Kulingania kwa ajili ya Mwenyezi Mu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulingania kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu

Question

Ipi njia sahihi ya Kisharia ya kuelezea Uislamu kwa watu? je kwa njia ya Jihadi au njia ipi?

Answer

Wanachuoni wa Sharia wameelezea kuwa wakati wowote Waislamu wanapotekeleza jambo la lazima ya kutosheleza ikiwa ni pamoja na kuziba mianya na kulinda mipaka ya nchi za Kiislamu basi kulingania kunatosha bila ya jihadi ya kushambulia nchi za Waislamu, bali wakati wowote ulinganiaji unapokuwa mzuri hakuna haja ya kukimbilia kwenye Jihadi, na kuuwa wasio Waislamu sio makusudio, na Jihadi ni njia na wala sio kusudio lenyewe, wakasema: “Wajibu wa Jihadi ni wajibu wa njia na wala si makusudio, ambapo makusudio ya kupigana vita ni uongofu, ama kuuwa makafiri sio kusudio hata kama itawezekana kuongoa kwa kuwapa dalili isiyokuwa Jihadi ni bora zaidi ya Jihadi”.

Msingi wa kumlingania mwingine na kushirikiana naye ni huruma na upole kwa hali yake, ambapo Mwenyezi Mungu Anasema akimwambia Mtume Muhammad S.A.W.: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} Al-Anbiyaai: 107. Maelezo haya ya Qur`ani kwa upana wake mkubwa ambao unakusanya sehemu zote wala hayahusishi sehemu moja bila ya sehemu nyingine, wala wakati kwa urefu wake na vizazi vyake vinavyofuatana, wala hayahusishi zama bila ya zama zingine, na hali zote za amani na vita wala hayahusishi hali bila ya hali nyingine, na watu  wote Waumini wao na makafiri wao Waarabu wao na wasio Waarabu wala hayahusishi kundi bila ya kundi lingine, ili kumfanya mwanadamu mwenye kuzingatia katika ukubwa wa wasifu wa Qur`ani wa ukweli wa Mtume Bwana wa watu wa mwanzo na wa mwisho: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} Al-Anbiyaai: 107. Rehema jumla inayokusanya wote, mandhari yake yameenea katika hali zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwa ulimwengu na watu wanaomzunguka.

Share this:

Related Fatwas