Hukumu ya kuchanganyika.

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuchanganyika.

Question

Je kuchanganyika wanawake na wanaume ni haramu moja kwa moja Kisharia na inapaswa kutenganishwa kati yao sehemu zote?

Answer

Kuchanganyika kati ya wanawake na wanaume Kisharia haikatazwi katika mipaka yake na wigo wake uliosalama kwa mujibu wa mafundisho ya Sharia ya Kiislamu, kama vile inavyofanyika mara nyingi kuchanganyika kati ya wanaume na wanawake katika maeneo ya elimu kama shule Vyuo kwenye usafiri wa umma maeneo ya kazi na maeneo mengine ya harakati za maisha ya watu na masilahi yao, kwa vile mwanamke na mwanamme kila mmoja analinda na kuchunga adabu za Uislamu kama vile mwanamke kufanya heshima katika mavazi yake ulimi wake kuinamisha macho yake katika yale yaliyokatazwa na Sharia na kutokaa kikao cha siri kati yake na mwanamme na kuibua shaka, vile vile mwanamme inapaswa kwake kuinamisha macho na kulinda yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, haya yote yakifikiwa basi hakuna kizuizi cha Kisharia cha kutochanganyika wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu Anasema: {Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za wanayo yafanya} An-Nuur:  30.

Ama ikiwa mwanamme na mwanamke hawakutekeleza adabu hizi za Sharia ya Kiislamu na mafundisho yake, na kuchanganyika huko kukawa ni sababu ya fitina na kupelekea kutendeka maasi na mambo yaliyoharamu basi kutakuwa ni harama Kisharia.

Share this:

Related Fatwas