Zaka kwa ajili ya Kozi za Mafunzo kwa Wanazunzi
Question
Je! Inajuzu kutoa mali ya Zaka baadhi yake au yote, katika matumizi ya kozi za kimafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Dini ili kuboresha utendaji wao wa kidaawa na kupata mbinu muhimu za kutekeleza wajibu wao? Pamoja na kujua kuwa hawa wanafunzi pato lao halikidhi matumizi yao?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Zaka ni faradhi na nguzo katika nguzo za Uislamu, Sharia tukufu imeweka mfumo wa kuitekeleza kwa kupanga wanaopewa, Mwenyezi Mungu Anasema: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.} [Al Tawba:60].
Na Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana kujuzu kuwapa Zaka wanafunzi, haya yamesemwa na Madhehebu ya Hanafi na Shafi na Hanbal, na huo pia ni muktadha wa Madhehebu ya Malik.
Na Ibn Abidin amenukuu kutoka katika Jaamii Al-Fatawa maneno haya: “Hakujuzu kutoa Zaka kumpa anayemiliki kiwango cha Zaka isipokuwa mwanafunzi, na mpiganaji jihadi, na Hujaji alieishiwa” ([1]).
Na An-Nawawy amenukuu kutoka kwa Asahab kwamba wao wamesema: “Iwapo mtu anaweza kupata riziki inayofaa hali yake, lakini anashughulika na kujipatia baadhi ya elimu ya kidini kiasi kwamba akijishughulisha na kazi ataacha kujipatia elimu, basi inafaa kwake kuchukua Zaka, kwa sababu kujipatia elimu ya dini ni faradhi ya kutosheleza.” ([2]).
Al-Khatib Al-Sharbini amesema: “Na mtu mwenye uwezo wa kujitafutia akijitoa kwa ajili ya kutafuta elimu ya Dini, na ijapokuwa si lazima kwake, na kukawa na uzito kukusanya kati ya mambo mawili, atapewa Zaka, lakini si akijitoa kwa ajili ya ibada na kumlisha mwenye njaa na mfano wake” ([3]).
Na Al-Bahouty anasema: “Na mtu mwenye uwezo wa kujitafutia akijitoa kwa ajili ya kutafuta elimu ya Dini, na ijapokuwa si lazima kwake, na kukawa na uzito kukusanya kati ya mambo mawili, atapewa Zaka, kutokana na haja yake” ([4]).
Na Al-Bahouty amenukuu hivi karibuni katika sehemu iliyotangulia “kwamba Ibn Taiymiya aliulizwa kuhusu mtu ambaye hakuwa na thamani ya kununulia kitabu cha elimu atakachotumia? Akasema kunajuzu kwake kuchukua anachokihitaji katika vitabu vya elimu ambayo ni lazima kwa ajili ya masilahi ya Dini yake na dunia yake, kisha akasema Al-Bahouty: Huenda hilo halitoki nje ya aina ya watu wa kupewa Zaka; kwa sababu hilo ni katika sehemu ya mahitaji ya mwanafunzi, hiyo ni kama matumizi yake” ([5]).
Ama wafuasi wa Madhehbu ya Malik wamesema: “Na kunajuzu kuitoa Zaka kwa mtu mzima mwenye uwezo wa pato, na lau kama ataacha hiyo ni kwa khiari” ([6]).
Na miongoni mwa waliyotolea dalili Maimamu Wakuu kujuzu kumpa Zaka mwanafunzi kuingia matumizi ya anayetafuta elimu katika wanaopewa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hii kwa Hadithi iliyotolewa na At-Tirmidy na akaisahihisha katika kauli ya Mtume S.A.W.: “Mwenye kutoka katika kutafuta elimu, basi anakuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka arejee”.
Pia Imamu Abu Hanifa ameelezea kujuzu Zaka kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa watafutaji elimu ([7]).
Na hapana shaka kwamba kutoa Zaka kwa mafunzo ya kisharia kwa wanafunzi wanaojifunza mambo ya lazima, ni katika hukumu ya kutoa ili kuwanunulia vitabu, ikiwa sio mahitaji yao ya mafunzo ya ujuzi huu kunasisitizwa zaidi kwa kuenea manufaa ya ujuzi wao kwa wote.
Hivyo basi, ikiwa hali kama ilivyokuja katika swali, basi kunajuzu kutoa Zaka kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Dini, hasa ikiwa pato lao halikidhi matumizi yao.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
([1]) Hashuya Ibn Abidin: Mlango wa zaka, sehemu ya wanapewa Zaka.
([2]) Majmou: Mlango wa Zaka, sehemu ya kutaja watu wa Zaka na yanayofungamana na hayo.
([3]) Al-Iqnaa: Mlango wa zaka sehemu ya kuwataja watu wa zaka na yanayofungamana nayo.
([4]) Kashaf Al-Qanaa Mlango wa zaka sehemu ya kuwataja watu wa zaka na yanayofungamana nayo
([5]) Kashaf Al-Qanaa Mlango wa zaka sehemu ya kuwataja watu wa zaka na yanayofungamana nayo
([6]) Hashiya Ad-Dousouqy: Mlango wa zaka, kifungu cha watu wanaopewa zaka na yanayofungamana na hayo.
([7]) Hashiyat Ibn Abdini: Mlango wa Zaka, sehemu ya wanaopewa Zaka na fungu la kumi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
