Kufunga kwa ajili ya marehemu.
Question
Ipi hukumu ya kufunga kwa niaba ya aliyefariki akiwa na deni la funga
Answer
Katika yaliyokubaliwa na Wanachuoni ni kuwa funga ni nguzo muhimu katika nguzo za Uislamu, ambapo Mwenyezi Mungu amewahidi wenye kufunga malipo makubwa, isipokuwa kwa mwanadamu inaweza kutokea udhuru unaomzuia kufunga, kama vile kuumwa, safari, kutokwa na damu ya hedhi, nifasi na kupoteza fahamu, ikiwe mfungaji amefungua kwa sababu ya uwepo udhuru unaodhaniwa utaisha, udhuru huu ukaendelea mpaka akafariki, basi Wanachuoni wamekubaliana asimfungie mtu yeyote wala kumlipia fidia kwani hana dhambi kwa kukosekana mapungufu yake, ama udhuru ukiwa umemalizika na kuweza kulipa siku zilizompita lakini akazembea kwenye hilo wala hakufunga mpaka anafariki, basi warithi wake wanatakiwa kutumia theluthi moja ya mali iliyoachwa kulisha masikini kwa kila siku aliyoacha kufunga, ikiwa ameacha usia kwenye hilo, na kama hajaacha basi inakuwa ni kujitolea kwa kile kinachotolewa kwa ajili yake.