Hukumu ya mwanamke kusoma Qur`ani Tukufu kwa mavazi ya kawaida ya nyumbani
Question
Ni ipi hukumu ya mwanamke kusoma Qur`ani Tukufu kwa mavazi ya kawaida ya nyumbani?
Answer
Ni bora kwa Muislamu akisoma Qur`ani awe amejisitiri uchi wake, awe anavaa mavazi mazuri, kwa mwanamke kusoma Qur`ani kwa mavazi ya kawaida ya nyumbani pasipo na kuvaa Hijabu ya kufunika kichwa chake kunakubalika kisharia, kwani kuvaa Hijabu si wajibu wakati wa kusoama Qur`ani kwa mwanamke, lakini akivaa Hijabu ya kufunika kichwa wakati wa kusoma Qur`ani huwa ni bora zaidi kulingana na kuwajibika na adabu za kusoma Qur`ani.