Hukumu ya ndoa ya kimila za utotoni
Question
Ni ipi hukumu ya kisheria ya ndoa za kimila za utotoni?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu ulizingatia silika za asili ndani ya mwanadamu, kwa hivyo haukuzikandamiza na haukuweka suala la dini kwenye utawa. Wakati huo huo, uliihalalisha ndoa na kuinua hadhi yake. Ili kuwaepusha watu na kutumia silika na kufukuza matamanio, na kuanzisha utu wa wanawake na kuinua hadhi yao, Uislamu ulianzisha uhusiano wa ndoa juu ya upendo na huruma, na kwa ajili ya kuendelea kwake, ulizingatia utangamano na maelewano kati ya wanandoa. Wanachuoni walizungumza kuhusu hali ya utangamano baina ya wanandoa, na walitofautiana katika maelezo yake, ambayo yanaweza kutofautiana kulingana na mazingira, nyakati, mahali, desturi na tamaduni, lakini hawakutofautiana katika asili ya uhalali wake. Yaani utangamano ni lazima uwe sababu muhimu ya kutokea kwa mapenzi, huruma, na kuheshimiana kati ya wanandoa na jambo linalosaidia katika kutimiza haki za pande zote kati yao. Kwa hiyo, kufikia kanuni ya utangamano katika mkataba wa ndoa ni hitaji la kisharia na madhumuni ya kidini. Ikiwa msichana ameolewa na mwanamume asiyefaa bila ridhaa yake, basi ana hiari ya kuibatilisha ndoa hiyo kwa mujibu wa Wanachuoni wengi.
Hapa tunakabiliwa na tatizo kubwa la kijamii ambalo udhihirisho wake na vitendo vyake vimepotea maana ya ndoa ya kawaida na vipengele vya uendelevu wake, kuanzia njia ya upatanishi ambayo hufanyika kwa kutoa wasichana wa umri wa chini ili mwanamume amchague yeyote ampendaye kati yao, ambayo yote ni ukiukwaji wa utu na ubatili wa ubinadamu, kana kwamba walikuwa wajakazi au bidhaa zilizouzwa na kununuliwa. Ni muhimu kujua kuwa hii ni raha ya muda tu, sawa na ukahaba wa kujificha, na kupitia unyanyasaji wa kijinsia kwa yule aliyemuoa, na kumalizia kwa kuondoka kwake, hali ambayo anaifahamu mapema bila yeye kudhamini haki zake au hadhi ya mtoto wake ambaye anaweza kuwa tumboni mwake kutoka kwa mwanamume huyu, ili basi apewe pamoja na wale wasichana wengine ambao hutolewa tena kwa mwanamume mpya ... na kadhalika ... Kuanza mzunguko mpya wa unyonyaji huu mchafu wa wasichana wetu wanyonge, bila kuzingatia mwisho wa kipindi chao cha kusubiri au kitu kingine chochote, pamoja na madhara ya kisaikolojia na kijamii ambayo hii inahusisha, tishio la usalama wa kijamii ambalo huleta watoto masikini wa mitaani ambao huzalishwa ambao hawana ukoo unaojulikana au baba, ambao baadaye huwa mabomu ya wakati ambayo yanatishia usalama wa kijamii na amani.
Ingawa watu wenye akili timamu wanakubaliana kwamba aina hii ya ndoa ina madhara kwa mtu binafsi na jamii, na kwamba haina hata viwango vya msingi vya utangamano na hata hadhi ya kibinadamu katika ndoa, Kuna kanuni na masharti ya Sharia ya Kiislamu ambayo yanatosha kuharamisha tabia hii, kuwazuia watendaji wake, kufanya kuwa ni jinai ndani yake, na hata kufuta uwalii wa baba juu ya binti yake mdogo kama atamtupa kwenye tope hili la unyonyaji wa kingono na kunufaika na mali kwa gharama ya utu na haki zake.
Wanachuoni wamesema kuwa utangamano ni haki ya kimsingi ya mwanamke, na hairuhusiwi kumlazimisha kuiacha haki hiyo. Baadhi ya Wanachuoni waliifanya haki hiyo kuwa ni sharti la kufunga ndoa, bila yake ndoa ni batili, na baadhi yao wanaithibitisha na kumpa mwanamke haki ya kuibatilisha ndoa akibaleghe. Yaani Wanachuoni wanakubaliana kuwa utangamano ni sharti la ndoa, ama katika hitimisho lake au katika hali yake ya kufungamana kwake, basi mkataba wa ndoa bila ya sharti ile hukumu yake ni kati ya batili na uwezekano wa kubatilisha. Ingawa baadhi ya Wanachuoni wameifanya umri kuwa miongoni mwa sifa za utangamano baina ya wanandoa, hawakumfanya mzee kuwa sawa na msichana, kama Imamu Al-Ruwayani wa Madhehebu ya Shafi’i alivyosahihisha hivyo.
