Kushirikiana kwenye mambo mema.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushirikiana kwenye mambo mema.

Question

Ni zipi thawabu za ushiriki wa kujitolea kukausha maji ya mvua barabarani.

Answer

Ushirikiano mzuri na watu wanaojihusisha na ushiriki wa kujitolea kukausha maji ya mvua kwa kuyaondoa kwenye maeneo maalumu ya wanadamu, katika hilo kuna malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kukausha barabara na mitaa kwa kuyaondoa maji ya mvua kwenye maeneo maalumu ni miongoni mwa kazi zinazohitajika, kama vile mwanadamu katika kazi hiyo ana malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani kuondoa kero kwenye barabara za watu ni sehemu ya Imani, Wanachuoni wamelezea kuwa kusudio la kuondoa kero barabarani: Ni kuondoa vinavyokera watu miongoni mwa mawe, au maji ya mvua, au tope, au miba, au vitu vingine vyenye kuleta kero, vile vile kukata miti kwenye maeneo magumu kupita, yote hayo ni Sunna kuondoa, miongoni mwake yapo yanayofikia kiwango cha wajibu kama vile kuwepo kisima katikati ya barabara na ikahofiwa kudondokea humo mlemavu wa macho, mtoto mdogo na mnyama, basi inakuwa ni lazima kukifukia au kukizungushia ikiwa hakutaleta madhara kwa wapita njia.

Share this:

Related Fatwas