Hukumu ya Kukana Katika Masuala ya ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kukana Katika Masuala ya Utata

Question

Hukumu ya Kukana Katika Masuala ya Utata

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa rehema

Sifa njema zote Anastahiki Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu, Mkarimu, Mwingi wa rehema, Mwenye heri nyingi, ukarimu, na ihsani, Ninamhimidi kwa sifa njema, na rehema na amani zimshukie mtukufu wa Daraja Mtume Adnan bwana wetu Muhammad, mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa jamii mbili, wanadamu na majini, na rehma na amani ziwafikie watu wa nyumbani mwake walio safi na maswahaba zake wema muda wote wa usiku na mchana. Na baada ya hayo…

Tunadai usahihi wa msingi usemao: “Hakuna kukana katika masuala yenye utata” na sehemu hii inathibitisha uadilifu wake, pamoja na masuala yaliyooegemezwa kwake ili kuyafikia kwayo manufaa.

Na nimeipanga katika sehemu mbili pamoja na utangulizi:

Utangulizi ni pamoja na yafuatayo:

Kwanza: sababu za utata, sifa zake, na adabu zake.

Pili: Kutoka mbali na utata ni jambo la kuhitajika.

Ama sehemu ya kwanza, inaeleza ukweli wa kukana na masuala yenye utata.

Sehemu ya pili katika hukumu ya kukana katika masuala yenye utata.

Na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aniongoze kwenye njia iliyonyooka, kwani njia hii ni nzuri kuombwa na kutarajiwa, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Dibaji

Kwanza: Sababu za Utata na Adabu zake

Hakika utata katika masuala ya kiakili kwa ujumla na hasa masuala ya kifiqhi ni jambo linalofaa, utata unaendelea kuwepo baina ya watu tokea zama za Nuhu (A.S) na hakuna hata taifa moja lililoepushwa nao, Mwenyezi Mungu aliujaalia umma wa Kiislamu utofautiane kama yalivyotofautiana mataifa yaliyo kuwepo kabla yake, na utata huu ndio hukmu ya Mwenyezi Mungu juu yao. Kuhusu jambo hilo Mwenyezi Mungu anasema: {Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana (118) Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba...}[Hud: 118-119]

Asili ya utata katika masuala ya kifiqhi ni hamu ya kufikia haki na wajibu, basi haki ni lengo la muumini analolitaka, Mwenyezi Mungu anasema: {Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?} [YUNUS: 32].

Al-Hajwi anasema katika [Al-Fikr As-sami] akieleza hali ya Fiqhi ya Kiislamu katika karne ya pili: “Yanayotokana na kutofautiana na kuamini kuwa mpinzani wake ni mkosaji katika suala fulani kwa mujibu wa dalili inayosisitiza  makosa yake kufuatana na dhana yake, si katika masuala yote, na inaaminika kuwa na udhuru kwa mujibu wa dalili yake, na wanafahamu  kuwa kila mwanachuoni ana haki ya, kuheshimiwa mawazo yake, hivyo, tofauti haina madhara kwao, lakini tofauti ilikuwa kwa ajili ya kufikia haki, kwa hivyo, Fiqhi ilikuwa na nguvu mno” [Al-Fikr As-samifi Tariikh Al-Fiqhi Al-Islami 1/525, Darul Kutub Al-Ilmiyyah].

Haki ilitambuliwa kutokana na ujumla wa dalili, na kutokana na hivyo utata wenyewe haukuwa lengo pekee yake, lakini kila mmoja anatafuta haki kwa njia zake. Tofauti inatokea kwa sababu yoyote, kwa kuyatumia haya katika hukumu za kivitendo za kisharia zilizoelezwa katika fiqhi, zinazonufaika tu na dalili za kisharia, nazo ni - yaani: dalili za kisharia- hazinufaiki ila kwa dhana tu; kwa sababu dalili zimegawanyika katika sehemu mbili: dalili zilizoafikiana nazo, na dalili zinazohitalifiana, basi kinachokubaliwa ni Qura’ni, Sunna, makubaliano na upimaji.  Ama upimaji unanufaisha dhana tu, na hali hii iko wazi. Ama makubaliano yanatofautiana katika aina mbili: makubaliano ya kimya, ambayo yananufaisha dhana tu, ikiwa yalipitishwa kwetu kupitia watu wengi au kupitia wachache tu, na makubaliano ya wazi. yenye manufaa, lakini ni machache sana. Ikiwa makubaliano yalipitishwa kwetu kupitia watu wachache, basi yananufaisha dhana tu, na ikiwa yalipitishwa kwetu kupitia watu wengi nayo yananufaisha uhakika. Lakini katika hali chache sana. Kuhusu Sunnah, ikiwa imepitishwa kupitia watu wachache, basi hunufaisha dhana tu, ikiwa dalili zake ni ya uhakika au ya kidhani, na ikiwa imepitishwa kupitia watu wengi – na hali hii chache sana. basi ni sawa na kitabu ambacho matini yake ni ya uhakika na maana yake ni wa kidhani kwa sababu inategemea kukataa kwa uwezekano kumi ambao asili katika maneno ni kuukanusha kwake. Ama dalili ambazo ndani yake kuna ikhtilafu hazinufaisha isipokuwa dhana tu kwa wale wanaosema hivyo.

Basi hukumu za kifiqhi zinathibitishwa kupitia dalili za kidhana, na dhana zote zinakubali upinzani, na wakati mwanazuoni wa fiqhi alipolazimika kufuata aliyoyadhani ni lazima kuwepo kutokukubaliana kwa mujibu wa dalili ya dhana hiyo.

Mtazamo kwa ujumla hutofautiana baina ya mtu mmoja na mwengine na kundi hadi lengine, na kila mtu au kikundi hutazama suala lenye utata kwa mtazamo wake kulingana na maoni aliyo nayo, na dalili ya ikhlasi katika kutafuta ukweli ni kurejea kutokana na yale yaliyomdhihirikia kutoka makosa yake, na wanachuoni wangapi wamechukua rai ambayo ndiyo lengo la dhana yake, na ilipombainikia kuwa amekosea, akayaepusha makosa hayo. Imepokelewa kutoka kwa Abd il-Malik Ibn Abi Bakr ibn Abd ir-Rahman ibn Al-Harith ibn Hisham kutoka kwa baba yake kwamba alimsikia Abu Huraira akisema: Yeyote ambaye ameamka akiwa na janaba pasipo kuona manii hapaswi kufunga. Basi Abu Bakr na baba yake Abd Ur-Rahman wakaondoka mpaka wakafika kwa Ummu Salama na Aisha, na wote wawili wakasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiamka asubuhi, akiwa na janaba pasipo kuona manii kisha alikuwa akifunga. Basi Abu Bakr na baba yake, Abd Ur-Rahman, wakatoka na kwenda kwa Marwan na kumwambia kuhusu hilo, kisha akasema: “Niliwaamulia nyinyi wawili mlipotoka kwenda kwa Abu Huraira wakazungumziana naye. Wakaondoka mpaka kufikia Abu Huraira wakamwambia akasema: Walikuambia? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Wote hawa wawili wanajua zaidi, lakini Al-Fadl Ibn Abbas aliniambia hivyo.

Na pale Amirul-Muuminina (kiongozi wa waumini), Omar Ibn Al-Khattab, (R.A), alipotoa rai yake juu ya suala maarufu la mirathi, ambalo linajulikana kuwa ni suala la pamoja, kwamba ndugu wa mama wachukue thuluthi ya urithi wa mama yao, wakati ndugu wa baba na mama wamenyimwa. Wakati ndugu wa baba na mama walipopinga mgawanyo huu wa urithi, Omar alitafakari upya hukumu yake ya kwanza, na akaona kwamba ilikuwa ni haki na usawa kugawana ndugu wa baba na mama na ndugu wa mama katika sehemu ya thuluthi, hivyo akatoa hukumu yake ya pili kwa msingi huu, na akatengua hukumu yake ya kwanza.

Katika suala hilo, anazingatia sana kauli ya Imamu wetu Al-Shafii, (R.A): “Iwapo Hadithi ni sahihi, basi Hadithi hiyo ni madhehebu yangu.” Ni sahihi kuifanya tafsiri ya kivitendo kwa kipengele hiki, kwa sababu kughairi kutoka katika kusema rai iliyopingwa na Hadith ni dalili ya kufuata ukweli na kuwa na nia ya kuufuata.

Imepokelewa kutoka kwa Wanavyuoni waliotangulia na wa hivi sasa kuwa mwenye kumhimiza Mwislamu kuacha madhehebu yake au maoni yake juu ya suala fulani, kama kuna maslahi, basi jambo hili lina faida kubwa kwake na kwa Waislamu wengine. Miongoni mwa hayo ni yale yaliyokuja katika Majmuu Al-Fatawa kwa Ibn Taymiyah katika maneno yake kuhusu Bismillah, je, Bismillah ni aya mwanzoni mwa kila sura au sio? Je, Imamu anaruhusiwa kupaza sauti kwake au la? Baada ya kutaja maoni yote katika suala hilo, alisema: “Inapendekezwa (Mustahabu) kwa mtu kuwa na nia ya kuiunganisha mioyo kwa kuacha mambo yaliyopendekezwa, kwa sababu maslahi ya kuunganisha mioyo katika dini ni bora zaidi ya maslahi ya kufanya vile”. Na habari za mahali hapo ni nyingi.

Mfuasi wa Sira ya hukumu za kifiqhi tokea zama za Mtume (S.A.W) hadi zama za maimamu na baada yao anagusa baadhi ya mitikisiko mikali iliyosababisha baadhi ya matukio ambayo yalianzisha mambo ambayo yalikuwa nje yake ndani ya mzunguko wa kukhitalifiana, ikiwa ni pamoja na kuibuka kwa madhehebu na fikra mbalimbali za kisiasa, huku mbinu za kiakili na kifikra zikiongezeka kwa wingi wa madhehebu hizo. Na kila dhehebu lilikuwa na nukta na kanuni ambazo lilianzia katika shughuli zake na matini za mtungaji wa Sharia, katika tafsiri yake ya vyanzo vya kisheria, na katika misimamo yake juu ya masuala mbalimbali yaliyojitokeza, na haja ikaanza kuonekana ya kuweka udhibiti na vikwazo, na kuainisha mbinu na njia za makisio, na kuainisha nini inayoruhusiwa kutofautiana na nini ambayo hairuhusiwi.

Katika suala hili, nasema yafuatayo:

Tunapaswa kuamua kuwa tofauti inafungika katika matawi ya kifiqhi na baadhi ya masuala yanayohusiana na vyanzo vya dini, pamoja na makubaliano kamili juu ya vyanzo vya dini ambavyo vinawakilisha utambulisho wa Uislamu, ambayo ni miongoni mwa utunzaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na udhamini wake kwa dini hii mpaka Mwenyezi Mungu atakapo irithi dunia na wote waliopo ndani yake. Kwa hiyo haikutokea kutokukubaliana katika mambo ya yakini, ambapo kukubaliana katika mambo ya yakini ni muhimu.

na kwamba tofauti katika matawi ni nafasi pana, hakuna umma uliobanwa na madhehebu fulani, kama ni madhehebu moja ni ngumu kwa umma unaelekea madhehebu nyingine. Imepokewa kutoka kwa Hamid At-Tawiil alimwambia Omar Ibn Abdul Aziz kuwa: Lau ungewaunganisha watu pamoja kwenye kitu Fulani. Akasema: Kinacho nifurahisha ni kwamba hawakuwa na tofauti. Kisha akawaandikia Maimamu katika nchi zote:“Mhukumu kwa watu wote kwa mujibu wa yale yaliyokubaliwa na wanavyuoni wao wa Fiqhi.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alikuwa ndiye chimbuko la kueleza hukumu, na pamoja na hayo, uwepo wake, (S.A.W), haukumzuilia maswahaba kuwa na jitihada, na hili linathibitishwa na kisa cha kutumwa Muadh Yemen, na Hadithi ya swala kwenye Banu Quraydhah. Imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Masoud, (R.A) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), alituita siku alipotoka kwenye Al-Ahzab (Makundi): kwamba asiswali yeyote Swala ya Adhuhuri isipokuwa katika Bani Quraydhah. Basi watu wakaogopa kuwa muda unapita, wakaswali kabla ya kufikia Banu Quraydhah, wengine wakasema: “Sisi tunaswali pale anapotuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata kama muda umepita.” Akasema: Mtume (S.A.W) hakukemea mojawapo ya makundi mawili.

Imepokelewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudari, (R.A), amesema: Watu wawili walitoka safarini, wakati wa Swala ukaja  na hawakuwa na maji, wakatayammamu udongo safi na wakaswali. Kisha wakakuta maji katika wakati wa Swala. Basi mmoja wao akarudia kuswali na kutawadha, na mwingine hakufanya hivyo, kisha wakaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), wakamtajia hilo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akamwambia yule ambaye hakurudia: “Umefuata Sunnah, na Swalah yako inatosha kwako.” Na akamwambia yule aliyetawadha na akarudia Swala: “Utalipwa mara mbili”.

Wanavyuoni waliweka udhibiti kwa ajili ya tofauti iliyozingatiwa, na wanavyuoni wengi walitilia maanani kutaja dhibiti hizi, na wengine walitilia maanani kusimamia sababu za tofauti zao, baadhi yao wamezifanya kuwa sababu sita kama vile Ibn Rushd Al-Maliki katika utangulizi wa kitabu chake: [Bidayatul Mujtahid], na baadhi yao wamezifanya kuwa sababu nane kama vile Abu Mohammed Al-Batliossi Al-Andalusi Al-Maliki katika kitabu chake: [Al-Tanbiih ala Al-Asbab allati Awjabt Al-Ikhtilaf baina Al-Muslimin], na miongoni mwao wamefikia sababu kumi na sita kama vile Ibn Juziy  katika kitabu chake: [Taqriib Al-Wusuul Ila Ilm Al-Ussul].

Zikiwemo sababu hizo ni zifuatazo:

Kukhitalifiana kuhusu kuthibitishwa kwa matini ya kisheria au kutothibitishwa kwake, na yanayoambatanishwa na hayo ni ukweli kwamba mwanachuoni wa faqihi hakuifikia matini hizi hapo awali, bali hiyo ilikuwa ni sababu ya kutokubaliana kwa sababu matini ya kisheria ndiyo tegemeo la kwanza kwa makisio.

Kukhitalifiana kuhusu lugha, kwani lugha inajumuisha vitawe na visawe, ukweli na sitiari, na maana ya jumla na maalum, hivyo tofauti kuhusu kuelewa maana ya istilahi hizi ilisababisha tofauti katika kuelewa matini na hukumu zinazohusika, kwa mfano Ain (jicho) linatumika bila kudhaniwa kwa chemchemi ya maji, au jicho la mtu, au jasusi, pamoja na wakati wa hedhi, na usafi kutoka kwake ... na kadhalika.

Kukhitalifiana kuhusu hoja ya baadhi ya dalili, ikiwa Qur’ani, Sunnah, Ijmah na upimaji vinaafikiana juu ya uhalali wake, lakini vyanzo vingine, kama Istihsan, Maslahi ya watu na vingine vinatofautiana katika uhalali wake. Baadhi yao wanaona kuwa kitendo cha Swahaba au fatwa yake ni hoja, huku mwengine anaona kinyume na hivyo... na kadhalika.

Kutokubali kwa dalili yenyewe kwa sababu ya udhaifu wake, au kwa maana ya umuhimu wake kutokana na tofauti ya ufahamu na tafsiri yake. Miongoni mwa mambo aliyowaandikia Mtume (S.A.W) kwa watu wa Yemen kwamba hakuna mtu anayeigusa Qur’ani ila aliye na usafi, na wanavyuoni wameifasiri kwa maana kadhaa, kwa sababu neno la safi linaweza kuashiria usafi kutokana na uchafu mkubwa au mdogo kabisa, na huenda likakusudiwa yule ambaye hana uchafu juu ya mwili wake. Kwa hiyo, palikuwa na khitilafu kuhusu kuigusa Qur’an bila ya kutawadha, baadhi yao wakaruhusu, na baadhi yao wakachukia. Mfano wa hili pia ni Hadithi iliyopita hapo juu isemayo: “Asiswali yeyote Swala ya Adhuhuri isipokuwa katika Bani Quraydhah”, ambapo baadhi yao waliichelewesha kwa makusudi swala kutoka wakati wake, wakichukua maana ya dhahiri ya Hadithi hiyo, na jitihada ya wengine ilisababisha kukiuka maana dhahiri ya Hadithi na kutenda kulingana na maana yake yaliyomo.

Kukhitalifiana kuhusu mbinu za kuchanganya na kuweka uzito baina ya matini zinazokinzana, hivyo kuchukulia makubaliano juu ya uthibitisho wa matini na kuafikiana kwao juu ya tafsiri yake, kunaweza kuwa na upinzani mzito ambao unatofautiana katika njia za kuichanganya na matini nyengine au kuipendelea, na miongoni mwa hilo ni Hadithi ya Abu Ayyub, (R.A), kwamba Mtume (S.A.W) alisema: “Mnapofanya haja zenu, msielekee Kibla wala usigeuke nayo, bali elekea mashariki au magharibi.”

Abu Ayyub akasema: Tulikwenda kwa Sham tukakuta vyoo vimejengwa mbele ya Kibla, kwa hivyo tukakengeuka na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Vile vile kuna Hadithi ya Abdullah Ibn Umar isemayo: “Nilipanda paa ya nyumba ya Bi. Hafsa kwa ajili ya baadhi ya mahitaji yangu, nikamuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akijisaidia na nyuma yake ni Kibla akielekea Sham. Mafakihi walikhitalifiana juu ya suala hilo, mitazamo yako ni pamoja na: Kuchanganya Hadithi hizi mbili: Hadithi ya Abu Ayyub ina maana kwamba kukataza ikiwa ni majangwani na hakuna majengo baina yake na kibla, ama Hadithi ya Abdullah Ibn Umar, ina maana ya kwamba inajuzu kukielekea kibla au kujiepusha nacho ikiwa kiko kwenye majengo. Miongoni mwao: kupendelea kufuata Hadithi ya Abu Ayyub kwa kuzingatia ukweli kwamba kukataza kunatanguliza juu ya kuruhusiwa wakati kunapotokea upinzani, na miongoni mwao: kufuata Hadithi ya Abdullah Ibn Umar kwa kuzingatia kanuni kwamba hakuna katazo.

Hii ni baadhi ya sababu za kukhitalifiana baina ya mafaqihi, ambapo huongezewa tofauti ya mazingira, fikra na uwezo, na hitilafu ya maelewano, na hili na lile haingeleta mzozo baina ya pande zake, au kurithisha ushabiki wa kimadhehebu. Kwani hili ni dhihirisho la kutoijua Sharia na kanuni zake, na maisha ya maimamu na kauli zao, na hitilafu yao pia isingewaondoa katika kuzingatia adabu katika kushughulikia masuala haya yenye ugomvi. Kwa upande wa kiutendaji, nilikuta mijadala mingi iliyojaa adabu za kukhitalifiana zilizosimuliwa kwetu na vitabu vya historia na wasifu. Haya ni pamoja na maneno ya maimamu - ambayo ni mengi na hayawezi kuhesabika - katika kipengele cha uungwana na mwenye kukiuka, kwa kuzingatia hitilafu na kuruhusiwa kuiga madhehebu nyingine, na kuhama kutoka madhehebu moja hadi nyingine.

Kabla sijaweka mikononi mwako hukumu za adabu za kukhitalifiana, nitakutajieni baadhi ya hali za Maswahaba na kauli za maimamu na hali zao katika suala hili:

Imepokelewa kutoka kwa Abu Habiba (R.A) amesema: “Niliingia kwa Ali (R.A), pamoja na Imran Ibn Talha baada ya kumalizana na wamiliki wa ngamia. Akasema: Basi akamkaribisha na akamwendea, na akasema: Natumai Mwenyezi Mungu atanijaalia mimi na baba yako miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kuhusu wao: {Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana.}.

Imepokelewa kutoka kwa Abi Al-Buhturi, amesema: Aliulizwa Ali, (R.A) kuhusu watu wa ngamia, je ni washirikina? Akasema: Wamekimbia ushirikina, ikasemwa: Je, ni wanafiki? Akasema: Wanaafiki wanamkumbuka Mwenyezi Mungu kidogo tu, ikasemwa: Ni nani hao? Akasema: Ndugu zetu wametudhulumu.

Ndugu zao wa Kiislamu hakuwakana, na wala hakuwatangaza kuwa ni makafiri ingawa kuwapigana naye na kumpiga silaha.

Imepokewa kutoka kwa Al-Khatib kutoka kwa Imam Sufyan Al-Thawri, (R.A), kwamba amesema: “Ukimuona mtu anafanya kazi ambayo amehitilafiana nayo na ukamwona mwengine, basi usimkataze”.

Na katika historia ya Ibn Maiyn: (Yahya Ibn Said Al-Qattan – ambaye ni miongoni mwa maimamu wa Hadithi – alisema: “Hatumkanushi Mwenyezi Mungu, labda tuliona rai miongoni mwa rai za Abu Hanifa, basi tukaridhia hivyo, kwa hivyo tulisema rai hiyo”.

Shuba Ibn Al-Hajjaj amesema alipopewa taarifa ya kifo cha Imam Abu Hanifa: “Alikwenda pamoja naye faqihi ya Kufa, Mwenyezi Mungu ambariki yeye na sisi kwa rehema yake”.

Imepokelewa kutoka kwa Al-Khatib Abu Hanifa akisema: “Hii ni rai yetu, nayo ndiyo ni bora ya yale tunayoweza kufanya, basi anayetujia kwa yaliyo ni bora kuliko rai yetu basi rai yake ni bora zaidi kuliko rai yetu”.

Imepokelewa kutoka kwa Al-Darwardi akisema: “Nilimuona Abu Hanifa na Malik Ibn Anas katika msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) baada ya Swala ya Isha, na walikuwa wakijadiliana na kusoma mpaka mmoja wao akasimama katika kauli aliyosema mwenzie, akamshika mwenzie bila jeuri, hakukemea, wala hakufanya makosa mpaka wakaswali asubuhi katika baraza lao”.

Imepokelewa kutoka kwa Salih Ibn Al-Imamu Ahmad, amesema: Yahya ibn Ma’in alinikutanisha na akasema: Je, baba yako haoni haya kwa anayoyafanya? Nikasema: Anafanya nini? Akasema: Nilimuona akiwa na Shafii na Shafii akipanda, naye alikuwa akitembelea kushika hatamu za ngamia wake. Basi nikasema: Ukimkutana naye, mwambie: Baba yangu anakwambia: Kama ukitaka kujifunza fiqhi, basi njoo na ushike naye kutoka upande mwingine.

