Eda ya mwanamke mjamzito ambaye mume wake amefariki
Question
Je, kwa mke ambaye mume wake alifariki akiwa mjamzito vipi kuhusu eda yake?
Answer
Eda ya mwanamke mjamzito inaisha wakati wa kuzaa, ni sawa ilikuwa kwa kutengana (kutaliki) au kunatokana na kifo au vinginevyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:{Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa} [At-Talaaq:4) Aya hii kwa ujumla inahusu mwanamke ambaye mume wake amefariki na mengine.
Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.