Kuacha Swala

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuacha Swala

Question

Nini hukumu ya aachaye kuswali?

Answer

Swala ni nguzo ya dini, nayo ni moja ya nguzo za Uislamu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alituamrisha kushika kwa Swala. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na shikeni Swala, na toeni Zaka} [Al-Baqara: 43]. Swala ina mazingatio malumu katika Uislamu, hivyo nguzo, nyakati, mwanzo na mwisho zimeainishwa kwa ajili yake, na haijuzu kuichelewesha zaidi ya wakati wake isipokuwa kwa udhuru wa kisheria, na aachaye Swala kwa uvivu inatubidi sisi  kuendelea kumnasihi na kumtia moyo kwa hekima na mawaidha mema kuihifadhi Swala. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema} [Al-Nahl: 125], Pamoja na subira kwa hilo hata jambo hilo likichukua muda mrefu; Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: {Na waamrishe watu wako kuswali, na uendelee mwenyewe kwa hayo} [Taha: 132], na kumuombea dua kwa uwongofu na Mwenyezi Mungu afungue kifua chake ili kumtii; Mtume (S.A.W) akasema: “Dua ya mtu huitikiwa kwa ndugu yake kwa ghaibu, kichwani mwake kuna Malaika anayesema amina kwa dua yake kila anapoomba kwa heri, akasema: Amina, nawe unayo heri kama hiyo.” Mtume (S.A.W) amesema: dua inayoitikwa kwa haraka ni dua ya mtu asiyekuwepo kwa mtu mwengine asiyekuwepo.” Kwa maana mtu yule anafanya dhambi na anahitaji mtu mwingine anayemsaidia ili kujiepusha mbali na dhambi yake hii, na siye mtu anayemfanya apoteze tumaini la kutubu kutoka kwake, akifanya hivyo atamsaidia kusisitiza juu ya dhambi hiyo kama shetani.

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas