Hukumu ya kufanya ziara kwa makabur...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kufanya ziara kwa makaburi ya wazazi

Question

Ni ipi hukumu ya kufanya ziara ya makaburi ya wazazi waliofariki siku ya Ijumaa kila wiki na kusoma Qur`ani kando ya makaburi yao?

Answer

Kufanya wema kwa wazazi ni jambo linalotakiwa milele, wala haliishi katika hali maalumu, wala katika muda fulani, na linatakiwa kufanywa wakati wa uhai wao na baada ya kufariki kwao, na miongoni mwa kufanya wema na hisani kwa wazazi baada ya kufariki kwao: kufanya ziara kwenye makaburi yao; kwa mujibu wa kauli yake Mtume (S.A.W.): “Nimewahi kuwakataza kutembelea makaburi, basi mnaruhusiwa kuyatembelea, kwani ziara hizo huwa na mafunzo na mawaidha” imesimuliwa na Abu Dauud, na kuhusiana na kufanya ziara kwenye makaburi ya wazazi hasa Mtume (S.A.W.) alisema: “Yeyote anayefanya ziara kwenye kaburi la wazazi wake siku ya Ijumaa kila wiki au mmoja wao, akasoma sura ya Yasiin, basi Mwenyezi Mungu Atamsamehe madhambi yake kwa idadi ya kila Aya au herufi”

Pia, kusoma Qur`ani kwa nia ya kutoa thawabu kwa wazazi, ambapo Hadithi za kuthibitisha hukumu hii ni sahihi na ziko wazi.

Share this:

Related Fatwas