Kuwafanyia watu uadui.
Question
Nini hukumu ya mwenye kuwafanyia watu uadui na kuwavunjia heshima zao?
Answer
Kutoka kwa Said Ibn Zaidi R.A kutoka kwa Mtume S.A.W amesema:
“Hakika miongoni mwa riba mbaya zaidi ni kushambulia heshima ya Muislamu bila ya haki”. Imepokewa na Imamu Ahmad na Abu Daud.
Katika Hadithi hii kuna onyo kubwa mno kutoka kwa Mtume S.A.W la kushambulia heshima ya Muislamu, na kueleza kufanya hivyo ni zaidi ya dhambi ya riba, hii inapelekea kuwa ni uhalifu mkubwa zaidi na katika dhambi mbaya sana, ambapo kushambulia heshima za watu ni kosa dhambi kubwa kwa kufungamana kwake na haki za waja, hivyo mtendaji wake amestahiki kuadhibiwa adhabu kali.