Kufanya kazi katika biashara ya vipodozi
Question
Ni ipi hukumu ya kufanya kazi katika biashara ya vipodozi?
Answer
Asili ya hukumu za kazi zote ni ruhusa isipokuwa zile zinazokatazwa kwa matini kutoka katika Qur'ani au Sunna za Mtume (S.A.W.), na ikiwa mapambo ya mwanamke kwa mumewe ni miongoni mwa mambo yaliyoruhusiwa na Mwenyezi Mungu, na ikiwa mapambo haya yanategemea kutumia baadhi ya vipodozi vinavyozalishwa na makampuni na viwanda vinavyoshughulikia biashara hiyo, basi hatuna pingamizi lolote kisharia kutendeana na shughuli hizi za kiviwanda na za kibiashara katika nyanja husika endapo mapambo haya hayana madhara yoyote kwa afya ya binadamu.