Kumlipia deni marehemu.
Question
Je inapaswa kwa warithi kulipa deni la marehemu wao ikiwa hajalipa deni yake?
Answer
Sharia ya Kiislamu imehimiza kutekeleza mambo ya lazima na haki ikiwemo ulipaji madeni. Mwenyezi Mungu Amesema:
{Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} Al-Maidah: 1. Sharia imebainisha kuwa deni linapaswa kulipwa kwa warithi wa marehemu, nalo hutangulizwa kwenye wasia ulioachwa na kwenye ugawaji mirathi kwa warithi. Mola Mtukufu Anasema:
{Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni} An-Nisaai: 11. Ikiwa hakuacha mali ya kuweza kulipa deni basi inatakiwa warithi wa maiti kulipa deni la mrithiwa wao, na kuligawa deni kati yao kwa kukubaliana, kwa sababu hilo ni katika wema wa hali juu sana kwa maiti, kwa kauli ya Mtume S.A.W:
“Nafsi ya Muumini imetundikwa kutokana na deni lake mpaka lilipwe”.