Kukusanya Swala.
Question
Ni ipi hukumu ya kukusanya Swala kwa sababu ya kunyesha mvua?
Answer
Kukusanya Swala – Swala ya Adhuhuri na Swala ya Alasir, Swala ya Magharibi na Swala ya Isha – ndani ya wakati wa Swala ya kwanza kati ya kila Swala mbili kwa sababu ya mvua kubwa bila ya kupunguza Swala, ni jambo linalofaa Kisharia, ili kuondoa uzito na ugumu, kwa sababu asili ni kuswali ndani ya wakati wake bila ya kuchelewa wala kutanguliza, na kukusanya kati ya Swala kunakuwa kwa kuwepo dharura, na mvua ni katika udhuru ambao unaruhusiwa kukusanya kati ya Swala mbili kwa sababu ya hali hiyo ya mvua, pamoja na kuchunga masharti ambayo yameelezwa na Wanachuoni kwenye hilo kama vile uwepo wa mvua kubwa mwanzoni mwa wakati wa Swala mbili na kuendelea mvua hiyo mpaka wakati wa Swala ya pili, na hiyo mvua iwe ya kulowesha nguo, kwa maana inapelekea uzito kwenda Msikitini kwa kuwepo kwake, na kukusanya huko kuwe ndani ya wakati wa Swala ya kwanza kati ya Swala hizo mbili uwe ukusanyaji wa kutanguliza na si wa kuchelewesha, na kuleta nia ya kukusanya wakati wa Swala ya kwanza na wakati wa kuanza Swala ya pili, na iwe Swala ya jamaa Msikitini, na zifuatane wala kusipite muda mrefu kati ya Swala hizo mbili.