Hukumu ya Alkoholi katika Manukato na Vipodozi.
Question
Assalaamu alaykum. Je, mfuasi wa Madhehebu ya Imamu Shafi anaweza kuvitumia vipodozi kama manukato, losheni na shampuu vilivyo na alkoholi ndani yake? Kuna mtu fulani aliniambia kwamba ikiwa alkoholi ni ya ulevi, basi inazingatiwa kuwa najisi, lakini ikiwa haina ulevi, haizingatiwa kuwa najisi. Kwa mfano, alkoholi ya Ethyl ni najisi kwa sababu ina ulevi, wakati alkoholi ya Sitisliy sio najisi kwa sababu siyo ulevi. Najua kwamba kulingana na Madhehbu ya Hanafy, mtu anaweza kutumia aina yeyote ya alkoholi isipokuwa ile iliyotengenezwa kwa zabibu na tende. Tafadhali nifafanulie hili na mniambie ni aina gani ya alkoholi inaweza kutumika kwa mujibu wa Madhehebu ya Shafi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hukumu Iliyo sahihi na inayotakiwa katika misingi ya Madhehebu ya Imamu Shafi – pia na ya Madhehebu mengine – Ni kwamba alkoholi asili yake sio najisi, na inajuzu kuitumia katika manukato na katika mambo ya usafi, madawa, na vitu vinginevyo katika matumizi nufaishi, na mtu anaposwali akiwa ametumia manukato, Swala yake ni sahihi, kwa sababu zifuatazo:
Ilivyo katika sharia ni kwamba asili katika vitu ni twahara, na japokuwa kunywa alkoholi ni haramu lakini jambo hilo halilazimishi kuwa kitu kilicho haramu kuwa ni najisi; kwani najisi ni hukumu ya kisharia na inapaswa kuwa na hoja maalumu. Mihadarati na sumu zinazo ua ni haramu ingawa ni twahara; kwani hakuna dalili za unajisi wake, kwa hivyo ilivyo katika misingi ya kifiqhi ni kwamba: Najisi inalazimisha uharamu, na uharamu haulazimishi unajisi; kwa hivyo basi kila kitu najisi ni haramu, na sio kinyume chake.
Madhehebu ya Shafi wameiita Pombe "Alkhamr" kwa ujumla ni kila kinacholewesha na kinatokana na Kinywaji cha zabibu, na wameweka masharti, ili kinywaji hicho kiwe najisi ni lazima kiwe na ladha kali inayopoteza akili, na Madhehebu ya Hanafi yameweka sharti la kuondosha povu, kisha wafuasi wa Shafi wameongeza yaliyo katika maana hiyo katika vinavyolewesha isiyokuwa kinywaji cha zabibu na pia kikiwa na ladha kali inayopoteza akili, na waliifanya hukumu yake kuwa kama pombe iliyotengenezwa kwa zabibu yaani ni haramu na najisi, lakini wafuasi wa Hanafi wanaona kwamba vinavyolewesha na havitokani na zabibu si najisi hata vikiwa ni haramu kwa upande wa kunywa. Basi kutokana na maelezo hayo alkoholi katika asili yake yenyewe si pombe mpaka iwe ni najisi, yaani najisi katika asili yake yenyewe, na hii si katika vinywaji vinavyolewesha na si kama pombe ambayo wametofautiana Wanachuoni katika unajisi wake au utwahara wake, bali hii ni mada ya sumu kama sumu zingine zote, na kwa hali ilivyo si kinywaji katika hali ya kawaida kwa kusudio la kulewa, na ilivyo ni kuwa alkoholi imeharamishwa kwa matumizi kama ni sumu kwani sumu husabibisha mauti na madhara, na alkoholi asili yake ni twahara kama utwahara wa bange na Afiyuni na kila kinachodhuru.
alkoholi si kinywaji na hainyweki, na kuwa kwake ni kimiminika hailazimishi kuwa ni najisi, na iliyozingatiwa katika Madhehebu ya Shafi kwamba kila kinywaji chenye kilevi ni najisi, makusudio ni kila kinywaji cha ulevi: Kilichokuwa na ladha kali inayopoteza akili na hawasemi kila kilicho majimaji: Wanaashiria kwamba kama inakuwa majimaji ya ulevi tu haitoshi kusema ni najisi, bali ni lazima kiwe kinywaji; ili kunywa si kuwa ni katika hali ya majimaji tu, na hayo yamefahamika kutokana na kauli yao kuwa kukamua kwa maana kukamua matunda kwa mfano yawe kama kinywaji, na kauli yao (mvinyo) na haya ni maji yaliyowekwa ndani yake yanayokuwa kama kinywaji chenye kilevi.
Asili ya kilevi ni haramu katika maandiko ya kisharia na ni kile kilichojulikana kuwa ni kinywaji, na ama ambacho hakinyweki, kama vile ilivyo alkoholi basi maandiko hayakijumuishia mpaka iwepo dalili ya wazi, na hasa kwa kuwa alkoholi haikuwepo wakati wa utungaji wa sharia, lakini ni haramu kuitumia kutokana na madhara yake.
Najisi ni hukumu ya kisharia na sio uhakika wa kikemikali, maana yake ni kwamba pombe ni najisi na hii najisi ni hukumu ya kisharia, na alkoholi ni sehemu inayosababisha kilevi katika pombe na huu ni uhakika wa kipimo cha kemikali, na si lazima kwa uhakika huu pekee kuwa ni najisi au haramu inapokuwa peke yake katika kimiminiko kingine kisichokuwa pombe; kwani najisi ya mchanganyiko hailazimishwi kwa unajisi wa viambato/vipengele vyake; hakika najisi walizoafikiana watu kuwa ni najisi; ni kama mkojo wa binadamu na kinyesi chake kilichochanganyikana na viambato/vipengele vya kemikali vinavyowezekana kuwa katika vitu vya twahara kama chakula na kinywaji; lakini unajisi unakuja kutokana na mchanganiko maalumu kwa kiasi maalumu. Na hali ya kuwa pombe inakuja inapokuwa maada ya kulewesha katika kitu cha asili, na bila ya hayo haiwezekani kutengenezeka ulevi hata ikibakia kwa muda mrefu kama vile Handhali, kulewesha ni kubadilika mada ya kilevi kuwa alkoholi na asidi ya kaboni, na kinywaji kinakuwa chenye uchachu na kwa hivyo itakuwa ulevi kwa sababu ya alkoholi hiyo, na alkoholi peke yake hailevi, lakini inadhuru; na inaponywewa peke yake, aliyeikunywa anaweza kulala fofofo au kupotea akili yake, na inapotaka kubadilishwa ili kuwa ulevi lazime ichanganywe na maji kwa kiasi cha mara tatu zaidi ya kiasi cha alkoholi, kisha itabadilika na itakuwa ulevi; basi kuchanganya na maji itaingia katika sifa ya kilevi, na msingi wa kutofautiana kwa mada zilizofanya kilevi ni kutofautiana kwa kiasi cha kilevi iliyopatwa kutoka kiasi cha maji na alkoholi wakati wa kuchanganyika kwa ziada au kupungua, kinywaji cha mtende kilichokuwa na kiasi cha asilimia 40 ya alkoholi na zaidi, na pombe zingine zilizokuwa na asilimia10 na Boza ya shairi ilikuwa na kiasi cha asilimia 5 na kadhalika, na alkoholi yenyewe ni mada yenye sumu na haiathiri kwa kutia katika kilevi ila kwa kuchanganyika na maji kwa kiasi maalumu.
Al-Imam An-Nawawi katika kitabu cha "Al-Minhaj" ameeleza juu ya najisi kwa kauli yake kuwa " Ni kila kinacholevya na kinakuwa na sifa ya majimaji" baadhi ya wafuasi wa Imamu Shafi walipinga juu ya kauli yake ya An-Nawawy, kuwa na sifa ya majimaji kwani kuna baadhi ya vinywaji vyenye sifa ya kulevya na majimaji lakini si najisi kama vile bangi iliyokuwa katika majimaji, na waliohojiwa kuhusu kauli ya An-Nawawi walifasiri kauli yake ni kuwa na ladha kali inayopoteza akili, na wapinzani na walioafikiana naye wanakubali kuwa sio kila majimaji ya kulevye ni najisi na sharti ya najisi ya majimaji ni kuwa na ladha kali inayopoteza akili. Lakini An-Nawawi katika mlango wa vinywaji katika kitabu hicho" Al-Minhaj" Alieleza kwa kauli yake: " Kila kinywaji kinacholevya kwa wingi wake basi uchache wake ni haramu na aliyekinywa lazima apate adhabu".
Kilichothibitika ni kwamba kitu kinachobadilika katika asili na sifa yake na kuwa kitu kingine hukumu yake itabadilika kufuatana na mabadiliko hayo, na najisi kwa mfano haibaki kuwa najisi inapotupwa katika maji mengi sana na rangi yake ikawa haikubadilisha rangi, ladha, au harufu ya maji hayo. na alkoholi inapochanganyika na manukato au dawa au vitu vya usafi, sifa yake ya pombe huondoka. Na mfano huu ni kama pombe iliyobadilika yenyewe na ikawa siki, basi siki hilo huwa linakuwa ni twahara katika sharia hata kama wanasayansi wa kikemia wakikuta baadhi ya alkoholi ndani yake, na hayo ni makubaliano ya Wanachuoni.
Na wafuasi wa Shafi wanaieleza najisi kama ni: Kitu kichafu kinachozuia usahihi wa Swala hali ya kuwa kitu hicho si chenye kuruhusiwa, na alkoholi si kitu kichafu kiasili, bali hutumika kwa shughuli za tiba kama maada ya kusafishia, na huondosha visivyo ondoshwa kwa maji pamoja na sabuni kutokana na uchafu na najisi, na pia inaingia katika kutengeneza baadhi ya manukato na michanganyiko ya dawa, kwani alkoholi ni mada iliyoandaliwa kwa ajili ya kusafishia na kwa ajili ya manukato, na kudai kwamba manukato na harufu yake vinatokana na najisi, ni jambo lenye tofuati na hisia na tabia, na manukato na uturi hayaitwi pombe katika istilahi ya kilugha au katika mila na desturi za jamii au hata katika utumiaji, na utumiaji wake kimakosa kwa kula na kunywa hakuondoi maana ya kuwa kwake manukato au uturi.
Na Imam Al-Izz Ibn Abdul-Salam Al-shafi katika kitabu chake "Kawa'd Al-Ahkam Fi Masalih Al-Anaam" amesema: "Asili ya twahara huambatana na sifa nzuri, na asili ya unajisi huambatana na sifa za uchafu. Kwa hivyo kama kinywaji kingekuwa pombe basi ingekuwa najisi kwa sababu ya kuwa kwake uchafu katika Sharia, na pia kama ingegeuka na kuwa siki basi ingekuwa twahara kwa sababu ya utwahara wa kisharia na kihisia, na pia maziwa ya wanyama wanaoliwa yanapobadilishwa sifa zake kwa kuchanganywa katika manukato yaliyokuwa twahara na pia makohozi, mate, machozi na jasho, na pia mnyama aliyetokana na najisi, na pia matunda yaliyomwagiliwa maji yaliyo najisika ni twahara, na ni halali kutokana na ubadilikaji wake wa sifa za utwahara, na pia mayai ya mnyama anayeliwa na miski. Na Wanachuoni wametofautiana katika majivu ya najisi; waliosema utwahara wake walitoa dalili ya ubadilikaji wa sifa zake za kiuchafu na kuwa katika sifa za kimanukato, na kama najisi zinatwaharika kwa ubadilikaji wa sifa zake pia vitu vingine vinavyopata najisi vinatwaharika kwa kuondoka najisi, na ngozi inapowambwa ni lazima kuondosha takataka zake na kubadilisha sifa yake. Na kwa hivyo basi baadhi ya Wanazuoni waliitaja rai ya kubadilika tu, na baadhi yao wakaitaja rai ya kutobadilika, na wapo waliozitaja rai zote mbili".
Na Imamu Al-Karafi anasema katika kitabu cha: [Az-Zakhira 1/188]:"Kanuni inabainisha yaliyotangulia, kwmba Mwenyezi Mungu alipohukumu juu ya unajisi wa miili maalumu, kwa sharti ya kuwa na sifa hasa hasa za uchafu, basi kama hakuna sifa hizo miili yote ni sawa, na tofauti zake ni kwa sifa za uchafu zilizoletwa, na zinapoondoshwa sifa hizi kwa sura kamili, hukumu ya unajisi wake huisha kwa makubaliano ya Wanachuoni.
Kama damu inavyobadilika kuwa manii na baadaye kuwa mwanadamu, na sifa hizo zinazobadilika zinapokuwa katika kitu kichafu zaidi ya kitu cha awali hukumu ya uchafu huthibitisha, kama damu itakuwa usaha, au damu ya hedhi, au damu ya kilichokufa. Na inapobadilika kuwa sifa zinazobadilika kwa tabia ya uchafu lakini ni mchache sana kuliko ya mwanzo, Je inasemwa kwamba sura hii ina inadhibitika tu kwa mujibu wa makubaliano ya Wanachuoni, na kwa hivyo basi hukumu ya asili pia huwa ni dhaifu, au huzingatiwa kuwa asili ya sababu sio ukamilifu wake, na kwa hivyo hukumu yake inalingana na hukumu ya Ijmaa (Makubaliano ya Wanazuoni wote?)
Sehemu hii kuna mitazamo mbalimbali kati ya Wanazuoni kwa maelezo yaliyotangulia; kwa hivyo Wanachuoni wanatofautisha kati ya ubadilikaji wa pombe na kuwa siki, na wametoa hukumu kuwa ni twahara, na kati ya ubadilikaji wa mifupa iliyokuwa najisi na ikawa jivu kwa sababu ya kuwa na baadhi ya uchafu na kutotumika, kinyume cha hali ya kwanza"[1]
Na kauli ya kwamba alkoholi si najisi na si pombe ni hukumu ya Fatwa iliyotolewa na Shekhe, Mwanachuoni mkubwa Bukhit Al-Moti'I katika gazeti la Al-Irshad, toleo la kwanza, mwaka wake wa kwanza, mwezi Shaabani, 1351 H, na Fatwa hii iliafikiana na Fatwa ya Idara ya Fatwa ya Misri; na ilitolewa Fatwa hiyo katika enzi za Shekhe Mohammad Khatir tarehe 27 mwezi wa mfungo pili (Dhul-Kaadah), mwaka 1391H, sawa na 13 januari mwaka 1972. Na Shekhe Mohammad Rashid Ridha Alishikamana na rai hii katika "Tafsir Al-Manar", na pia ni kauli ya wanazuoni Wengi wa wa kisasa na baadhi ya taasisi za kielimu ziliyothibitishwa kama vile katika mkusanyiko wa Fatwa za kisharia zilizotolewa na Kitengo cha Fatwa katika Wizara ya Mambo ya Waqfu nchini Kuwait, na kwa hivyo alkoholi sio pombe, si katika Madhehebu ya Shafi au Madhehebu nyingine, na ni halali kuitumia alkoholi katika manukato, uturi, mambo ya usafi, na madawa, na hakuna shaka kwa hilo katika Sharia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
[1] Al Dakhera: 1/188.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
