Kufanya kazi katika Benki
Question
Ni ipi hukumu ya kufanya kazi katika Benki za uwekezaji? Kwa kuzingatia kwamba aina ya kazi yangu inahusisha kusajili maombi ya wateja na idara nyingine za Benki.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Tangu kuibuka kwa mabenki na vitabu vya akiba katika zama za sasa, wanasheria wametofautiana katika tafsiri yao ya suala hilo. Hii inatokana na tofauti kati ya Wanachuoni wa sharia na uchumi kuhusu kama uhusiano kati ya wateja na Benki ni uhusiano wa mkopo, kama wanasheria walivyobishana, au uhusiano wa uwekezaji, kama wachumi walivyokubaliana. Tofauti hii ya tafsiri husababisha tofauti katika uainishaji wa tukio. Wale wanaoutaja kuwa ni mkopo wanaona kuwa ni mkataba wa mkopo unaoleta manufaa, na hukmu, kwa msingi huu, ni kwamba ni riba iliyoharamishwa. Kisha fatwa zikatofautiana. Baadhi yao walilichukulia hili kuwa ni la lazima ambalo Muislamu anaweza kujihusisha nalo anapolazimishwa kufanya hivyo, kwa kuzingatia kanuni kwamba “Dharura zinaruhusu yale yaliyoharamishwa.” Ikichukua kutoka katika jumla ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [Al-Baqarah: 173] Baadhi yao waliona kwamba si jambo la dharura; dharura imefafanuliwa katika sharia ya Kiislamu kuwa ni jambo ambalo mtu asipolishughulikia litapelekea kifo au kukaribia kufa. Baadhi ya wanavyuoni hawa wameiona kuwa inaruhusiwa kwa kuzingatia kanuni kwamba haja inachukuliwa kuwa ni hitaji la jumla au maalumu. Wale ambao wamepita njia ya uwekezaji katika suala hili wameiona kama aina ya Mudharaba (Mudharabah ni neno la Kiarabu ambalo linamaanisha mkataba wa kifedha kati ya mwekezaji (mudharib) na mjasiriamali (sahibul-maal) ambapo mudharib anahusika na kufanya kazi ya kibiashara na sahibul-maal anatoa mtaji.) ya kifisadi ambayo unaweza kurekebishwa kwa kukodisha. Wengine wamesema kwamba ni muamala mpya na mkataba mpya ambao haukutajwa katika sheria ya kurithiwa ya Kiislamu, na wamefanya juhudi mpya katika suala hili, kama vile wanasheria wa Samarkand walivyofanya juhudi mpya katika mkataba wa uuzaji wa Al-Wafa )ni aina ya uuzaji ambao mnunuzi anaweza kurudisha bidhaa na kupewa pesa yake), wakizingatia kuwa ni mkataba mpya. Sheikh Al-Islam Abu Al-Su'ud alifanya juhudi mpya katika mkataba wa Al-Mu'amalah, akihukumu kuwa inajuzu, sawa na vile wanavyuoni wa mwanzo walivyoihukumu kuwa inajuzu. Hii ni kwa sababu ya kuzingatia masilahi ya watu, hitaji lake kubwa, uthabiti wa hali ya soko, utegemezi wa maisha ya watu juu yake, na kufaa kwake kwa mahitaji ya enzi hiyo, pamoja na maendeleo ya usafirishaji, mawasiliano, teknolojia ya kisasa, kuongezeka kwa idadi ya watu na kudhoofika kwa uhusiano wa kijamii, maendeleo ya sayansi ya uhasibu na uwekaji hesabu, uhuru wa watu waliopewa kipaumbele ambao ni tofauti na watu wa kawaida na kadhalika.
Jambo la msingi ni kwamba kumezuka kutofautiana kuhusu suala la muamala na Benki, uainishaji wake, hukumu zake, na utoaji wa fatwa zinazoihusu. Miongoni mwa kanuni zilizowekwa na Sharia ni:
Kwanza: Yale tu waliyokubaliana (Wanazuoni) ndio yanaweza kukemewa, na wasioyokubaliana (wanazuoni) hayakemewi.
Pili: Kuepuka migogoro kunapendekezwa.
Tatu: Atakayefikwa na jambo lenye tofauti ndani yake na amfuate aliyeliruhusu.
Inajulikana katika dini kwamba riba ni haramu, kwani uharamu wake umeelezwa wazi katika Qur’ani Tukufu na Sunna, na Umma umeafikiana kwa kauli moja juu ya uharamu wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu} [Al-Baqarah: 275] Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kula riba, mwenye kuilipa, mashahidi wake wawili, na mwenye kuiandika. Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim. Hata hivyo, kulizuka kutofautiana kuhusu iwapo tabia hii katika Benki ni riba, ambayo imeharamishwa na sharia ya Kiislamu, au ikiwa ni aina ya mikataba batili ambayo pia imekatazwa na sharia ya Kiislamu, au iwapo ni mkataba ulioanzishwa hivi karibuni ambao hukumu yake inaruhusiwa ikiwa inakidhi maslahi ya pande zinazohusika na haijumuishi chochote kilichokatazwa na sharia ya Kiislamu.
Kwa kuzingatia hayo hapo juu, ni lazima kila Muislamu atambue kwamba riba imeharamishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwamba kuna maafikiano juu ya kuharamishwa kwake. Ni lazima pia atambue kwamba shughuli za Benki zimekuwa chini ya tafsiri tofauti, uainishaji, maamuzi, na Fatwa. Ni lazima pia atambue kwamba kuepuka mbali na mambo waliotofautiana (Wanazuoni) kunapendekezwa. Hata hivyo, anaweza kuwafuata wale wanaoruhusu, na hakuna katazo kwake katika kufanya muamala na Benki kwa namna yeyote ile—kuchukua, katika, kufanya kazi, muamala n.k.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
