Hukumu ya Mwanamke Muislamu Kuvaa M...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Mwanamke Muislamu Kuvaa Mavazi ya Rangi

Question

Je, inapaswa kwa mwanamke Muislamu kuvaa nguo za rangi za giza na kuepuka rangi ang’avu kama nyekundu, ya manjano na nguo zenye michoro ya maua?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Si sharti kwa nguo za mwanamke ziwe za rangi za giza, na hakuna pingamizi kwa mwanamke Muislamu kuvaa nguo za rangi zinazong’ara kama vile rangi za maua; nyekundu, samawati n.k., sharti zisiwe za kuchocheza fitina na kuvutia machoni. 

Kwa yaliyotajwa hapo juu, jibu la swali limebainika iwapo hali ni kama ilivyoelezwa.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas