Kuchelewesha Swala.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchelewesha Swala.

Question

Ipi hukumu ya kuchelewesha Swala ya Isha mpaka usiku wa manane.

Answer

Yaliyopokewa kwenye Hadithi zilizothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W ni ubora wa kuchelewa Swala ya Isha kutoka mwanzo wa wakati wake mpaka wakati wa theluthi ya usiku au nusu yake, miongoni mwa Hadithi hizo ni pamoja na iliyopokewa na Imamu Tirmidhy kutoka kwa Zaidi Ibn Khalid Al-Jahny kuwa Mtume S.A.W amesema:

 “Lau nisingewaonea huruma Umma wangu basi ningewaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa Swala, na ningewaamrisha kuchelewesha Swala ya Isha mpaka muda wa theluthi ya usiku”.

Haya yanakuwa kwa yule mwenye kujua yeye mwenyewe ikiwa ataichelewesha hatozidiwa na usingizi wala uvivu, pamoja na kuwa anaiswali nyumbani kwake, kwa kuchunga nyakati za adhana na kukimiwa Misikitini, hivyo ni lazima aiwahishe na kuiswali mwanzoni mwa wakati wake. 

Share this:

Related Fatwas