Hukumu ya biashara ya dawa za bima ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya biashara ya dawa za bima ya afya

Question

Baadhi ya wauzaji madawa wananunua dawa zinazohusishwa kwa bima ya afya na kuziuza ndani ya maduka yao ya dawa kwa wasio na haki ya kupewa dawa hizo na nchi, ni nini hukumu ya hayo? 

Answer

Madawa za bima ya afya si haki ya mtu yeyote, lakini hutolewa kwa wagonjwa wanao haki ya kunufaika kwa mfumo huu kupitia kuwapa dozi za kutosha kulingana na muda wa matibabu yao ili wazitumie dawa hizo katika wakati mwafaka, nchi ndiyo inayogharamia kufadhili mfumo huu kwa sharti kwamba wagonjwa hawa hawana ruhusa ya kuziuza dawa hzio, ambapo ni mali ya umma ambayo haikubaliki kutumiwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu husika, kwa hiyo ni haramu kuuza au kununua dawa hizo, pamoja na kwamba kufanya hayo ni ukiukaji unaosababisha madhara makubwa kwa mfumo wa afya na uharibifu wa jamii kwa ufisadi na uadui wa kukiuka haki za wagonjwa.

Kufanya hivyo au kusaidia kuchangia ifanywe na baadhi ya wauzaji dawa au wengineo ambao wana mamlaka ya kuuza au kuhifadhi dawa hizo na kuzifikisha kwa wanaozistahiki ni udanganyifu na uharibifu wa amana, kwa hiyo anayethibitika kufanya hivyo hustahili kuadhibiwa na kuwa miongoni mwa wale amabo Mwenyezi Mungu Atakasirika nao siku ya Mwisho, mbali na kustahiki kushtakiwa mbele ya nchi na jamii.

Share this:

Related Fatwas