Hukumu ya kumsomea maiti baada ya k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kumsomea maiti baada ya kuzikwa

Question

Ni ipi hukumu ya kumsomea maiti baada ya kuzikwa?

Answer

Kumsomesha maiti ni Sunna kutoka kwa Mtume (S.A.W.), ambapo Wanachuoni wa Hadithi za Mtume wamesisitiza kuwa Mtume alikuwa anasisitiza Sunna hii, pia, Wanachuoni wengi pamoja na watafiti wa Fiqhi wamehakikisha uhalali wake, licha ya kuifuata Sunna hii bila ya kupingwa na yeyote, kwa hiyo haikubaliki kuharamisha Sunna hii ya kumsomea aliye kufa au kumtuhumu anayefanya hivyo kuwa amefanya kosa au dhambi kwani ni kinyume cha rehma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake.

Wala haijuzu kuwa suala kama hili liwe sababu ya kuchochea fitina na mfarakano baina ya Waislamu, bali tunatakiwa kuwajibika kwa adabu za kutofautiana na kuheshimu yaliyozoelewa kufanywa kuhusiana na suala hili.

Share this:

Related Fatwas