Kuswali jamaa kwenye swala ya jeneza.
Question
Je kuswali jamaa katika Swala ya Jeneza ni sharti?
Answer
Swala ya Jeneza kuswaliwa na watu watatu au zaidi au wachache ni swala sahihi Kisharia, kwa sababu kuswali pamoja au kuswali jamaa si sharti la kufaa au kusihi Swala ya Jeneza, bali usahihi wake hufikiwa hata kwa kuswali mtu mmoja tu, na kuswali jamaa au kwa pamoja ni jambo la Sunna, hayo yameelezwa na Jamhuri ya Wanafiqhi viongozi wa madhehebu yanayofuatwa ya kifiqhi.