Zaka kwa ajili ya Kutatua Matatizo ya Vijana
Question
Katika juhudi za “Mfuko wa Ijumaa” wa taasisi ya “Al-Ahram” katika kusaidi kutatua matatizo ya vijana, kwa kuwapatia fursa za kazi na kuwasaidia katika kuoa kwa kununu vifaa na kuwalipia kodi, na baada ya wasomaji wetu wengi kutaka kusaidia kwa mali za Zaka na sadaka, tunajiandaa kufungua akaunti maalumu kwa lengo hili, na ili tunayoyafanya yaendane na yale yanayoamrishwa na Sharia Tukufu, tunataka kujua kutoka kwa Mashekhe zetu uhalali wa kutoa mali za Zaka kwa lengo hili. Pia je! Kunajuzu kuwakopesha hawa vijana, ili mkopaji awekeze pesa aliyokopa, na kulipa hata kama kwa awamu? Pia tunaomba mtuwekee wazi makundi mengine ya kupewa Zaka kama mlivyopenedekeza, kwa namna vijana wapambanaji watafaidika ambao wanapata tabu kutafuta chakula chao na cha familia zao.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Watu wanaopewa Zaka ni aina nane waliotajwa katika Qur`ani Tukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima} [Al-Tawba, 60], na hili linamaanisha kwamba Zaka imefaradhishwa kwa ajili ya kumjenga mwanadamu, kumtosheleza na haja zake, na yanayofunagamana maisha yake na uhai wake, kama ndoa na kusoma na mengineyo katika mambo muhimu ya maisha yake na mahitaji yake.
Wanazuoni wa hakiki wanaona kwamba lengo la kutoa Zaka ni kurekebisha; hivyo kunajuzu kumpa Zaka mwanadamu ili imtoe katika kuhitaji na kumpeleka kwenye kujitosheleza, na katika Madehehebu ya Shafi kwamba anapewa kitachomtosheleza maisha yake yote kwa kukadiria umri ambao watu wengi wa mfano wake huishi; akiwa fundi atapewa vifaa vya kazi yake vinavyomtosha kujikimu yeye na familia yake, akiwa msomi atapewa mali itakayomtosha yeye na familia yake na iatakayomfanya ajitenge kwa ajili ya elimu maisha yake yote, kwa kununua vitabu, ada ya masomo na kuwafundisha wengine, na katika hilo pia kushughulika na kitu kimoja ambako kuna mpa mwanafunzi wakati wa kupata ngazi maalumu ya masomo unaoendena na uwezo wake wa kielimu na kiakili, ili anaehitaji ngazi hii ya elimu kufanya vyema katika kazi yake na kupata pato la kutosha yeye na familia yake, kwani tabia ya zama za sasa kupata kazi uutokana na ngazi ya elimu, ngazi ya elimu imekuwa kama kitendea kazi kwa fundi, Pamoja na kuwa anachokichuma katika hilo kinatokana na elimu inayomsaidia na kusaidia Umma wake … na kama hivyo.
Imepokewa kutoka Umara bin Abdula Aziz kwamba yeye alimwamrisha mpiga mbiu kwa watu: “Wakowapi masikini? Wakowapi wenye madeni? Wako wapi wanaotaka kuoa?” kwa maana ambao wanataka kuoa na hawana uwezo, amewaita ili awape katika pesa za Hazina ya Waislamu.
Ama kuwakopesha vijana kwa namna mkopaji atawekeza kiasi cha pesa anachokopa na kukirudisha, hata kama kwa awamu, huko hakuwi katika kutoa Zaka; kwa sababu zaka sharti yake ni kumiliki, lakini inawezekana kutengeneza mfuko maalumu kwa jambo hilo, ambao utakusanya sadaka, lakini si Zaka.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
