Hukumu ya kuchelewesha sala
Question
Ni nini hukumu ya kuchelewesha sala kwa kauisali pamoja na wengine?
Answer
Kuisubiri sala ya pamoja au kusuburi watu wahudhurie ni bora kuliko kusali mwanzo wa wakati wake peke yako, kwa iliyosimuliwa na Imamu wawili Bukhary na Muslim katika “Sahihi” kutoka kwa Mohammed bin Amr bin Al-Hassan bin Ali bin Abi Talib (R.A.) kuwa alisema: “Tulimwuliza Jaabir bin Abdulaah (R.A.) kuhusu sala ya Mtume (S.A.W.) akasema: alikuwa anasali Adhuhuri wakati wa jua kali, Alasiri wakati ambapo jua bado lipo, Maghrib katika wakati wake, Isha wanapokusanyika umati wa watu anaiharakisha na wakiwa wachache anaichelewesha, na Alfajiri kabla ya jua halijachomoka”.
Al-Hafidh Al-Qistalany alisema katika kitabu cha “Irshadul-Sary” (1/502): “hadithi hii ina ishara na dalili ya kwamba kuichelewesha sala kwa ajili ya kuisali pampja na wengine ni bora zaidi kuliko kuisali peke yako mwanzoni mwa wakati wake, bali ina dalili ya kuwa kuichelewesha sala ya pampja kwa ajili ya kuwa na watu wengi zaidi ni bora” imeisha.
Hata hivyo, inapaswa kuwajibika kwa iliyopitisha na mamlaka husika kuhusu muda wa sala misikitini na kwa taratibu za namna ya kusimamisha sala kwa ajili ya kuhifadhi utukufu wa ibada na kuzuia mizozo na mifarakano.