Mipaka ya Miamala kati ya Wanadoa kabla ya Harusi
Question
Naomba kufahamu kwa ujuzi na maarifa yenu ambayo tunayafuata kwa kuwa sisi si wajuzi wa baadhi ya mambo, hivyo tunaomba ushauri kwa wenye elimu na maarifa, ili tufanye mambo kwa mujibu wa Fatwa zenu katika mambo hayo:
Mimi ni kijana mwenye umri wa kiaka ishirini nane, nimeoa miezi mitano iliyopita lakini sijamuingilia mke wangu, kutokana na hali anayopitia kijana kwa zama zetu, baadhi ya rafiki zangu wameniambia kwamba huyo anazingatiwa kuwa ni mke wangu, na ninaweza fanya nae tendo la ndoa muda wa kuwa tumeshafunga ndoa mbele ya ndugu na jamaa, japo sina haki ya hilo. Nataka kujua ni upi ukomo wa mahusiano yetu ya mke na mume?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ndoa ni Sunna katika Suuna za Uislamu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri}[Ar-Roum, 21].
Na imepokewa kutoka kwa Ibn Masoud R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: “Enyi vijana mwenye kuwa na uwezo miongoni mwenu, basi aoe, na asieweza basi afunge, kwani hilo kwake ni kinga” imepokelewa na Bukhari.
Na muda wa kuwa ndoa imefungwa kiusahihi kwa nguzo na sharti zake, basi athari zake zinafuata katika kuhalalisha tendo la ndoa, na kupatikana watoto na haki ya mke ya matumizi na mengineyo.
Swali linaonesha kuwa: Muda wa kuwa muulizaji anathibitisha kwamba ndoa ni sahihi kwa nguzo zake na sharti zake za kisharia, basi ana haki kwa mke yote yanayoruhusiwa kwa mke na mume kwa vidhibiti vya kisharia vinavyojulikana, na kukutana nae kimwili kunakuwa ni sahihi kisharia, kwani ndoa imefungwa kiusahihi kisharia, lakini kunapasa kwa mume kuheshimu mila na desturi, na asikae faragha na mke wake katika nyumba ya wazazi wa mke; na hii ili kuepuka mambo ambayo yanaweza kuharibu sifa ya mke na familia yake, na tahadhari hii ipo, na kuingia kwenye hatari hii huwenda kukaingia katika njia ya haramu kwa kulinda sifa na heshima ya familia ya mke, na huenda kitendo hiki kukasukuma kutoa talaka, na hii ni dhambi kubwa, hivyo ni wajibu tendo la ndoa lianze kabla ya kuhamia katika nyumba ya wanandoa katika wigo wa kuheshimu mila na desturi ambazo zimezoeleka kwa watu.
Na katika yaliyosemwa linapatikana jibu la aliyeuliza.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
