Ukweli wa jihadi katika Uislamu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukweli wa jihadi katika Uislamu.

Question

Je imefikiwa hali ya kuzuiliwa ulazima wa jihadi katika zama za sasa, kisha kuna ulazima wa kuirudisha tena? Na nani anaweza kufanya hilo?

Answer

Jihadi ni jambo la lazima haliwezi kukwamishwa na kuzuiliwa, na ulazima huu una vigezo vyake vilivyowekwa na kuainishwa na viongozi katika Umma wa Kiislamu, jambo si kwamba limeachwa tu kwa kila mtu, na vigezo hivyo Wanachuoni wamevitaja kwenye vitabu, ikiwa havitafanyiwa kazi vigezo vyake na makusudio yake ya Kisharia wakati huo haitaitwa Jihadi, bali inakuwa uharibifu au usaliti na uhaini, kwani si kila vita huitwa Jihadi.

Kile kinachofanywa na vikundi na harakati za misimamo mikali ndani ya nchi za Waislamu ikiwa pamoja na mauaji, au wanayoyafanya kwenye nchi za Waislamu ikiwa pamoja na vitendo vya kujitoa mhanga, au visivyokuwa hivyo miongoni mwa vitendo vya uharibifu vinavyotokana na kufuata mfumo wa upotoshaji ni haramu Kisharia, na uhalifu wa kibinadamu na kisheria, na haya yote yanaelezea aina ya uovu ambao unapaswa kuondolewa kwa nguvu, imekuja katika maandiko ya Sharia Takatifu amri ya kupambana na hali hiyo na kuwashambulia watu wake ikiwa hawataacha vitendo hivi viovu ambavyo vinaathiri ulimwengu mzima kwa Waislamu na wasio Waislamu.

Ama matendo wayafanyayo kuita Jihadi hiyo ni aina ya udanganyifu na kuwaongopea watu wenye udhaifu wa akili ili kuwakinaisha na huu uharibifu, na watu wake wanazingatiwa ni waovu wanastahiki kupigwa ili kuacha uovu wao.

Share this:

Related Fatwas