Kwa hivyo, kauli za Maimamu zilikuwa moja baada ya nyingine, na kukhitilifiana kwao kulikuwa kukiendelea kwa mujibu wa kanuni zinazozingatiwa zilizojaa maadili mema ambayo yalikuwa mbali na kupingana na kanuni za Kiislamu katika maudhui yake, na miongoni mwa adabu hizi ni zile zifuatazo:

Hali ya kukhitilafiana isiwe inakusudiwa yenyewe, kwa kumfanya kila mmoja wa wapingaji awe na lengo la kufikia ukweli mbali na hoja na mabishano.

Kuondoa kwa hali ya kukhitilifiana na kuizingatia, na maelezo mengi yatakuja baadaye.

Kulifikiria vyema kundi lingine, na kuamini kuwa lengo lake lilikuwa kufikia ukweli, na maneno ya Imam Ali (R.A), yamepita na yanaidhihirisha maana hii.

Kukiri kosa na kuliepusha, pia kumekuwa na ushahidi unaounga mkono maana hii.

Upole katika kukhitilifiana ili kuepusha uzembe unaoleta ugomvi baina ya wanaohitilafiana, na katika hilo Ibn Taymiyyah anasema: “Walikuwa wakijadiliana kuhusu masuala ya kielimu na kivitendo kwa kuhifadhi kuziunga nyoyo, umaasumu na udugu wa dini, hata. lau kila Waislamu wawili wanapohitilafiana juu ya jambo fulani, wakagombana, kusingekuwa na umaasumu au udugu baina ya Waislamu.”.

Kwamba kila mmoja kati ya pande hizo mbili ampe udhuru mwenzake, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni “kutokana”; Masuala yenye utata yanazunguka na dhana, na dhana zinaweza kuhitilafiana, kama tulivyowasilisha hapo juu.

Kutozungumza bila ujuzi, na kwa hivyo kila kitu kinachohusiana na suala hilo kieleweke kabla ya kuhitilafiana juu yake, na pia ihakikishwe kutoka kwa kauli ya mwenye kuhitilifiana kabla ya kumnasibisha kauli bila ya kujali kuhitilafiana kwake.

Pili: Kuepukana na kuhitilafiana kunapendekezwa:

Wanachuoni wameweka msingi ambao unachukuliwa kuwa ni dhihirisho la maadili ya hali ya juu na nia ya dhati ya kutaka kuungana tena, msingi ambao ni: “Kuepukana na kuhitilafiana kunapendekezwa.” Na Wanachuoni wa umma wanasawazisha kati ya msingi usemao: “Kuepukana na kuhitilafiana” na msingi usemao “Kuzingatia kwa kuhitilafiana.” Ama kwa Imamu Maliki, wanatofautisha baina yao. “Kuepukana na kuhitilafiana”, kwao ni msingi unaojitegemea, na  “Kuzingatia kwa kuhitilafiana.” Ni msingi mwingine.

Maana ya kauli ya wanavyuoni: “Kuepukana na kuhitilafiana kunapendekezwa.” kwamba anayeamini kuwa jambo fulani linajuzu aache kitendo chake ikiwa mtu mwingine anaamini kuwa kitu hiki ni haramu. Halikadhalika katika upande wa uwajibu inapendekezwa kwa yule anayeona kuruhusiwa kwa jambo kulifanya ikiwa wapo Maimamu wanaoliona kuwa ni wajibu, na hilo ni ili lisije likamfanya aanguke katika jambo lililoharamishwa au kuchukizwa na kwamba kila upande hazisemi hivyo.

Wanazuoni wengi wameutumia msingi huu katika masuala mengi yenye utata, ikiwa ni pamoja na: Al-Zarkashi, Al-Ezz Ibn Abd Al-Salam, Al-Taj Al-Sobky, Al-Suyuti, na Al-Jarhazi, mwandishi wa kitabu cha “Al-Fauaid Al-Janiyah”, na wakaeleza kuwa ni jambo la kupendekezwa kwa Muislamu kutilia maanani kuhitilafiana kwa Maimamu, na kwamba kuepukana na kuhitilafiana ni bora zaidi kuliko kujihusisha nayo.

Al-Taj Al-Sobki alisema: “mara moja nimechukua msingi huu kama ni dalili yaani: kuchukua tahadhari, Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi.} [Al-Hujuraat: 12], Mwenyezi Mungu ameamuru kuepuka baadhi yasiyo madhambi kwa hofu ya kufanya yaliyo madhambi, na hivyo ni kuchukua tahadhari, nayo ni ufahamu mzuri.”

Al-Jarhazi alisema: “Katika Aya, kuna ombi la kuhifadhi kwa mambo, na imechukuliwa kutoka kwa ombi hili kupendekezwa kwa kuepukana na kuhitilifiana. Kwa sababu ni miongoni mwa jambo la kuhifadhi.”

Wametoa dalili ya hilo kutokana na Hadithi iliyopokelewa katika Sahihi mbili kutokana na Hadithi ya Bi Aisha R.A. alisema: “Saad Ibn Abi Waqqas na Abdu Ibn Zamah waligombana kuhusu mtoto, Saad alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Utbah Ibn Abi Waqqas mwana wa ndugu yangu aliniambia kuwa mtoto huyo ni wake, uangalie anafanana naye. Abdu Ibn Zamah alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, huyo ni ndugu yangu, alizaliwa kitandani mwa baba yangu, Mtume S.A.W. akamwangalia akamwona anafanana na Utbah, akasema: Ewe Abdu Ibn Zamah mtoto huyo ni wako, mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa (yaani mume au bwana wa  mjakazi), na mzinifu haki yake ni kupigwa mawe, ewe Sawadah binti Zamah ujifiche mbali naye. Wakati alipoona ufanano wake na Utbah. Basi Sawadah hakumwona kabisa”.

Mtume (S.A.W) akachukua hadhari na akazizingatia hukumu zote mbili, ni kumaanisha hukumu ya kitanda na hukumu ya ufanano, hivyo kwa kumuambatanisha mtoto kwa mwenye kitanda – ambaye ni Zamah - alizingatia hukumu ya kitanda, na kwa kuamuru Sawda, (R.A), kujificha mbali na mtoto aliyeambatanishwa na baba yake, akizingatia hukumu ya ufanano huu.

An-Nawawiy anasema kuhusu jambo la kuhifadhi: “Mtume (S.A.W) alimwamuru Sawda kwa jambo hilo – yaani kujificha mbali na mtoto- ili kumhifadhi; kwa sababu yule mtoto katika Sharia ni ndugu yake kwa sababu aliambatanishwa na baba yake, lakini Wakati alipoona ufanano wake na Utbah Ibn Abi Waqqas akaogopa kuwa labda mtoto yule atakuwa mgeni kwake, kwa hivyo alimwamuru ajifiche mbali naye kumhifadhi.”

Imepokelewa kutoka kwa Bi. Aisha (R.A) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alisema: “Mwanamke yeyote anayeolewa bila idhini ya walii wake ndoa yake ni batili. (Mume) akimuingilia mwanamke huyo ana haki ya kupata mahari kwa alichohalalishia tupu yake. Wakishindana  basi Sultani (mtawala) ni walii wa asiyekuwa na walii”.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alihukumu ubatili wa mkataba huo wa ndoa, na sharti lake ni kutozingatia yale yaliyomo ndani yake, bali alifuata yale yaliyolazimu kuzingatiwa baada ya kutokea, ambayo ni uthibitisho wa mahari, na kwa maneno mengine, Mtume (S.A.W) alitoa kila dalili kati ya hizo mbili baadhi ya yale anayohitaji mwingine.

Vile vile Msingi huu unathibitishwa kwa Hadithi ya An-Nu’man Ibn Bashir (R.A) anaposema: nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W) akisema: “Halali iko wazi na haramu iko wazi, na baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui. Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara huingia ndani (ya shamba la mtu). Hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allah ni makatazo Yake”.  Na miongoni mwa vitu venye shaka ni vitu ambavyo Wanachuoni wamehitilifiana kuhusu uhalali wake na uharamu wake.

Miongoni mwa mifano ya matawi ya kifiqhi yaliyotajwa na wafuasi wa madhehebu, ambamo kuhitalifiana kunazingatiwa yafuatayo:

Al-Haksafi alisema katika Kitabu cha "Al-Durr Al-Mukhtar" wakati wa alipokuwa akizungumzia hukumu za ndoa: “Inapendekezwa kumwambia, kutoa hotuba, na kuwa Msikitini, siku ya Ijumaa, kwa mkataba sahihi na mashahidi waadilifu.”  Ibn Abdiyn alisema: “Kwa mkataba sahihi na mashahidi waadilifu” Hairuhusiwi kufunga ndoa ya mwanamke bila ya kuwepo kwa yeyote miongoni mwa ukoo wake, wala kwa mwanamke mzinifu, wala kwa mashahidi wasio waadilifu, ili tuondoe kuhitilifiana na Imamu Ash-Shafi.

Sheikh Al-Dardir alisema alipokuwa akizungumzia Sunna za Swala: “(Na nia ya kutekeleza inapendekezwa) katika hali ya sasa, ili kuondoa kuhitilifiana.” As-Sawiy alisema: “Kauli yake (ili kuondoa kuhitilifiana), yaani kuhitilifiana kwa wale wanaosema ni wajibu”.

Ibn Hajar Al-Haytami amesema: “Huharakisha kwa aliyokosa... na ni sunna kuipanga na kuitangulia” ikiwa ameikosa kwa udhuru (kabla ya kuswali Swala ya hivi sasa ambaye haogopi kuikosa), na kama akiogopa kukosa Swala ya jamaa; Kuondokana na kuhitilifiana kwa wale waliowajibisha hilo”.

Al-Bahwati amesema: “Na ni bora zaidi kuchinja iliyo wajibu kwa ajili ya Hijja katika Mina, na kuchinja iliyo wajibu kwa Umra katika Marwah” Kuondokana na kuhitilifiana kwa Imamu Malik na waliomfuata.”

Lakini, kuna masharti ambayo lazima yatimizwe ili msingi huu utekelezwe:

La kwanza ni Kuwa: Tofauti ni yenye nguvu, kama tofauti ni dhaifu basi haizingatiwi. Al-Dardiir anasema katika «Al-Sharhul Kabiir» akizungumzia hukumu zinazoondolewa na zisizoondolewa: “Hairuhusiwi kwa Mufti kutoa Fatwa kwa utata wa hukumu iliyotolewa na kiongozi, hali hii kuhusu tofauti inayozingatiwa kati ya wanavyuoni, lakini suala ambalo ni dhaifu kwa sababu limepingana na matini au imedhihirisha kipimo au makubaliano basi linaondolewa”.

As-Suyuti alielezea sharti hili akisema : “Tofauti iwe yenye nguvu ili isiwe dhaifu” kisha akatoa mfano kwa tofauti ambayo ni dhaifu akisema: "Kufunga katika safari ni bora kwa wenye nguvu. Na hakutilia maanani kauli ya Daud aliyesema kuwa: Hairuhusiwi kufunga katika safari. Imamu wa Misikiti Miwili Mitukufu (Al-Haramain) amesema katika suala hili: Wachunguzi hawazingatii tofauti katika maoni ya wenye Madhehebu ya Adhahir”.

Al-Khatib Al-Sherbiny anasema: “Na Mwanachuoni hakanushi suala lolote isipokuwa kwa kauli moja katika kukanusha, silo suala lenye utata isipokuwa mtendaji anaona uharamu wake. Kama ikisemwa: Wamesema kuwa Imamu Hanafi amesema, anaadhibiwa kwa unywaji wa mvinyo, ijapokuwa ukanushaji kwa vitendo ni bora zaidi kuliko ule wa maneno. Inajibiwa kwamba dalili za kutokukataza mvinyo ni dhaifu, na hivyo tofauti inawekwa kati ya adhabu ya unywaji pombe na kutoadhibiwa kwa mwenye kuoa bila ya walii.

La pili: kutosababisha kuzingatia tofauti katika maoni kuacha Sunna iliyothibitika, au kuvunjwa kwa makubaliano.

La tatu: Kwamba mchanganyiko wa madhehebu uwezekane, vinginevyo haiachwi imani yake kuzingatia uwezekano; Kwa sababu katika hilo ni kujiepusha na yale ambayo alilazimika kuyafanya kwa kufuata yale aliyoyadhania zaidi, na hali hii haijuzu kabisa. Mfano wa hili ni: Kauli ya Abu Hanifa kwamba ni lazima ibainishwe katika siku ya Ijumaa. Haiwezi kutiliwa maanani na wale wanaosema: Iwapo watu wa vijijini watafikia idadi ambayo inafanyika mkusanyiko wa Ijumaa, lazima washikamane nao - yaani: Ijumaa - na Swala ya Adhuhuri haiwatoshi..

La nne: Usitarajie mazingatio katika tofauti nyingine, kwa hivyo tunahitaji kuiondoa tofauti, kwa hivyo jukumu ni la lazima, na mfano wake: kutenganisha Swala ya Witri ni bora kuliko kuunganisha, na ikhtilafu ya Abu Hanifa haikuzingatiwa; Kwa sababu miongoni mwa baadhi ya wanazuoni ambao hawaruhusu kuiunganisha.

La tano: Mpingaji awe miongoni mwa wanavyuoni wanaozingatiwa, na kuhusu jambo hili Sheikh/ Mohamed Hassanein Makhlouf anasema katika kitabu chake: (Bulugh As-Suul fi Madkhal Elmul Usuul uk.15, Mustafa Al-Halabi): “Wanachuoni wa Usuul na  miongoni mwa Wanavyuoni na wengine walizingatia maneno ya wenye jitihada juu ya wenye kufuata kama ni dalili za Kisharia zinazohusiana na wenye jitihada, sio kwa sababu maneno yao ni hoja kwa watu inayothibitisha hukumu za kisheria kama maneno ya Mitume A.S. basi hakuna yeyote anayesema hivyo, lakini kwa sababu maneno yao yanategemea kasoro za Sharia, wamefanya bidii katika kuzisoma na kuzichunguza dalili zake pamoja na uadilifu wao na kuelewa kwao, kuzingatia kwa udhibiti wa Sheria na kuhifadhi matini zake, Kwa hiyo waliweka sharti kuhusu mwenye kuzalisha dalili anayefahamu hukumu za Sharia kutoka dalili zake kuwa na uwezo maalumu, nguvu maalumu, kipawa maalumu kinachomwezesha kuchunguza dalili kwa njia ya kufanya dhana zake ni kama elimu iliyothibitika kwa ajili ya kulinda hukumu za Dini mbali na makosa kama iwezekanavyo”.

Sehemu ya kwanza: Maelezo ya msamiati wa msingi huo

Mzizi wa kiisimu wa kukanusha (Nakara), Ibn Fares alisema: “Nun, Kaf, na Ra’a ni mzizi sahihi ambao unaonesha ukinzani wa elimu ambayo moyo unakaa ndani yake. Alikanusha jambo hilo na akalikanusha: moyo wake haukukubali na ulimi wake haukukiri.

