Maana ya kuomba msaada
Question
Nini maana sahihi ya Kisharia kuomba msaada kutoka kwa Mawalii na waja wema?
Answer
Maana ya Kisharia ya kuomba msaada kutoka kwa Manabii na waja wema ni kuonekana kuwa kwao ni sababu ya kunufaika, kama vile miongoni mwetu mtu akataka msaada kwa daktari ili kupona kutokana na maradhi, bila ya kufikiria kupata ponyo kutoka kwa Muumba katika hali hiyo au kuleta taathira ya kupona kutokana na maradhi, lakini ni kwa njia ya kutaka msaada ni miongoni mwa mlango wa kuchukuwa sababu na kuwataka watu wenye weledi, vile vile Mawalii na waja wema Mwenyezi Mungu Amewafanya kuwa ni sababu ya watu kuongoka na mafanikio ya hali zao na malezi yao, ili wawe nje ya dhambi ya wazi na ya ndani, kama ilivyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Na acheni dhambi zilizo wazi na zilizofichikana} Al-An’aam: 120, wao ni watu wa waledi na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyasimamisha miongoni mwa ulinganiaji wa wito wake na kuhudumia Waislamu, hakuna tofauti katika hilo kati ya waliohai miongoni mwao na waliofariki, kwani wote hawawezi kuleta manufaa wala madhara kwa nafsi zao, bali kwa kuwa kwao sababu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuomba msaada kwao ukweli ni kumuomba Mwenyezi Mungu Atupatie yale aliyowapa Mawalii wake na waja wake wema, na atufanyie mambo ya kheri kwa sababu yao na kwa mikono yao, ikiwa ni kuwakarimu kwa sababu ni vipenzi vyake na waja wake na ukaribu wao kwao, haya ni yaliyofanywa na Waislamu waliotangulia na waliopo miongoni mwa Masahaba na Taabiin pamoja na Taabii Taabiin, hakuna mazingatio katika hilo kwa aliyetofauti na maana hii au kuipinga.