Hukumu ya mwanamke aliye katika eda kutoka ndani ya nyumba
Question
Ni ipi hukumu ya mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe kutoka nje ya nyumba ya ndoa?
Answer
Mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe ni lazima abaki katika nyumba ya ndoa kisharia, na kuacha kujipamba na kujitia manukato; hili ni kwa ajili ya kutimiza haki ya mume wake na kuomboleza kifo chake. Mwanamke huyo hauruhusiwi kutoka nje ya nyumba ya ndoa katika kipindi cha eda isipokuwa kwa sababu ya haja au dharura kama kununua chakula na vinywaji au kwenda kwa daktari pale anapokuwa mgonjwa.
Hata hivyo, inaruhusiwa kwa mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe kutoka nje kwa ajili ya kazi au kupata kipato, au kwa hofu ya kupoteza kazi yake inayomuingizia pato lake, kwa kuwa hakuna mwegine wa kumpa huduma hiyo na mfano wake, Kwa sharti arudi baadae kwenye nyumba ya ndoa kulala humo. Kama ambavyo, inafaa kuondoka katika nyumba ya ndoa kwa sababu ya kutokuwepo na usalama, au hofu kwa usalama wake na kwenda katka nyumba nyengine ambayo atamalizia muda wa eda yake kama ilivyo hali katika nyumba ya ndoa (nyumba ya mumewe).
Maelezo
Katika yaliyopitishwa kisharia ni wajibu kwa mwanamke ambaye amefiwa na mumewe kukaa eda[1] katika nyumba ya ndoa siku za eda yake, na kuacha mapambo, kujitia manukato, na dalili za kuonesha furaha katika masiku hayo ; kwa ajili ya kutekeleza haki ya mumewe na kuwa na huzuni kwa kutengana nae.
Eda ya mwanamke liyefiwa na mumewe hutofautiana kulingana na hali ya mwanamke huyo, kama ifuatavyo:
Iwapo mwanamke liyefiwa na mumewe alikuwa mjamzito, basi eda yake ni hadi ajifungue.{ Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa} [At-Talaq: 4].
Iwapo mwanammke aliyefiwa na mumewe si mja mzito, sawa iwe amekutana (ameingiliwa) na mumewe au hapana, eda yake ni miezi mine na siku kumi. Kwa kauli yake Mwenyezi Mungu {Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi.} [Al-Baqara: 234].
Na miezi ambayo mwanamke huhesabu katika eda yake ni miezi ya mwandamo (miezi ya mwezi wa Kiislamu); Na idadi ya siku za miezi ya mwandamo inaweza kutofautiana, mwezi wa mwandamo unaweza kuwa na siku ishirini na tisa, na unaweza pia kufikia siku thelathini. Na kauli yenye nguvu ni kwamba mwanamke aliyefiwa na mumewe ahesabu eda yake kwa kuzingatia idadi ya siku, nazo ni siku mia moja na thelathini, kwa tahadhari.”[2]
Ama kuhusu mahali panapomlazimu mwanamke kukaa katika kipindi cha eda: ni nyumba ya ndoa aliyokuwa akiishi wakati ulipotokea utengano kwa sababu ya kifo cha mumewe.
Imepokewa kutoka kwa Zaynab bint Kaab R.A kwamba Furayah bint Malik R.A alimweleza kuwa: “Alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akimuomba ruhusa ya kurejea kwa watu wake katika kabila la Banu Khudrah; kwa sababu mume wake alikuwa ametoka kwenda kuwatafuta watumwa wake waliotoroka. Alipowafikia katika eneo la al-Qadum -mahali palipo umbali wa maili sita kutoka Madina -walimuua. Akasema: Nilimuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) nirudi katika familia yangu, kwa kuwa mume wangu hakuacha nyumba anayoimiliki wala hakuniachia matumizi. Akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akaniambia: ‘Ndiyo.’Akasema: Nikageuka kuondoka. Nilipofika chumbani -au msikitini -Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), akaamuru niitiwe. Akaniambia: ‘Umesemaje?’ Akasema: Nikamsimulia tena mkasa wa mume wangu. Akasema: Mtume (S.A.W) akasema: ‘Kaa katika nyumba yako mpaka muda uliowekwa (wa eda) ukamilike.’ Akasema: Basi nikakaa humo nikahitimisha eda ya miezi minne na siku kumi. Akasema: Wakati wa ukhalifa wa Uthman R.A, aliniita akaniuliza kuhusu jambo hilo. Nikamweleza, naye akafuata hukumu hiyo na akaihukumu kwa mujibu wake.”[3]
Hivyo, hadithi hii inaonyesha kwamba ni wajibu kwa mwanamke kubakia katika nyumba ya ndoa mpaka amalize eda yake[4].
Ama kuhusu hukumu ya kwa mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe kutoka katika nyumba ya ndoa, hukumu yake inaelezwa kwa ufafanuzi ufuatao:
Iwapo atatoka nje mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe bila haja au dharura kitendo hiki hakifai kisharia.
Iwapo atatoka nje mwanamke aliyefiliwa na mumewe kwa haja au dharura kitendo hiki kinafaa kisharia; kama mfano kutoka kwa ajaili ya kununua chakula, vinywaji, au kwenda katafuta mahitaji ambayo ni lazima ayapate, katika hali ambayo hapana mtu mwengine wa kumsaidia jambo hilo, au kwenda kwenye matibabu anapougua na mfano wake.
Ikiwa kutoka nje mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe kwa ajili ya kazi au kupata kipato katika hali ambayo hakuna mwengine wa kuweza kumsimamia katika kupata mahitaji yake, katika hali hiyo inafaa kutoka nje, kwa shart kuwa arudi kwenye nyumba ya ndoa na kulala humo.
Iwapo kutoka nje kwa mwanamke aliyefiwa na mumewe ni kwa sababu ya kutokuwapo kwa usalama wa kukaa peke yake katika nyumba ya ndoa na kuhofia madhara juu ya nafsi yake, katika hali hiyo inafaa kuhamia mahali pengine atakapokamilisha eda yake, lakini asitoke humo kama hali ilivyokuwa katika nyumba ya ndoa.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe ni wajibu kwake kisharia kubaki katika nyumba ya ndoa, na kuacha kujipamba na kujitia manukato; hilo ni kwa kutimiza haki ya mume wake juu yake na kuonyesha huzuni kwa kuondokewa naye.
Hairuhusiwi kwa mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumuwe kutoka katika nyumba ya ndoa wakati wa eda isipokuwa kwa kutimiza haja au dharura, kama kununua chakula na kinywaji au kwenda kwa daktari endapo ataumwa.
3- Inajuzu kwa mwanamke aliye katika eda ya kufiwa na mumewe kutoka na kwenda kazini kwa ajili ya kujipatia riziki au kwa kuogopa kupoteza kazi anayojipatia kipato chake, ikiwa hakuna wa kumhudumia kwa matumizi na mfano wa hayo; lakini kwa sharti la kurejea baadaye katika nyumba ya ndoa na kulala humo.
4- Inaruhusiwa kwa mwanamke aliye katika eda kuhamia kutoka katika nyumba ya ndoa kwa sababu ya kutokuwepo kwa usalama na kuogopa madhara juu yake na kwenda nyumba nyingine atakayokamilisha humo muda wa eda yake, kama ilivyokuwa hali katika nyumba ya ndoa.
[1] Al-‘Iddah”: ni muda wa kipindi wa muda ambao mwanamke anasubiri na kukaa katika nyumba ya ndoa baada ya kutengana na mumewe kwa sababu ya talaka au kifo.
[2] “Badaai‘ as-Sanaa’i fi Tartib ash-Sharaa’i” cha Al-Kaasaani (3/ 196).
[3] Amepokea Imam Attirmidhy katika "Jami'I" (3/501)
[4] “Nihayat al-Muhtaj” cha Ar-Ramli (7/ 155), na “Sharh Muntaha al-Iradat” cha Al-Bahuti (3/ 204).
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