Mwanachuoni Al-Shihab Ahmad Al-Ramli Al-Shafi’i amesema: “Al-Ruwayani Amesema: “Mzee si sawa na msichana, na mjinga si sawa na mwanamke mwanachuoni. Mmiliki wa Al-Rawdah akasema: nayo ni dhaifu. Amesema katika kitabu cha Al-Anwar: Udhaifu huu kuhusu mjinga na mwanamke mwanachuoni. Kwa sababu ikiwa elimu ya mababa ni heshima kwa watoto, basi vipi kuhusu elimu yao, na kwa sababu ufundi unakuzwa kwa mke ingawa hauwi sawa na elimu, na imesemwa kwa makubaliano ya Al-Ruyani, mfasiri wa Mukhtasar Al-Juwayni na wengineo. Sheikh wetu amesema: Kinachotegemewa ni kile kilichomo kwenye kitabu cha Al-Anwar.”
Ijapokuwa kauli hii inasahihishwa na Wanachuoni wa kishafi na pia haikubaliki na wengi wa Wanachuoni, aina hiyo ya ndoa ya watoto wadogo haiwezi kupingwa kuwa ni kamili na kwa undani isiyo na kufaa. Iwapo Shari’a imempa mdogo jukumu la kujitegemea la kifedha na ikafanya utupaji wa mlinzi wa fedha zake utegemee juu ya riba, kiasi kwamba hairuhusiwi kutoa pesa yake isipokuwa kwa njia ambayo ni ya manufaa kwake tu, basi kuzingatia maslahi katika ndoa yake ni ya uhakika zaidi na ni wajibu zaidi. Kwa sababu heshima ni ya thamani zaidi kuliko pesa.
Imaamu Al-Nawawi Al-Shafi’iy amesema katika kitabu cha “Al-Minhaj”: “Kuna rai mbili kuhusiana na kumuozesha baba msichana bikira mdogo au mzima asiyemfaa bila ya ridhaa yake, Kwa rai ya wazi zaidi, ni batili, lakini kwa rai nyingine ni halali. Mwanamke mzima ana chaguo, na msichana mdogo ana chaguo kama akifikia balehe.
Mwanachuoni Al-Khatib Al-Sharbini Al-Shafi’iy amesema: “(Inadhihirika zaidi) kwamba ndoa iliyotajwa (ni batili) kwa sababu ni kinyume na Ghibtwa (ambayo ni kutamani alicho nacho mwenzako pamoja na kumuomba Allah akupe mfano wake au zaidi lakini bila kuondokewa au kupunguziwa kwa ndugu yako); kwa sababu walii wa pesa hawezi kuiondoa bila ya Ghibtwa, hivyo walii wa ndoa anastahiki zaidi.”
Uislamu umemfanya baba walii wa asili wa binti yake kwa sababu silika yake ya kimaumbile aliyoumbwa nayo inamfanya kuwa na huruma juu ya binti yake, na kuchagua mwanamume anayemfaa, na kumsukuma kufanya kazi kwa ajili ya maslahi ya binti yake, usalama wake na amana yake. Hata hivyo, ikiwa binti ni mdogo, baadhi ya mafakihi wanaamini kuwa hairuhusiwi kumuozesha. Haya ni maoni ya Imam Uthman Al-Batti, kama ilivyoripotiwa na Imam Al-Kasani Al-Hanafi. Pia ni rai ya Imam Ibn Shubrumah na Abu Bakr Al-Asam, kama ilivyoripotiwa na Imam Abu Bakr Al-Jassas na Imam Al-Sarakhsi. Ushahidi wao juu ya hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao.}. [An-Nisa: 6] “Kama ndoa ingeruhusiwa kabla ya baleghe, kusingekuwa na manufaa yoyote, na kwa sababu ulezi juu ya msichana mdogo umewekwa kwa haja ya mtu anayemsimamia, pia katika mambo ambayo haijatimizwa haja, ulezi hauthibitishwi, kama vile michango, na hakuna haja ya kuoa; kwa sababu makusudio ya ndoa ni, bila shaka, kukidhi matamanio, na kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, na uzao, lakini hali ya ndoa ya wasichana wenye umri mdogo inapingana na vyote viwili. Kisha mkataba huu unafanyiwa kwa umri na masharti yake yanawafunga baada ya kubaleghe, kwa hivyo hakuna mwenye haki ya kuwalazimisha kufanya hivyo. Kwani hakuna ulezi juu ya mmoja wao baada ya kubaleghe.
Mtazamo huu ulitumiwa na sheria za Misri kuamua umri wa ndoa, na kuzuia kusikilizwa kwa kesi ikiwa mmoja wa wanandoa alikuwa chini ya umri maalumu. Hata hivyo, sheria haikuzuia uhalali wa ndoa hiyo, kama Sheikh Muhammad Abu Zahra alivyoonesha katika kitabu chake.
Wanachuoni wengi walimruhusu baba - na mlezi wake kwa mujibu wa wanavyuoni wa Madhehebu ya Maliki na Hanbali - kumuozesha binti yake mdogo kutokana na huruma yake kamili, ambayo ndiyo silika yake ya kimaumbile inamwelekea. Imaam Ibn Abd Al-Barr Al-Maliki amesema: “Mwanaume ana haki ya kumuozesha mtoto wake mdogo kwa sharti ya kumwangalia, hii si haki ya mlezi yeyote asiyekuwa baba, kwa mujibu wa Imam Malik, mlezi anayo haki ya kumuozesha mtoto kwa sharti ya kumwangalia kama vile baba anayo haki.
Imaam Ibn Qudamah Al-Hanbali amesema: “Hakuna mtu mwingine isipokuwa baba au mlezi wake mwenye haki ya kumuozesha mvulana kabla hajabaleghe.
Mashafii pia walimuongeza babu kwa sababu yeye ni baba wakati baba hayupo, lakini hawakuruhusu hilo kwa mlezi mwingine yeyote.
Imaam Al-Mawardi Al-Shafi’iy amesema: “Ama mabikira wachanga, akina baba wana haki ya kuwalazimishia ndoa. Baba anamwozesha binti yake mchanga ambaye ni bikira bila kuzingatia chaguo lake, na mkataba ni wajibu kwake akiwa mdogo na baada ya kukua kwake. Vivyo hivyo, babu, hata cheo chake kiko juu kiasi gani, anachukua nafasi ya baba katika kumwozesha bikira mchanga ikiwa baba hayupo.
Hanafi walipanua juu ya jambo hilo na wakalifanya hivyo pia kwa ajili ya wenye jamaa upande wa mwanaume, na mafakihi wakaiita kesi hii “ulezi wa lazima,” na msingi wa kuanzishwa kwake ni huruma inayochochea kujali maslahi ya mtu aliye chini ya ulezi, na kuchunga mambo yake hali ya kuwa yeye ni mdogo na katika mustakbali wa maisha yake, na rai nzuri na kuchagua vipengele vya manufaa kwake, ikiwa sivyo, basi hana ulezi kwake. Kwa sababu hukumu inahusu sababu yake, kuwepo na kutokuwepo kwake.
Ama wanavyuoni walio wengi waliweka masharti kwamba mlezi lazima awe mwadilifu. Hawaamini kuwa ulezi ni halali kwa baba asiye na maadili, na wameamua kuwa kuozesha msichana kwa mtu asiyemfaa ni ishara ya uovu wa mlezi.
Mwanachuoni wa Hanbali Al-Bahuti anasema: “Ni haramu kwa mlezi wa mwanamke kumuozesha kwa asiyemfaa bila ya ridhaa yake.” Kwa sababu inamdhuru na inamletea aibu, na (mlezi anafanya uchafu) maana yake kwa kumuozesha kwa asiyemfaa bila ya ridhaa yake. Nikasema: Ikiwa (mlezi) alifanya hivyo kwa makusudi.
Ama Hanafiy walieleza kuwa uhalali wa mkataba katika suala la ulezi wa kulazimishwa ni kwamba amuozeshe binti yake kwa mwanamume anayefaa kwa mahari sawa na ya wenzake. Iwapo atamwoza kwa mwanamume asiyefaa au pasipo na mahari, basi mkataba huo si sahihi. Kuna tofauti katika usemi wao baina ya wanaosema kuwa ni batili na wanaosema kuwa wanandoa wanatenganishwa. Haya yote ni ikiwa uchaguzi mbaya wa baba haujulikani kuwa wa ufisadi au uovu. Ikiwa inajulikana, mkataba sio sahihi kwa makubaliano.
