Zaka kwa ajili ya Kuoa

Egypt's Dar Al-Ifta

Zaka kwa ajili ya Kuoa

Question

Kamati za Zaka hukusanya mali za Zaka na Sadaka, na kuwapa wanaostahiki, na baadhi ya vijana wasio na uwezo wa kuoa wanaziomba ili kuwasaidia kukamisha taratibu za ndoa, na kutoa matangazo ya kukusanya pesa ili kuwaozesha, je kunajuzu mali hizi kuwa ni mali zilizotengwa kwa ajili ya Zaka?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Kutoa Zaka ili kusaidia anayetaka kuoa asieweza kumudu ghara zake ni jambo linalojuzu kwa Madhehebu ya Malik, na kama wasemavyo baadhi wafuasi wa Madhehebu ya Hanbal, wanasema kwamba katika kutimiza kutoshelezana ni kumpa masikini katika mali ya Zaka ili kufikia kupata kitakachomwezesha kuoa akiwa hana mke na akawa anahitaji kuoa([1]). Imamu Al-Hattab Al-Maliki amesema: “kwamba yatima anapewa katika mali ya Zaka kiasi ambacho atakitumia katika mahitaji yake ya ndoa, na ni jambo ambalo amelipendekeza kadhi Hassan katika haki ya mtoto aliezuiwa kutumia mali zake, hivyo basi, yule ambaye hana vitu na mapambo ambavyo ni lazima kwa ajili ya ndoa atapewa katika mali ya zaka, hii ni bora lizangatieni([2]).

Imepokewa kutoka Umara bin Abdula Aziz kwamba yeye alimwamrisha mpiga mbiu kwa watu: “Wakowapi masikini? Wakowapi wenye madeni? Wako wapi wanaotaka kuoa?” kwa maana ambao wanataka kuoa na hawana uwezo, amewaita ili awape katika pesa za Waislamu zinazohifadhiwa.

Zaka ni wajibu kwa Waislamu tu; kwa sababu inachukuliwa kutoka kwa matajiri Waislamu na hupewa masikini wao. Na Zaka ya mali asili yake ni kutolewa mali, ikiwa anayestahiki anahitaji kitu kitakachomsaidia, basi hakuna ubaya kuitoa katika hali ya kitu; kwa sababu kinachotakiwa ni kufikia masilahi yake.

Hivyo katika uhalisia wa swali kunajuzu kwa kamati kutoa Zaka kwa lengo lililotajwa kwa Waislamu wanaohitaji katika njia ya msaada wa kifedha, ikiwa wanaofaidika na hilo wanahitaji kitu miongoni mwa mahitaji ya ndoa na kamati ikaweza kuwapa, basi kunajuzu hilo pia.Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

([1]) Hashiyat Al-Rawdha Al-Murabba, 1/400.

([2]) Mawahib Al-Jalil fi Sharh Mukhtasar Al-Khalil, 2/347.

Share this:

Related Fatwas