Hukumu ya Mwanamke Kumkataa mume am...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Mwanamke Kumkataa mume ambaye Familia yake Imemchagulia.

Question

Je, inajuzu kwangu kuolewa na mtu ninayempenda licha ya kutokubaliwa na familia yangu kwa sababu ana maradhi ya kisukari na wana shaka kuwa hataweza kupata watoto? Ikithibitika kuwa anaweza kupata watoto, je naweza kuipinga familia yangu na kuwakataa wale walionichaguliwa badala yake?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Mwanamke ana haki ya kisharia ya kumkataa mwanamume ambaye familia yake imemchagulia kuolewa ikiwa hajaridhika naye. Haya ni kwa sababu imepokelewa kutoka kwa Aisha – (R.A) – kwamba: “Akamjia msichana mmoja akasema: Baba yangu aliniozesha kwa mpwa wake ili nimpandishe hadhi yake, nami sijaridhika, akasema: “Kaa mpaka Mtume wa Mwenyezi Mungu – (S.A.W) – aje. Akaja Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) na akamwambia. Akamwita baba yake na kumwachia suala hilo. Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi naridhia aliyoyafanya baba yangu, lakini nilitaka kujua iwapo wanawake wana neno katika jambo hili?”

Vile vile mwanamke ana haki ya kufahamisha familia yake juu ya hamu yake ya kuolewa na yeyote anayemtaka. Mama, baba, na familia pia wana haki ya kupinga ndoa na mtu yeyote ampendaye ikiwa mtu unayempenda hakufai na inaweza kusababisha matatizo ya kiafya au kijamii kwa familia au kwako.

Suala la kupata watoto au kutozaa ni suala lako binafsi na si sababu ya msingi kwa familia kukataa ndoa na mgonjwa wa kisukari ilimradi anakufaa wewe na familia yako kwa ujumla.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas