Maana ya kuzuia umwagaji damu katik...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya kuzuia umwagaji damu katika Uislamu

Question

Ni nini maana ya kuzuia umwagaji damu katika Uislamu, na ni nini sababu za kuwajibisha kinga hii?

Answer

Kuzuia umwagaji damu katika Uislamu humaanisha kuzilinda kwa mujibu wa Sharia, kanuni na desturi za jamii husika, ambapo kulinda damu zisimwagike isipokuwa kwa haki ni miongoni mwa malengo na makusudio makuu ya Sharia ya kiislamu, kwa hivyo damu hazimwagiki kwa jina la kutekeleza maagizo ya Sharia, bali anayefanya hivyo hustahiki adhabu kubwa zaidi duniani na akhera, kwani kufanya hivyo ni dhambi mojawapo madhambi yaliyo kubwa zaidi, Mtume (S.A.W.) amesema: "Kwa hakika dhambi iliyo kubwa zaidi ni kumshirikisha na kitu katika ibada pamoja na Mwenyezi Mungu na kuua nafsi" (Imekubaliwa na Maimamu wote), hivyo, Sharia ya kiislamu inalinda damu na kutunza utukufu wake kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Walamsiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini" [Al-Ana'am: 151]

Kwa hakika, Uislamu umekuja kwa ajili ya kulinda haki, kueneza amani na usalama, kuzuia umwagaji damu, mali na heshima zisikiukwe pasipo na haki, kwa hiyo yeyote anayepuuza kuzuia umwagaji damu sawa za Waislamu au za wasio waislamu huwa anapinga mafunzo ya Sharia ya kiislamu.

Share this:

Related Fatwas