Masharti ya kusihi kwa sala ya jeneza
Question
Masharti ya kusihi kwa sala ya jeneza ni nini?
Answer
Kusali sala ya jeneza ni kati ya faradhi za kifaya ambazo zikitekelezwa na sehemu ya waislamu hutakiwi kutekelezwa na wengineo kwa mujibu wa wataalamu wa fiqhi, sheria ilipendekeza na kuwahimiza waislamu kusali sala hiyo na kufuata jeneza mpaka mazishi, imesimuliwa na Abu Hurairah (R.A.) alisema kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Yeyote anayehudhuria jeneza mpaka isaliwe basi atapata sehemu ya peponi iliyo saw ana qirati moja, na atakayefuata jeneza mpaka maiti izikwe hupata qirati mbili” akaulizwa: “ni kiasi gani qirati mbili hizo? Akajibu: ni sawa na milima miwili mikubwa” imekubaliwa na wote.
Sala ya jeneza ili iwe sahihi yapo masharti maalumu ambayo ni yale yale masharti ya usahihi wa sala iliyofaradhishwa ambayo ni pamoja na kuwa na twahara ya mwili, nguo na mahali kutoka katika najasa zote na kusitiri uchi, kuelekea Qibla na nia.