Namna ya kuswali Swala ya jeneza.
Question
Ni ipi namna ya Swala ya Jeneza.
Answer
Swala ya Jeneza ina Takbira / Rakaa nne, mwenye kuiswali baada ya takbira ya kwanza atasoma ufunguzi wa Kitabu kwa maana ya Suratul-Fatihah, baada ya takbira ya pili atasoma nusu ya Attahiyyatu ya mwisho ambayo anaisoma akiwa kwenye swala za kawaida, kwa maana mwanzo wa: mpaka mwisho wa attahiyyatu, baada ya takbira ya tatu atamuombea duwa maiti, na baada ya takbira ya nne mwenye kuiswali atajiombea yeye mwenyewe na kuwaombea Waislamu wote duniani, kisha atatoa salamu mbili.