Mwenye kukataa ni kinyume na mwenye kujua, na kila kibaya kinachokatazwa na Sharia ndicho kinachokataliwa.

kukataa kinyume na kukiri, na miongoni mwa maana zake ni kukanusha na kujinga.

Mwenye kufuatilia maana za kukataa katika matumizi ya wanavyuoni anakuta kwamba kitenzi hicho kina maana mbili, nazo ni: mabadiliko na kukataza, basi kukataa kulitajwa katika maneno ya wanavyuoni kwa maana zifuatazo :

Pingamizi,

 Kuzuia,

Taarifa ya udhaifu wa kusema,

Ukosefu wa utambuzi kwa kusema au kwa kitendo,

Kasoro ya mkosaji,

Kulauma, unyanyasaji,

Kuhubiri, kuomba, kutakaza, na adhabu.

Ni wazi kutokana na maana ambazo tumezitaja kwamba tunamaanisha kwa kutokataa kazi yeyote, si kusema kwa hukumu, migogoro ni katika kazi maalumu, kwa hivyo mijadala ya kisayansi kati ya wanavyuoni inajitokeza kama tunavyoona. Kwa hivyo basi mijadala ni kukataa hukumu, pamoja na kujua kwa wanaojadiliana kwamba kila mmoja wao hakatai kazi kwa yanayosemwa na upande mwingine.

Ama neno la ikhtilafu imechukuliwa kutoka katika kitenzi cha (Khalafa : alipinga), inasemekana: alimpinga kwa jambo alilomuasi, au alikusudia baada ya kulikataza, na Al-Khilaf ni kinyume chake.

Neno la Khilaaf (kinyume) na neno Ikhtilaaf (kutokukubaliana) maana yake ni moja, linapotumika katika lugha au katika istilahi, na huwa inajitokeza hali hiyo katika maneno ya baadhi ya wanavyuoni na wataalamu wa lugha na wataalamu wa Fiqhi. Wakati mwingine wao hutumia maneno mawili haya kwa maana moja. Kila mambo mawili moja wapo likipingana na lingine, basi huwa yametofautiana sana. Kutokana na hivyo, maneno ya wanavyuoni kutoka katika madhehebu ya Hanafi katika [Al-Fataawa Al-Hindiyah 3/312, Dar Al-Fikr]: “Kama wanavyuoni waliotangulia wakitofautiana kwa maoni mawili, kisha wanavyuoni waliokuja baada yao wamekubaliana kuhusu oni moja la kauli hizi. Je, makubaliano haya yanaondoa mzozo uliotangulia? Waliyoyaelezea mwanzoni kwa kutokukubaliana ni yale yale waliyoyaelezea katika mara ya pili kwa kupinga, kwa hivyo haya yote ni jambo moja.

Katika “Ad-Durr Al-Mukhtar kwa Al-Hasfaki: “Asili ni kwamba mahakama yanaruhusiwa katika hali ya kutokukubaliana siyo katika hali ya upinzani, na tofauti kati yao ni kwamba hali ya kwanza ina dalili na ya pili haina dalili, Ibn Abdin alisema kuwa: “(kauli yake: na tofauti ni)  huu ni ubaguzi wa kimila kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wala hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho} [AL BAQARAH 213] Vile vile Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana} [AL BAYINAH: 4] hakuna dalili kwao, na maana ya hivyo ni: Mzozo ambao hauna dalili kwa mujibu wa mkosaji, au mwenye kusema alipitisha dalili”.

Na miongoni mwa wanavyuonini waliotofautisha kati ya maneno mawili haya ni, Abul baqaa aliyesema katika kitabu cha Al-Kulliyaat: kutokukubaliana: Ni kama njia ambayo ni tofauti lakini makusudio ni moja. Mzozo ni kwamba njia na makusudi ni tofauti. Kutokukubaliana: Ni hali ya kutegemea dalili, lakini mzozo hali yake haina dalili.

Al-Tahanawi ni mmoja miongoni mwa waliotaja tofauti kati ya maneno haya mawili katika istilahi, alisema: “Baadhi ya Wanavyuoni walisema kuwa: kutokukubaliana kunatumika kwa maneno yanayotegemea dalili, na tofauti haina dalili kwayo ... na inasisitiza hivyo kuwa rai isiyochaguliwa inaitwa ni tofauti siyo kutokukubaliana”.

Ar-Raghib Al-Asfahani anasema: “Al-Ikhtilaaf (kutokukubaliana) na Al-Mukhalafah (Ukiukaji) ni: Kwamba kila moja inachukua njia nyingine katika hali yake au kauli yake. Ama mzozo ni: Ni neno la kiujumla zaidi kuliko kutokukubaliana, kwa sababu maneno ambayo ni kinyume ni tofauti na siyo maneno ambayo ni tofauti ni kinyume”

Muhtasari ni kwamba tofauti ni ya maneno tu, na si zaidi ya istilahi tu.

Sehemu ya pili: hukumu ya kukana katika masuala ya Utata

Wanavyuoni wote yanasema kuwa hakuna kukana katika masuala tata. Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad kwamba anakanusha kitu kinachojadiliwa. Ibn Taymiyah na Ibn Al-Qayim walitofautisha kati ya masuala tata na masuala ya Jitihada. Wakati wa kuzingatia na uchunguzi wa suala hili, tunakuta kuwa tofauti ni ya tamko tu, taarifa ni kama ifuatavyo:

makusudi ya masuala tata kwa Wanavyuoni wa Umma ni yale masuala yanayofichwa maana yake, kwa ajili ya kutokukubaliana juu yao, au kwa ajili ya kutokuwepo kwa dalili, kila suala ambalo halina matini inayohusiana nalo, au lina matini inayothibitika, basi suala hili ni la utata. Hii ina maana kwamba kuwepo kwa matini inayothibitika haina maana ya kuondoa utata, isipokuwa kama makubaliano yakifanyika juu ya kuainisha maana moja inayowezekana, hali ile kama kauli ya kiongozi kuhusu kuondoa  tofauti.

Udhibiti huu unatumika kwa baadhi ya masuala ya maneno na masuala mengi ya Kifiqhi. Hivyo, kwa sababu inajulikana kwamba wenye jitihada hawawezi kuathiriwa na tofauti katika masuala yenye matini inayothibitika, lakini tofauti yao ni bado katika masuala yasiyo na matini, na masuala yenye matini lakini isiyothibitika.

Wanavyuoni walieleza tofauti kuwa inayozingatiwa, nayo ambayo ina bahati ya kuiangalia, yaani: kutoka dalili, maana suala lisilo na dalili hailizingatiwi, au lina dalili lakini haina nguvu.

kwa hiyo, wanavyuoni waliweka masharti yanayofanya tofauti yao inazingatiwa, na yanayotajwa chini ya masharti hayo yanazingatiwa, na masharti hayo yametajwa tunaposema kuwa kuondoa hitilafu ni jambo linalopendekezwa.

Kulingana na hapo juu, hitilafu imegawanywa katika sehemu mbili:

Ya kwanza: Inaonekana wazi na inategemea dalili na misingi, pia inategemea vyanzo vya jitihada na kuelewa hukumu, hali hii ni kinyume na mambo yanayozingatiwa, hii ni maana ya maneno yao: Hapana kukanusha katika masuala tata, wanavyuoni wanaoiunga mkono sehemu hii ni wengi. Kuhusu hivyo,Al-Shatibi anasema: “Tofauti inayozingatiwa ipo katika masuala mengi ya Sheria, lakini tofauti isiyozingatiwa ipo chache”(Al-Mwafaqaat 1/105), na kutokana na hivyo, kuna mengi ya masuala tata katika zama zilizopita na hivi sasa, miongoni mwao ni: Kuoa bila ya Walii, na kula kilichoachwa kutajwa jina la Mwenyezi Mungu baada ya kuchinjwa,  kunyoa ndevu, na kuweka fedha katika mabenki ya kawaida, bima katika zama hizi ... nk.

