Kutumia manukato kwa ajili ya mgonjwa.
Question
Ipi hukumu ya kutumia mafuta mazuri kwa ajili ya mgonjwa na kumuombea duwa wakati wa kumtembelea?
Answer
Ni Sunna kwa Muislamu pindi anapoingia kwa mgonjwa ili kumtembelea kumuombea duwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kumpunguzia huzuni yake, na kumfariji na hali yake ya maradhi, kama vile kumuombea umri mrefu kuondokewa na maradhi pamoja na mfano wa hayo, kama kumwambia: “Hakuna ubaya utapona kwa utashi wa Mwenyezi Mungu” au “Mwenyezi Mungu atakuponya na kukupa afya njema” au “Mwenyezi Mungu akupe umri mrefu” na maneno yanayofanana na hayo, hakuna shaka kuwa kuchunga hisia za mgonjwa na kumpa matumaini ya kuishi umri mrefu pamoja na kumtakia kupona ni jambo lenye thamani kubwa ya kibinadamu na kiustarabu, na ndani yake kunaleta furaha kwa mgonjwa, na kuupa furaha moyo wake, pia kuipa nguvu azma yake na kuuchangamsha moyo yake jambo linalosaidia kupelekea kupona kwake.