Kufanya kazi za vifaa vya urembo.
Question
Ipi hukumu ya kufanya kazi kwenye uzalishaji vifaa vya urembo?
Answer
Asili ya vitu ni halali isipokuwa ikiwa limekuja tamko kutoka ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu au katika Sunna ya Mtume wake S.A.W la kuharamisha, ikiwa kujipamba kwa mwanamke ni katika mambo halali ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amehalalisha, na pambo hili wakati mwingine linamtaka mwanamke kuhitaji baadhi ya vifaa vya urembo ambavyo huzalishwa na baadhi ya viwanda na mashirika ya urembo, hivyo sisi hatuoni kizuizi cha Kisharia kinachozuia kufanyika kazi za uzalishaji wa viwanda na kibiashara madamu vifaa hivi havina athari yeyote inayoleta madhara kwa afya ya mwanadamu.