sharhu Mukhtasar Khalil Li Khurashi 2/167 Daru lfikr].

Imamu Shaafiy: Zaka ni lazima katika mazao na matunda yanayoliwa. [Mughni Al-Muhtaj 2/81, Dar Al-Kitab Al-Ilmiya.

Imamu Ahmad: Zaka ni lazima katika vyote vinavyotoka nje ya ardhi ambavyo vinapimwa na vinawekwa kama akiba. [Sharhu Muntaha Al-Iradat 1/413, Alam Al-Kutub].

Ikiwa kauli ya anayedai kuwa kuacha kupokelewa ni kupokelewa kwa kuacha ndio sahihi pamoja na kuchukua masharti haya matatu basi kauli ya wanaosema kuwa wajibu wa Zaka ni katika vyote vinavyoliwa na wafanyakazi wanavihifadhi inapinga yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume saw, na hali hii haikubaliki.

Na vitendo vya Mtume S.A.W. kwa baadhi ya watu havimaanishi kwamba jambo hilo linaruhusiwa kwao wao tu bila ya watu wengine, na pia Mtume saw kuacha jambo fulani hakumaanishi kutojuzu kwake.

Dalili ya uhalali wa kumtaja Mwenyezi Mungu inapatikana katika hali zote ikiwa katika hali ya upweke au katika hali ya pamoja, na anayehusisha na hali fulani inapasa alete dalili yake, au itakuwa miongoni mwa uzushi wa kidini kwa sababu anaharimisha yaliyohalilishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W. Inaruhusiwa kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kudhihirisha pamoja na wenzake wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu katika wakati unaofaa kwa kutekeleza masharti yote, na pia inaruhusiwa kumtaja Mwenyezi Mungu kwa njia nyingine, na njia hiyo haipungui katika malipo, lakini mwenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu anaweza kuichagua njia ambayo inafaa na shughuli zake na kumsaidia kufikia madhumuni yake kupitia kumkumbuka Mwenyezi Mungu, basi kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja, na tofauti ipo katika hali ya pamoja au hali ya upweke na ikiwa kwa kudhihirisha au laa. Na hakuna dalili yoyote inayozuia kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kudhihirisha au kwa pamoja.

Mambo kama hayo siyo miongoni mwa yaliyoachwa na Mtume S.A.W. lakini mambo hayo yamepokelewa katika hadithi zake kama ilivyotangulia hapo juu.

Ama kuhusu kauli yake juu ya msingi unaosema: kuacha yaliyoachwa na Mtume na hairuhusiwa kuyafanya kwa mujibu wa hadithi iliyopokelewa na Bukhari na Muslim kutoka Bibi Aisha R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Atakayezusha katika mambo yasiyokuwa yetu basi kitarudishwa", ni dalili isiyofaa hapa; kwa sababu hadithi hiyo inaonyesha kwamba atakayezusha na kuingiza itikadi na matendo mapya katika dini ya Kiislamu au mambo ambayo hayana dalili za wazi katika Quraani au Sunna, basi mambo hayo yaliyozushwa yatarudishwa kwake, yaani mambo hayo ni batili, lakini kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja kuna dalili kutoka Quraani na Sunna.

Al-Hafidh Ibn Hajar amesema: "maana ya hadithi hiyo: Atakayezusha katika dini jambo ambalo halina msingi, basi halitaangaliwa jambo hilo".

Na maana ya hadithi hiyo ni kwamba atakayezusha jambo jipya katika dini, na jambo hilo lina dalili ya wazi au siyo ya wazi katika Quraani na Sunna basi halitarudishwa kwake. Ibn Rajab amesema: (Hadithi hii inaonyesha kwamba amali yoyote isiyofuata amri ya Mwenyezi Mungu haikubaliwi. Na inaonyesha pia kwamba amali yoyote inayofuata amri ya Mwenyezi Mungu inakubaliwa, na maana ya amri hapa ni dini na sheria yake). [Jamiil Uluum wa Al-Hikam uk. 119, Muasasatu Risala].

Imamu Al-Nawawi anaeleza maana ya uzushi katika sheria akisema: "Ni kuzusha kile ambacho hakikuwepo wakati wa Mtume SAW, na kuna aini mbili za uzushi, mzuri na mbaya". [Tahdhibu Al-Asmaa wa Al-Lughat 3/22. Dar Al-Kutub Al-Ilmiya].

Imepokelewa na Al-Bayhaqi kutoka kwa Imamu Shaafiy R.A, alisema: "uzushi ni aina mbili: moja ni uzushi unaopingana na Quraani au Sunna au maneno ya masahaba au makubaliano ya wanavyoni, nao ni uzushi batili. Pili: ni uzushi mwema ambao watu wote hawatofautiani juu yake, nao ni uzushi siyo mbaya". [Manaqib Al-Shafii 1/469, Maktabtu Dar Al-Turath].

Saad Al-din Al-Tiftizani alisema: "Ni ujinga kujaalia kila jambo ambalo halijakuwepo wakati wa masahaba kuwa uzushi mbaya, hata kama hakuna dalili inayothibitisha ubaya wake, kwa mujibu wa kauli ya Mtume SAW: "Jihadharini kuzusha mambo mapya". Na huyu anayejaalia hivyo hajui kwamba madhumuni ya hadithi ni kujaalia katika dini ya Allah S.W. mambo yasiyokuwemo ndani yake. [Sharhul Maqasid 5/232, Dar Al-Maarif Al-Numaaniya].

Na hakuna mwanachuoni yoyote aliyesema kwamba uzushi unagawika kwa kweli na ziada isipokuwa Al-Shatibiy, na kauli yake inakubalika, lakini kwa mtazamo wetu, uzushi hauwi isipokuwa katika kweli tu. Na amali zikiingizwa katika asili moja inaonyesha kuruhusiwa kwake, basi hakuna vibaya katika kuzitekeleza amali hizo kwa njia yoyote, au hali inayokubalika kisheria hata jambo hilo halikupokelewa kutoka kwa Mtume SAW, na katika hali hiyo, amali hizo sifa zake hazibadiliki hadi ziwe kama uzushi wenyewe.

Ama kuhusu yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Masuod juu ya ubaya wa mambo hayo hayajuulishi hukumu jumuishi. Na riwaya za athari ambazo zilieleza asili ya hadithi zinaonyesha kuwa hadithi hiyo ni moja tu, ambapo Ibn Masuod aliwakataza watu waliokuwa wakimsabihi Mwenyezi Mungu msikitini kwa pamoja, na dalili hiyo ina maana kwamba Ibn Masuod alikataza kwa sababu anaogopa watu hawa kujifakharisha, au kudhani kuwa wao ni waongofu kuliko masahaba, au wanaelekea kupinga waislamu katika tabia zao au madai yao kwamba wao wanafanya bidii zaidi na wanamcha Mwenyezi Mungu zaidi kuliko wengine.

Amru Ibn Salamah alisema katika hadithi ya Al-Daramiy: "Tuliwaona watu hawa wakitupiga vita pamoja na Al-Khawarij katika siku ya Al-Nahrawaan".

Hiyo inaonyesha kwamba watu hawa walikuwa wakijulikana kwa ukali wao na kupingana na waislamu, na Abdullah Ibn Masuod na wanaofanana naye walikuwa wakiona watu hawa walikuwa na sifa za Al-Khawarij ambao Mtume Muhammad SAW aliwaonya.

Ufafanuzi huo wa juu unaondosha kauli inayosema hadithi ya Abdullah Ibn Masuod inapinga vikao vya pamoja vya kumdhukuru Allah S.W.

Al-Suyuti alisema katika kitabu cha Al-Hawi lilfatawa [1/394, Dar Al-Fikr]: "Ukisema kwamba: imepokelewa kutoka kwa Ibn Masuod kwamba aliwaona baadhi ya watu wanamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa sauti katika msikiti, akasema: nyinyi ni wazushi, akawafukuza nje ya msikiti. Nitasema: hadithi hii kutoka kwa Ibn Masuod inahitaji kuhakikiwa mapokezi yake, na nani ameipokea miongoni mwa maimamu katika vitabu vyao, na kama ikithibitika, itapingana na hadithi nyingi thabiti zilizotangulia. Kisha imepokelewa kutoka kwa Ibn Masuod kwamba amekataa hivyo kwa mujibu wa kauli ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal anaposema katika kitabu cha Al-Zuhd kwamba: imepokelewa kutoka kwa Amer Ibn Shafiiq kutoka kwa Abu Wael akasema: Wale wanaodai kwamba Abdullah Ibn Masuod alikuwa akikataza kumkumbuka Mwenyezi Mungu, basi sikukaa na Abdullah katika kikao ila alikuwa akimkumbuka Mwenyezi Mungu".

Al-Alusi alisema katika kitabu cha [Roho Al-Maani 16/163, Dar Al-Kutub Al-Ilmiya]: "na kuhusu yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Masuod kwamba aliwaona baadhi ya watu wanamtaja Mwenyezi Mungu kwa sauti msikitini, akasema: nyinyi ni wazushi, akawafukuza nje ya msikiti. hadithi hii si sahihi, na kama ikithibitika, itapingana na hadithi nyingi zilizopokelewa kutoka kwa maimamu wengi zinazothibitisha kwamba Ibn Masuod mwenyewe alikuwa akimkumbuka Mwenyezi Mungu kwa sauti ya wazi".

Na mwuulizaji wa fatwa hii alitaja aya: {Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu} [AL MAIDAH: 3] kama ni dalili kwamba mambo ambayo hayakutufikia –kama vile kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa pamoja- kutoka kwa Mtume SAW. basi mambo hayo siyo miongoni mwa mambo ya dini, basi mtazamo wake huo si sahihi.

Ufahamu sahihi wa aya: Mwenyezi Mungu ndiye anayethibitisha hukumu ya kisheria peke yake, hakuna tofauti kati ya wanavyuoni kuhusu jambo hilo, basi hukumu ya kisheria ni maneno ya Mwenyezi Mungu yanayohusu vitendo vya waja wanaotakiwa kuitekeleza hukumu hii au kuichagua, na kujua hukumu hizo kwa kupitia Quraani au Sunna au makubaliano ya wanavyuoni au kipimo, ama kwa dalili ambazo wanavyuoni wamehitalifiana nazo, kama vile manufaa ya kijamii na kadhalika, na dalili za kisheria zinabainisha hukumu za Mwenyezi Mungu bila ya wasiwasi.

Mwenyezi Mungu amebainisha hukumu za matukio yote, na matini hazikujumuisha hukumu za matawi yote kwa urefu, na hukumu nyingi za kisheria hazikutajwa katika Quraani na Sunna kwa uwazi sana, na jukumu la mwanafiqhi hodari linajitokeza katika hali hii ili aeleze uhusiano kati ya dalili na hukumu, na anaeleza hoja ya dalili kwa ajili ya kubainisha hukumu yenyewe, basi anajitahidi kufahamu matini kwa ajili ya kuitekeleza katika hali zote, au anajitahidi kuzielewa hukumu kutoka misingi jumuishi iliyomo katika sheria, au anajitahidi kuambatana na hukumu ambazo hazikutajwa kwa uwazi, na hukumu zinazotajwa kwa sababu upo uhusiano baina yao, na hiyo ni hoja iliyoeleweka kutoka matini.

Imamu Abdullah Ibn Masuod mwanachuoni mkuu wa sheria alisema katika kitabu chake Al-Tawdhih: “Hakuna shaka kwamba hukumu zinazothibitishwa waziwazi kupitia Wahyi kuhusu matukio yatokeayo ni chache sana, basi kama hukumu za matukio hayo hazikujulikana kupitia wahyi, na hukumu zikawa zinapuuzwa basi dini haitakuwa kamili, ni lazima wanavyuoni wenye kujitahidi watohoe hukumu hizo kupitia wahyi”. [Al-Talwiih Sharhul Tawdhiih 2/100, Dar Al-Kutub Al-Elmiya].

Ukamilifu wa dini haizuii kujitahidi, na wanavyuoni hawakuelewa kutokana na aya hii kwamba Mwenyezi Mungu amewazuia kujitahidi na kutohoa, bali wameelewa kwamba Quraani na Sunna zinakusanya misingi ya itikadi, hukumu na sheria ya kujitahidi, na masahaba walijitahidi katika masuala ambayo hayana matini za kisheria. Miongoni mwa jitihada hiyo ni kwamba Omar bin Khattab amemfukuza Nasr Ibn hajaaj akichelea kuhofia kufitinishwa Waislamu, na kuchoma misahafu ambayo iko kinyume na Masahafu wa Othman ili kuondosha fitna na ugomvi baina ya Waislamu, na Ali amewachoma Zanaadiqa ambao walijidai uungu, na aidha yapo masuala mengi masahaba wamejitahidi kwa mujibu wa kuelewa misingi jumuishi na malengo ya sheria.

Wanaokanusha kupima wamechukua aya hii kama dalili ya ubatili wa kipimo katika wakati wote baada ya Mtume SAW, Al-Sobki alijibu akisema: “jambo la kimsingi ni kutoainisha wakati maalumu, pia hakuna mtu yeyote anasema kwamba kipimo kilikuwa hoja mpaka kushuka kwa aya hii kisha kikatoweka, na maana ya kauli yake: {Leo nimekukamilishieni Dini yenu} yaani misingi, ama kuhusu matawi ya dini, basi aya hii haijaeleza matawi yoyote. Pia unaweza kujibu kwa kusema kwamba: maana ya kauli yake: {Leo nimekukamilishieni Dini yenu} yaani taarifa zote zinazohitajiwa katika dini, na aya hii ni jumuishi kwa mujibu wa maoni hayo.

Basi taarifa hizo zinawezekana ziwe katika hali ya moja kwa moja kama katika kuainisha, na inawezekana ziwe katika hali isiyo ya moja kwa moja.

Kwa nini mlisema “hayapatikani hayo isipokuwa taarifa inapokuwa bila ya msaidizi? Na katika hali hii kutekeleza kipimo hakupingani na ukamilifu wa dini, bali itakuwa miongoni mwa ukamilifu wa dini na haihitaji aya maalum, lakini itabaki kwa ujumla tu” [Al-Ibhaj fi Sharhil Minhaj 6/2197: 2199, toleo la 1, Darul Buhuth Lel-Derasaat Al-Islamiya wa Ihyaa Al-Turath].

Maana ya aya hii ni ukamilishajj wa misingi ya dini, na miongoni mwa misingi hii ni kujuzu kuleta uzushi mzuri. Anayezusha haimaanishi kuwa kazi yake imeongeza kitu katika dini, au amurekebisha upungufu uliopo katika Sheria, au ameyafuata matamanio yake, au ametunga sheria kwa akili yake, bali inamaanisha ni utekelezaji wa msingi wa Quraani na Sunna .

Kwa hiyo, vikao vya kumkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja ni Sunna inayopendeza, na imethibitishwa na masahaba na wanavyoni waliowafuata, na jambo hilo limepitishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., ama kuhusu pingamizi hizi ambazo hazina faida yoyote, tumezijibu hapo juu katika fatwa hii.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas