Kufanyia ukatili maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufanyia ukatili maiti

Question

Je, kufanyia ukatili maiti inaruhusiwa?

Answer

Haijuzu wala haikubaliki kufainyia ukatili maiti, kwani sharia ya Kiislamu ilihimiza vitendo vizuri na tabia njema katika hali zote hata katika vita, kwa kudhihirisha ukweli wa dini ya kiislamu ambayo huheshmu ubinadamu wa mwanadamu na nafasi yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} [Al-Israa: 70], naye Mtume (S.A.W.) amewakataza Maswahaba zake kufanya ukatili kwa maiti za maadui wao wakati wa vita akisema: "Msifanye ukatili kwa maiti za wanadamu, wala wanyama, msifanye hiyana, msivuke kiwango" (Imesimuliwa na Al-Bayhaqiy), Wataalamu wamesema kuwa kauli yake Mtume (S.A.W.) "Msifanye ukatili kwa maiti za wanadamu, wala wanyama", imeeleza kuwa katazo hilo ni la kijumla na kwamba kufanya ukatili kwa maiti ya mwanadamu au wanyama ni jambo lililokataliwa katika hali zote, pia zipo Hadithi nyingi za kukataza tendo hilo baya.

Share this:

Related Fatwas