Hukumu ya kazi kwa mwanamke na athari yake katika urithi
Question
Je, Mwanamke kufanya kazi kunaathiri haki yake katika urithi?
Answer
Haijuzu kwa sababu yeyote au katika hali yeyote kubadilisha hali ya mwanamke au kupungua kwa haki zake kwa sababu ya kwamba anafanya kazi, na kuchangia katika gharama za nyumbani akisaidiana na mumewe au baba yake, na kubatilisha mafunzo na sharia zatokanazo na matini wazi, wala si sababu ya kutoa wito ya kubadilisha sehemu zake katika urithi.
Vile vile, kuzingatia haki ya watu katika urithi huwajibisha kumkabidhi mwenye sehemu haki yake, awe na uhuru wa kutumia ile sehemu apendavyo sawa kwa kuichukua au kuiacha, wala haijuzu kumlazimisha mtu aiache haki yake katika urithi kwa kuwa anafanya kazi wala kwa sababu yeyote nyingine.