Ya pili: Ni yenye ufahamu dhaifu, na mwenye kuelekea mbali na dalili, hii inarudishwa kwa mwenye kusema hivyo, sehemu hii ina majibu ya baadhi ya Maimamu  juu ya baadhi yao, kukanusha kwa maneno yasiyo ya kawaida.

Wanavyuoni wa Umma waliondoa baadhi ya mambo katika kukanusha masuala tata, miongoni mwao ni: Udhaifu wa ufahamu, jambo hili limepita. Miongoni mwao pia ni: Hukumu ya kiongozi. Kama Wanavyuoni wametofautiana kuhusu uhalali na uharamu wa jambo fulani, huletwa suala hilo kwa kiongozi, lazima atoe Fatwa kwa mujibu wa itikadi yake, na hukumu yake inaondoa tofauti hii. Miongoni mwao pia ni: Mwenye kukanusha awe na haki katika masuala tata. Mume ana haki ya kumzuia mkewe kunywa mvinyo mchache kama mkewe akidhani inaruhusiwa. Miongoni mwao pia ni: Kwamba anayefanya jambo la haramu anaitikadi kuwa jambo lile ni haramu tena analifanya, na hivyo kwa sababu amekiuka uharamu kwa mujibu wa itikadi yake, si kwa sababu anaitikadi kuwa ni halali.

Wanavyuoni wa Umma wametoa dalili kwamba katika masuala tata hayakanushwi kwa kuwa moja ya maoni mawili si bora zaidi kuliko ya mengine; kwa sababu masuala ya kifiqhi ni ya kidhana tu, na dhana inawezekana kupingwa, na hakuna ubora kati ya dhana na nyingine. Na kwamba kila mwenye jitihada ni mwenye kupatia, au mwenye kupatia ni mmoja ambaye hatumfahamu na wala hakuna dhambi juu ya asiyepatia, lakini kama akimshauri aache tofauti basi inapendekezwa hivyo.

Al-Jarhazi anasema katika kitabu cha «Al-Mawahib Al-Sunniah»: (2/333, Darul Bashair): “(Wakasema masuala amabayo ni utata hayakanushwi) huu ni msingi mkubwa unaotokana na tawi kubwa; kwa sababu uhusiano wake kwa yaliyoharimishwa si bora zaidi kuliko uhusiano wake kwa yaliyohalalishwa”. Al-Fadani amesema: “(kwa sababu uhusiano wake) yaani: Ni jambo lililojadiliwa (kwa yaliyoharimishwa) yaani: Mwenye jitihada amesema juu uharamu wake kama Ash-Shafi aliyeharamisha mvinyo kwa mfano, (zaidi kuliko uhusiano wake) yaani: Ni jambo lililojadiliwa (kwa yaliyohalalishwa), yaani mwenye jitihada aliyesema kwa uhalali wake kama Abu Hanifa alihalalisha mvinyo, kwa mfano”.

Sheikh Zakaria Al-Ansari anasema: “(wala hakatai) Mwanachuoni (isipokuwa yaliyokubaliwa kwayo) yaani: Kuhusu kuyakataa, si yale yanayojadiliwa, au mkosaji anaona uharamu wake, kwa sababu kila mwenye jitihada ni mwenye kupatia, au mwenye kupatia ni mmoja ambaye hatumfahamu na wala hakuna dhambi juu ya mkosaji”

Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ahmad kwamba anakanusha jambo ambalo lina mjadala kwa mwenye kufuata na mwenye jitihada hakanushwi, pengine mapokezi hayo yanazuia yaliyotangulia, kwamba mapokezi yaliyotangulia– ambayo yanaruhusu kukanusha jambo lenye mjadala - Ibn Moflih ameiona ni kukana kauli iliyopingana na dalili yenye nguvu au habari ya mmoja. Lakini Ibn Rajab kwa upande mwingine, alisema: “Iliyojulikana kuhusu Imamu Ahmed ni kukanusha kwa anayecheza Chess, na Al-Qadhi alieleza kuwa anayecheza pasipo na jitihada au kuiga, ambapo hali hii inawezekana kujadiliwa, Iliyojulikana kuhusu Imamu Ahmed ni kumwadhibu anayekunywa mvinyo aliyejadiliwa na kutekeleza adhabu ni kiwango cha juu zaidi cha kukanusha, ingawa hakuwa mpotovu kwake, hii inathibitisha kwamba Imam Ahmed anakanusha kila linalojadiliwa kwa udhaifu kwa kuonesha Sunna juu ya uharamu, wala mwenye kutenda uharamu huo hatoki mbali na uadilifu”.

Ama kuhusu kutofautisha kati ya Ibn Taymiyah, Ibn Alqayim, Al-Shawkaani na waliowaunga mkono katika masuala tata na masuala ya jitihada, Ibn Taymiyah anasema: “Kauli yao kwamba  masuala tata hayana kukanusha mtazamo huu si sahihi, ukanushaji unaelekeza kauli kwenye hukumu au kwenye kazi, ya kwanza -nayo ni kauli kwenye hukumu-, kama kauli ni kinyume na Sunna au makubaliano ya zamani ni lazima kuikanusha kwa muwafaka, kama si hivyo,basi inakanushwa hali ya kuonesha udhaifu wake kwa anayesema kuwa mwenye kupatia ni mmoja tu, nao ni wanavyuoni wa Fiqhi na wanavyuoni waliotangulia. Ama kuhusu kazi: Kama ikiwa kinyume na Sunna au makubaliano ni lazima kuikanusha kwa mujibu wa viwango vya ukanushaji. Vile vile hukumu ya kiongozi inabatilishwa kama ikiwa kinyume na Sunna, hata kama ikifuata baadhi ya wanavyuoni.

Na kama hakuna katika suala fulani Sunna wala hakuna makubaliano, lakini kuna jitihada, basi atakayefuata rai ya jitihada hakanushiwi. Utata huu uliingia upande mmoja, nao ni mwenye kusema hivi anaaminika kuwa masuala tata ni masuala yanategemea jitihada kama walivyodhani jamii ya watu, na haki ambayo Maimamu wanaisisitizia ni kwamba masuala yanayotegemea jitihada hayana dalili ambayo ni lazima kuifuata, kama vile Hadithi Sahihi ambayo haina upinzani kutokana na jinsi yake, basi inaruhusiwa kuifuata, lakini kama kuna Hadithi nyingine kinyume na ile inaruhusiwa kufuata jitihada kwa sababu kuna dalili zinafanana au kwa sababu ya kuficha dalili. Kama ikitajwa kwamba suala hili limethibitika, basi hakuna tuhuma kwa wapinzani miongoni mwa wenye jitihada kama masuala mengine yote ambayo wanavyuoni waliotangulia walitofautiana, ingawa tumehakikisha kuhusu usahihi wa mtazamo mmoja miongoni mwa mitazamo miwili”.

Ibn Al-Qayyim pia alisema kama yaliyotangulia hapo juu, pia alisema katika kitabu cha: [Ilaam Al-Mwaqiin 3/288]: Wakati alipotoa dalili ili kuthibitisha kauli yake: “Namna gani mwanachuoni wa Fiqhi anasema kuwa hairuhusiwi kuyakanusha masuala tata, pindi Wanavyuoni wa Fiqhi wamesema kuwa inaruhusiwa kuibatilisha hukumu ya kiongozi kama ikiwa kinyume na Qur`ani au Sunna”.

Sababu ya tofauti baina ya Ibn Taymiyah na Ibn Al-Qayim katika masuala tata na masula yanyaotegemea jitihada ni kwamba masuala yanayotegemea jitihada hayana matini katika Qur`ani au katika Sunna au hata makubaliano, lakini masuala tata ni kinyume na hayo, na kwamba yeye anamkana mkiukaji katika hali ya pili, bila ya kumkana katika hali ya kwanza. Kwa maneno mengine: masuala yanayotegemea jitihada ni yale tata na yanahitaji kuyatilia maanani.

Hayo Makundi mawili yanakubaliana kwamba masuala ambayo yana matini au makubaliano – yakinifu – basi huwa anakanushwa mkiukaji ambapo makundi yote mawili yanayayaita masuala haya kuwa ni tata, lakini masuala yanayojadiliwa na hayana dalili inayoyathibitisha, basi makundi haya mawili yameafikiana kuwa hakuna kukana mkiukaji, ingawa Wanavyuoni wa Umma wanayaita masuala haya kuwa ni tata kama yale ya kwanza. Na Ibn Taymiyah pamoja na Ibn Al-Qayim wanayaita hayo kama masuala yanayotegemea jitihada, na istilahi zote ni sahihi. Ni kweli kwamba masuala haya ni tata kwa sababu sio ya kutokukubaliana nayo, vile vile ni masuala yanayotegemea jitihada kwa sababu jitihada inaruhusiwa ndani yake.

Zaidi ya hayo, kila suala tata, kwa kweli, ni suala linalotegemea jitihada za wanazuoni kwa sharti kuwa utata huo uwe unazingatiwa kama iliyotangulia kuelezwa hapo juu. Lakini kama utata haukuzingatiwa, basi suala hilo halitegemei jitihada. Ukweli ni kwamba suala hilo ni tata, na utata huo hauzingatiwi, na kama ipo tofauti basi ni kati ya masuala ya Ijtihadi na masuala tata ambayo hayazingatiwi.

Katika hotuba yenye thamani ya Dakta Al-Qaradhawi, ambamo anaijibu hoja ya Ibn Al-Qayyim, anasema: “Hotuba ya Imam Ibn Al-Qayyim inakubalika, na baadhi yake inahitaji mjadala. Inakubalika kukemea yale yanayopingana na hukumu ya mtawala kwa makubaliano, na ni yale yanayopingana na matini za Qur’ani Tukufu, au matini za Hadithi sahihi, au maafikiano ya uchamungu yasiyoegemezwa kwenye desturi au maslahi ya kimuda.

Bali tulisema matini sahihi, na tunamaanisha kwayo kuwa ni dhahiri ya dalili ili isichukue kipengele kingine, kwa sababu kilichowezekana kufasiri na kuhalalisha ijtihad ndani yake, haijuzu kuikanusha kwa yeyote aliyesema kwayo, hata kama inapingana na iliyo dhahiri, na kuna mifano mingi ya hii katika madhehebu yote, hata kama viwango vya tafsiri vinatofautiana ndani yake.

Na kuzuilia kwetu Sunna kwa Sahihi ili itoke isipokuwa kwa Hadithi Sahihi, na tunataka kwa Sahihi yale ambayo yameafikiwa juu ya usahihi wake, ama kwa yale ambayo wengine wameyarekebisha na wengine wakaacha, au yamesahihishwa na wengine katika idadi ya njia, au kulikuwa na msimulizi tofauti ndani yake, na kadhalika, basi inahalalishwa kwa mfano wake kwa ijtihadi na kutofautiana, na haijuzu kuikanusha kwa wale wanaoivunja.

Ama kuhusu uzuiaji wetu wa makubaliano kwa yakini, hii ni kwa sababu madai mengi ya kauli moja hayakuthibitishwa kwa yakini, bali kutokubaliana kulithibitishwa ndani yake. Bali baadhi yake ile iliyokhitalifiana nayo ndiyo ilikuwa sahihi zaidi na yenye uwezekano mkubwa zaidi kuliko nyingine, kama kwamba makubaliano yakiwa yameegemezwa kwenye desturi au maslahi yalibadilika kufuatana na mabadiliko yake, na hukumu inaendana na sababu yake kama ipo sababu au haipo.

Muhimu ni kwamba kinachopingana na Qur’ani yenye maamuzi na Sunna sahihi yenye maamuzi au makubaliano kwa yakini, basi kukanusha ni halali, na huenda ikawa ni wajibu. Ama mengine yasiyokuwa hayo, ndiyo yenye kuhitaji mjadala. Baadhi ya yale yaliyotajwa na Ibn al-Qayyim, ikiwa tuna hakika kwamba moja ya rai hizo mbili ni sahihi, inaweza isikubaliwe kabisa naye. Baadhi ya rai hizi zinapendelea dhehebu ya fikra zaidi kuliko dhehebu lengine la fikra ambalo wafuasi wake wanaweza kulitetea, na hiyo ni kama suala lisemalo (Muislamu hawezi kuuawa kwa ajili ya kafiri) na madhehebu ya Hanafi yanajulikana sana, ambayo ni tafsiri ya kafiri. kwa vita, na hii ni sawa na alivyokwenda Ibn al-Qayyim mwenyewe kwa mujibu wa sheikh wake Ibn Taymiyyah katika kuruhusiwa kumrithi Muislamu kutoka kwa kafiri, na wao wanaipendelea rai hii, nayo ni Imepokewa kutoka kwa baadhi ya waliotangulia, na inapingana na maana ya dhahiri ya Hadithi sahihi: “Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi Muislamu.” Hadithi hii pia imekubaliwa. Na Hadithi nyingine isemayo: “Hawarithi watu wa dini mbili” pia baadhi ya hukumu zilizotajwa ambazo ndani yake upinzani na madhehebu ya Maliki, Hanafi au Shafi. Je, hii inamaanisha kuondolewa kwa madhehebu mengine?

Kisha, kuzingatia madhehebu au maoni juu ya suala fulani kuwa dhaifu au isiyo ya kawaida mara nyingi ni suala la usawa, maoni dhaifu yanaweza kuja yanayoyaimarisha, maoni yaliyoachwa yanaweza kutoka kwa mtu anayeyaeneza, na maoni yasiyo ya kawaida yanaweza kuja wakati ambayo yanajulikana. Ibn Taymiyyah (R.A) mwenyewe, kama vile mitazamo yake juu ya mambo ya familia na talaka, na yanayohusiana nayo, ambayo ndiyo aliyojaribiwa kwake na alidhuriwa kwa ajili yake, na alipelekwa gerezani zaidi ya mara moja mpaka akafa. Kama tukitekeleza yale ambayo yaliyosemwa na Ibn Taymiyyah na Ibn al-Qayyim kwa mujibu wa rai za Sheikh Al-Islam, ni lazima tuzikanushe kwa nguvu zote kwa sababu ziko kinyume na makubaliano tangu zama za Umar”.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu; utajua kwamba masuala ya utata ambayo yanakusanya mambo yote ambayo yalipelekea hitilafu, hata yakiwa na udhaifu, au yasiyo ya kawaida, au miongoni mwa makosa ya wanavyuoni, na kama ni hivyo basi yatarejeshwa. Basi masuala haya yanakusudiwa ni yale ya utata, na utata wake unazingatiwa kwa masharti yake yenyewe yaliyotajwa hapo juu.

Na Mweyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas