Hukumu ya kujifananiza na wasio Wai...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kujifananiza na wasio Waislamu katika Mavazi

Question

Assalaamu Aleykum. Mimi  ninaishi nchini Ufaransa . Nataka kujua ni mavazi gani yanayofaa kwa kutokea barabarani, na kadhalika wakati wa Swala? Ili yasiwe yenye kuvutia (kama shati n.k.) na isifanane na mavazi ya wasiokuwa Waislamu.  Na ni ipi mipaka ya kushabihiana na wasio Waislamu katika nchi isiyo ya Kiislamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Suala la mavazi katika Uislamu linaachiwa katika mila na desturi za watu zisizopingana na Uislamu; kwa maana kuwa Uharamu huwa unapatikana kwa kwenda kinyume na mwonekano wa kiislamu kama vile mavazi yaliyovaliwa yakawa yanaudhihirisha uchi au yanaonesha kilicho ndani ya mwili na hivyo kudhihirisha uchi na maeneo yanayotakiwa kufunikwa.

Ama Muislamu anapovaa mavazi ya watu wa nchi yake – ni sawasawa wawe watu hao ni Waislamu au makafiri – huko sio katika kujifananisha kwa lolote; kwani Uislamu hauhangaikii wafuasi wake wawe na sifa ya kipekee kwa kuwa tu na sifa hiyo. Hakika mambo yalivyo ni kuwa Uislamu unawaamrisha wao kuwa na maadili mema ya kipekee na yenye kujumuisha wema na kuchunga utukufu wa binadamu pamoja na utekelezaji wa ahadi na mikataba mbali mbali, na kuchunga mfumo mkuu, na kuheshimu maadili na kuwapenda watu pamoja na kuwahurumia.

Kwa hiyo, Maswahaba walipoingia Uajemi, waliswali wakiwa wamevalia suruali zao. Na kushabihiana/kujifananisha ni haramu kwa masharti mawili: Kwanza, kwamba mavazi yenyewe ni haramu, na pili, kwamba mtu ana nia ya kufanana nao. Ikiwa hali zote mbili hazipo, basi sio haramu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas