Hukumu ya kwenda kwa waganga na wachawi
Question
Ni ipi hukumu ya kwenda kwa waganga na wachawi?
Answer
Kwa hakika kuomba msaada wa waganga na wachawi na kuwategemea katika kupata manufaa na heri au kujikinga kutoka shari ni tabia iliyokatazwa katika sharia, kwa mujibu wa Hadithi iliyosimuliwa kutoka kwa Omran bin Husein (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Si miongoni mwetu anayeamini bishara za waganga akiwa yeye mwenyewe atatoa bishara au atatolewa, wala anayeamini uchawi kwa kufanya au kufanyiwa, na yeyote anayekwenda kwa mganga akamwamini, basi huwa amekufuru kwa yale yaliyoteremka kwa Mtume Muhammed (S.A.W.)” imesimuliwa na Al-Bazzar kwa isnad iliyo nzuri, naye Mtume (S.A.W.) alisisitiza kuwa kwenda kwa hawa waganga na wachawi na kuwaamini ni sababu ya kukataliwa matendo mema ya mja, akasema: “Yeyote anayekwenda kwa mganga na kumwuliza kuhusu mustakbali au hali yake akamwamini, basi Swala zake hazikubaliki kwa muda wa siku arobaini” imesimuliwa na Muslim.