Maana ya kuhama katika Uislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya kuhama katika Uislamu

Question

Upi mtazamo wa Kidini wa maana ya kuhama? Na je kwa mwenye kuishi nchi za Kiislamu anapaswa kuhama kwenda nchi zingine kwa sababu ya dini yake kama inavyoelezwa na watu wenye msimamo mkali?

Answer

Mawimbi ya msimamo mkali na ugaidi yamefikia kiwango cha kughushi kwa watu maana ya kuhama na kulazimisha kwa kila mwenye kuishi kwenye nchi za Waislamu kuondoka nchi hizo na kwenda nchi nyingine, hilo ikiwa ni kukimbia kwa ajili ya dini yao na kulinda imani yao, na hilo linafanyika chini ya maana kuhama ya Kisharia katika Uislamu kama wanavyodai.

Ukweli ni kuwa kuhama ni elimu ya kubadilisha hali iliyopo na kwenda iliyobora zaidi kwa lengo la kufikia ushirika wa kijamii kiroho na kimwili, huenda maana hii ndio ambayo ameikusudia Mtume S.A.W. baada ya ufunguzi wa Makka, pale aliposema: “Hakuna kuhama baada ya ufunguzi wa mji wa Makka, lakini kuna jihadi na nia” Imepokewa na Muslim.

Kwa maana baada ya ufunguzi wa Makka hakuna kinachowajibisha kuhama mji au nchi, bali kunapatikana kinacholazimisha kuhamisha fikra kutoka fikra potofu na kwenda fikra iliyo bora zaidi, uharibifu na kudumaa kulikothibitika kusababisha kile tunachofikiri au kuona kuwa ni wema na mabadiliko, kutoka kwa Abdillah Ibn Amr Ibn Aas R.A Mtume S.A.W. amesema: “Muislamu ni yule Waislamu wanasalimika na ulimi wake pamoja na mikono yake, na mwenye kuhama ni yule mwenye kuyaacha yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu” imepokewa na Bukhari.

Share this:

Related Fatwas