Masharti ya kufanya jitihada

Egypt's Dar Al-Ifta

Masharti ya kufanya jitihada

Question

Ni nini maana ya jiithada, yapi masharti yake?

Answer

Jitihada hurejelea dhana ya kufanya juhudi za kupata elimu au kufikia jambo fulani, hapa katika muktada huu hurejelea kufanya juhudi za kuainisha hukumu inayokubalika kulingana na dalili zatokanazo Qur`ani na Sunna kwa ajili ya kuunda hukumu za kisharia na kuzipitishia hali halisi na matukio ya maisha, kwa lengo la kuhakikisha kuwa jitihada hizo hufanywa kwa mujibu wa misingi imara Wataalamu wameweka masharti maalumu kwa anayehusika jambo hilo ili jitihada yake iambatane na vigezo maalunu vya kitaaluma, vigezo hivi ni kama vile kuwa na maarifa kwa Aya za Qur`ani na hasa Aya zikusanyazo hukumu na Hadithi zote za Mtume zilizo thabiti au zilizofutwa, kutambua elimu ya Fiqhi na vyanzo vyake, kujua elimu za Hadithi ikiwemo kuainisha wasimuliaji wa Hadithi ili awe na uwezo wa kuainisha Hadithi iliyo sahihi na ile isiyo sahihi na kutambua hukumu zilizokubalika na wataalamu wote  na zile zilizokubalika na baadhi na kukataliwa na wengine ambapo mwenye kutoa jitihada haruhusiwi kutofautiana na maoni ya wataalamu wote (Ijmaa), pia anayefanya jitihada anatakiwa kuwa na ujuzi wa lugha ya kiarabu na hasa maana za maneno pamoja na mitindo ya waarabu ili ahakikishe kuwa anatambua maana iliyo sahihi ya neno bila ya kuchanganya maana, ambapo asiye na maarifa ya kutosha kwa lugha ya kiarabu, basi elimu yake na jitihada zake haziwi imara, vile vile mwenye kutoa Fatwa kutegemea jitihada zake mwenyewe anatakiwa kuwa anatambua vyanzo vingine vya kutunga sharia kama vile; kawaida ya watu (Urf), Qiyas, na awe na uwezo wa kupatanisha dalili ambazo huonekana kuwa zinatofautiana kuhusu hukumu fualni, la msingi awe miongoni mwa wataalamu wabobezi anayeaminiwa na wataalamu na taasisi rasmi za kidini ambazo zinahusika kuwaandaa watoaji Fatwa na kufundisha sharia. 

Share this:

Related Fatwas