Imepokewa katika “Al-Fatawa Al-Hindiya” katika Fiqhi ya Hanafiy: “Akimwozesha mwanawe mdogo kwa mwanamke asiyemfaa, kama vile kumuozesha mwanawe kwa mjakazi au kumuozesha binti yake kwa mtumwa, au kumuozesha kwa ulaghai mkubwa, kama vile kumuozesha binti yake na kupunguza mahari yake, au kumuozesha mwanawe na kumuongezea mahari ya mke wake inaruhusiwa kwa mujibu wa Abu Hanifa, Mwenyezi Mungu amrehemu, vivyo hivyo kwenye kitabu cha (Al-Tabiin). Kwa mujibu wao, haijuzu kuzidisha au kupungua isipokuwa katika mambo ambayo watu wanadanganywa. baadhi yao walisema: Ama asili ya ndoa hiyo ni sahihi, na mtazamo sahihi zaidi ni kwamba ndoa hiyo ni batili kwa mujibu wao. Walikubaliana kwamba hii hairuhusiwi hivyo kutoka kwa mtu mwingine yeyote isipokuwa baba, babu, kama ilivyoelezwa katika Fatwa za “Qadi Khan.” Wametofautiana kuhusu uchaguzi mbaya wa baba haujulikani kwa sababu ya ukosefu wake wa ufisadi au uovu, hata hivyo, ikiwa hilo linajulikana kutoka kwake, basi ndoa ni batili kwa makubaliano.
Hapana shaka kwamba njia hiyo ya ndoa, ambayo ndani yake hakuna kuzingatia kufaa, na ambayo haina hata dalili kidogo za heshima kwa ubinadamu, ni moja ya ushahidi wa wazi zaidi wa uovu wa mlezi. Wanachuoni wa Fiqhii wamesema - kama ilivyotajwa hapo awali - kwamba baba kumuozesha binti yake kwa mwanamume asiyefaa humfanya baba kuwa mchafu, na mchafu ambaye hana uadilifu haruhusiwi kuwa mlezi kwa mujibu wa wanavyuoni wengi, hivyo basi hayupo kisharia. Yaani kuwepo kwake katika mkataba wa ndoa ni kana kwamba kutokwepo, hivyo ulezi wake unaondolewa kwa mujibu wa wanavyuoni walio wengi kutokana na uovu wake, na mkataba huo ni batili. Ulezi wake pia umeondolewa kwa mujibu wa Madhehebu ya Hanafi, kutokana na uovui wa wazi na ufisadi katika chaguo lake. Ambapo atabadilishwa kutoka kwenye maana ya ulezi - ambayo iliwekwa kwa ajili yake kwa msingi wa huruma ya asili ambayo inamsukuma kuwa na hamu ya maslahi ya binti yake na Na kumtunza katika ujana wake na mustakbali wake, na kuwa na uamuzi mzuri na kuchagua mambo ya manufaa kwa ajili yake - kwa mtu mchoyo ambaye hana uhusiano wowote na maana yoyote kati ya hizi, na ambaye hisia za baba yake zimefutika, hata yeye na mama yake wamegeuka kuwa viziwi na hamu yao ni kukusanya pesa kwa gharama ya utu na usalama wa binti yao, bila ya kuzingatia maslahi, dini, maadili, au desturi. Badala yake, hakuna hata mmoja wao aliyefanya chaguo hata kidogo. Bali, walimtoa binti yao kuwa kama mjakazi au kama bidhaa ya kununuliwa na kuuzwa kwa mwanamume huyo, miongoni mwa wasichana waliotolewa kwake, na wakaidhinisha ndoa yake kwa njia hii ya kufedhehesha, licha ya ujuzi wao wa maonyo na hatari zote zilizozunguka hilo. Waliongeza kuwa kwa kupuuza usaidizi wa binti yao alipoomba msaada wao na kuomba msaada kutoka kwao kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia aliopata kutoka kwa wale waliompata, na hata kutishia kujiua kwa sababu yake. Mlezi wake hakukidhi maelezo ambayo sharia ilimweka kuwa mlezi wake.
Kwa hiyo, tunachagua - na hali ni kama tulivyoeleza - kutoka kwa Madhehebu za maimamu zinazothibitisha kwamba tunaelekea kubatilisha aina hii ya mkataba wa ndoa kwa sababu ya ukosefu wa masharti ya kweli na nguzo za ndoa. Hakuna mtu ambaye angemtia binti yake katika hali kama hiyo isipokuwa mtu mwovu ambaye ni waziwazi hana maadili na hana uadilifu. Hii ni ndoa isiyo na mlezi anayetambulika kisharia, na hivyo ndoa basi ni batili. Vile vile huwa tunayachukulia matukio haya kutokana na matokeo yake kuwa ni unyonyaji wa kijinsia ambao kwao mhusika, wazazi, mpatanishi, na kila aliyefanikisha au kutaka kulikamilisha kwa namna hii, jambo ambalo halikubaliki kwa Mwenyezi Mungu, wala halikubaliki kwa Mtume wake – Mwenyezi Mungu (S.A.W) – wala halikubaliki kwa waumini.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
