Hukumu ya Mkubwa Kunyonya

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Mkubwa Kunyonya

Question

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa nyumbani kwake Maswahaba zake na wale wenye kumfuata kwa uzuri na kwa wema.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa nyumbani kwake Maswahaba zake na wale wenye kumfuata kwa uzuri na kwa wema.

Baada ya Utangulizi:

Huu ni utafiti katika hukumu ya mtu mkubwa kunyonya na kubainisha madhehebu ya Wanachuoni katika hilo.

Mlango wa Hadithi:

Amepokea Imamu Muslimu katika sahihi yake kutoka kwa Mama wa Waumini Bi Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake, amesema:

 “Siku moja Sahla bint Suhail alikuja kwa Mtume S.A.W na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi naona katika sura ya Abi Hudhaifa kuingia kwa Salimi - Naye ni kijana wake wa kazi - Mtume S.A.W akasema: Mnyonyeshe, Sahla akasema: Ni vipi nimnyonyeshe hali ya kuwa ni mtu mkubwa, Mtume S.A.W akatabasamu na akasema: Nafahamu ni mtu mkubwa”.

Katika tamko lingine: Kutoka kwa Mama wa Waumini Bi Aisha R.A amesema kuwa Salimu mtumishi wa Abu Hudhaifa alikuwa na Abi Hudhaifa pamoja na familia yake nyumbani kwao, ndipo akaja – kwa maana Sahla - kwa Mtume S.A.W akasema: Hakika Salimu amefikia yanayofikiwa na wanaume na utambuzi wa wanayotambua wanaume, anaingia kwetu na ninadhani katika nafsi ya Abi Hudhaifa kuna kitu, Mtume S.A.W akamwambia: Mnyonyeshe utakuwa haramu kwake na kuondoka ambayo yapo kwa Abi Hudhaifa, akarudi na akasema: Nimeshamnyonyesha na kuondoka yaliyo ndani ya nafsi ya Abi Hudhaifa ([1]).

Kauli za Wanachuoni:

Ibn Hazmi amesema kuhusu Hadithi hii ya Sahla – baada ya kutaja kwake njia tofauti – Hadithi hii imekuja ikiwa na wapokezi wengi imepokelewa na wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kama ilivyoelezwa, na Sahla bint Suheil ni katika wahamiaji wa Madina kutoka Makka na Zainabu Ibn Ummi Salama, na imepokelewa na Taabiin Kassim Ibn Muhammad na Arwat Ibn Zubeir, na Hamid Ibn Nafii, na imepokelewa kutoka kwa hawa na Zahry, na Ibn Abi Malika, na Abdulrahman Ibn Kassim, na Yahya Ibn Saidi Al-Answary, na Rabiia, na imepokelewa kutoka kwa hawa na Ayubu Sakhtiyany, na Sufyan At-Thawry, na Sufyan Ibn Ayiina, na Shuuba, na Maliki, na Ibn Jariir, na Shuaibu Ibn Abi Hamza, na Yunus Ibn Yaziid, Jafari Ibn Rabia, Sulaiman Ibn Bilal, Muammar na wengine, na imepokelewa kutoka kwa hawa na Wanachuoni wengi, imepokelewa na wengi ngumu kutenganisha katika usahihi wake ([2]).

Na Shaukany amesema: “Hadithi hii imepokelewa na Maswahaba Mama wa Waumini, na Sahla bint Suhail ni katika wahamiaji Madina, na Zainabu bint Ummu Salama naye ni binti wa kambo wa Mtume S.A.W, na imepokelewa na Taabien Kassim Ibn Muhammad, na Urwat Ibn Zubeir, Hamidu Ibn Nafii, na imepokelewa kutoka kwa hawa na Zahry, na Ibn Malika, Abdilrahman, Yahya Ibn Saidi Al-Answary na Rabia, kisha ikapokelewa kutoka kwa hawa na Ayubu Sakhtiyany, na Sufyani Thaury, Sufyani Ayiina, Shuubah, Maliki, Ibn Jariih, Shuaibu, Yunus, Jaafar Ibn Rabiah, Maamar, Sulaiman Ibn Bilal na wengineo, na hawa ndio Maimamu wa Hadithi na marejeo katika zama zao, kisha wakapokea kutoka kwao idadi kubwa, baadhi ya Wasomi wamesema: “Wapokezi hawa sita wamefikia kiwango cha wapokezi wengi” ([3]).

Madhehebu ya Wanachuoni katika kumnyonyesha mtu mkubwa:

Madhehebu ya Jamhuri ya (Madhehebu Manne).

Abu Hanifa:

Abu Hanifa amesema kunyonyesha kunakopelekea haramu ni kunyonya wakati wa utoto, ama yanayokuwa katika hali ya ukubwa si haramu kwa kauli za Wanachuoni na Maswahaba wa Mtume Radhi za Mola ziwe kwao, isipokuwa Hadithi iliyopokelewa na Mama wa Waumini Bi Aisha R.A kunapelekea uharamu kunyonya katika utoto na ukubwa pia.

Kisha wakatofautiana katika mpaka kati ya mtoto na mkubwa, Imamu Abu Hanifa akasema: Muda wa mwisho wa kunyonya kunakopelekea uharamu ni miezi thelathini, hakuna uharamu baada ya hapo ni sawa sawa ameachichwa kunyonya au hajaachichwa.

Wakati ambapo Wanachuoni wawili Abu Yusufu na Muhammad wanaona kuwa: Muda ambao unathibiti ndani yake uharamu ni miaka miwili, wala hakuna haramu baada ya hapo ni sawa sawa ameachishwa kunyonya au hajaachishwa.

Na Zafari akasema: Hali tatu – Kwa maana: Miaka mitatu ([4]).

Imamu Maliki: Imamu Maliki ameeleza kuwa sharti la uharamu wa kunyonya ni miaka miwili au zaidi kidogo kama vile mwezi mmoja au miezi miwili na ikasemwa miezi mitatu, ama kinachofika mpaka ndani ya utumbo baada ya miaka miwili mara nyingi hakipelekei kwenye uharamu ([5]).

Imamu Shaafi: Imamu Shaafi amesema, sharti la uharamu kwa kunyonya ni kabla ya kubaleghe kwa miaka miwili, ikiwa atafikia umri wa baleghe hakuna uharamu wa kunyonya ([6]).

Imamu Hambali: Imamu Hambali amesema, sharti la uharamu kwa kunyonya ni mtoto kunyonya katika umri wa miaka mwili, ikiwa atanyonya baada ya miaka mwili kwa muda mdogo tu uharamu hauthibiti ([7]).

Ufupisho wa maelezo ya Madhehebu Manne:

Kunyonya kunakothibiti uharamu ni kunyonya wakati wa utoto na si ukubwani, na muda unaotenganisha kati ya utoto na ukubwa unatafauti.

Kwa upande wa Imamu Shafi, Imamu Hambali na Maimamu wawili katika Maimamu wa madhehebu ya Imamu Hambali: Ni kuwa mpaka wa mtoto mdogo ni miaka miwili.

Ama Imamu Maliki kaongezeka kidogo zaidi ya miaka miwili kunaingia katika uharamu wa kunyonya, na mpaka wake ni mwezi mmoja au miwili kwa kauli yenye kukubalika kwao.

Wakati ambapo Imamu Abu Hanifa anasema mpaka wa mtoto mdogo ni umri wa miezi thelathini, kwa maana ya miaka miwili na nusu, na Zafar Ibn Al-Hadhiil – ni katika madhehebu ya Abu Hanifa – amesema: Mpaka wa mtoto mdogo ni miaka mitatu.

Na kauli ya Jamhuri – ni kuwa kunyonya ambako kunathibiti uharamu wake ni unyonyaji katika umri wa mtoto mdogo bila ya mkubwa – ni kauli ya Wanachuoni wengi, imepokelewa mfano wa hilo kwa Umar, Ally, Ibn Umar, Ibn Masoud, Ibn Abbas, Abi Huraira na wake za Mtume S.A.W ukiondoa Bi Aisha, na matazamo huo pia amekubaliana nao Imamu Shafi, Ibn Shubruma, Al-Auzai, Is-haka na Abu Thauri ([8]).

Dalili za Jamhuri:

 Jamhuri ya Wanachuoni wamechukuwa dalili walipoelezea kuwa – kunyonya kunakoingia uharamu ni kule kunyonya wakati wa utoto na sio ukubwani kwa dalili mbalimbali:

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha} Al-Baqarah: 233. Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya kukamilika kunyonyesha kukawa kipindi cha miaka miwili, na kufahamika kuwa hukumu baada ya muda huo ni tofauti.

Na Aya hii Tukufu imeelezea pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

{Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thelathini} Al-Ahqaaf: 15. Muda mdogo wa ujauzito na ukamilifu wa muda wa kunyonyesha ([9]).

Yaliyopokelewa kutoka kwa Bi Aisha R.A kuwa Mtume S.A.W aliingia kwake na kumkuta mtu kana kwamba sura yake ilibadilika, kana kwamba alichukia hilo, Bi Aisha akasema: Huyu ni ndugu yangu, akasema: “Angalieni ndugu zenu kwani kunyonya ni kunakopelekea kukata njaa” Mtume S.A.W akaashiria kuwa kunyonya katika utoto ndio unaoleta uharamu, kwa sababu ni kipindi cha kuhitaji lishe na maziwa, nayo ndio yanayoondoa njaa, ama njaa ya ukubwani haiondoki kwa kunyonya ([10]).

Kutoka kwa Ummu Salama amesema: Mtume S.A.W amesema: “Hakuna uharamu utokanao na kunyonya isipokuwa utumbo unapofunguka kwa maziwa ya chuchu na ikawa kabla ya kuachishwa kunyonya”, kunyonya wakati wa utoto ndiko ambako kunafungua utumbo na wala si kunyonya ukubwani, kwa sababu utumbo wa mtoto mdogo unakuwa umebana haufunguki isipokuwa kwa maziwa kwa kuwa maziwa ndio lishe laini kabisa, ama utumbo wa mtu mkubwa kufunguka kwake hakuhitaji kufunguliwa na maziwa ya kunyonya ([11]).

Hadithi: “Hakuna kunyonyesha isipokuwa ndani ya kipindi cha miaka miwili” ([12]).

Yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W kuwa amesema: “Kunyonyesha kunaotesha nyama na kueneza mifupa”, huku ni kunyonyesha wakati wa utoto na sio ukubwani, kwa sababu kunyonya kwake hakuoteshi nyama wala mifupa ([13]).

Na imepokelewa Hadithi hii kutoka kwa Abdillah Ibn Masoud kuwa, mtu mmoja kutoka shamba mke wake alijifungua mtoto wa kiume kisha mtoto yule alifariki matiti ya mama yakajaa maziwa yule mtu akawa Ananyonya na kuvyonza chuchu kisha maziwa yakaingia kwenye kolomeo lake, akamuuliza Aba Musa Al-Ash’ary R.A na akasema: Ni haramu kwako huyo mwanamke, kisha akeanda kwa Abdillah Ibn Masoud R.A akamuuliza na akasema: Je umemuuliza yeyote? Akasema, ndio, kwani nilimuuliza Aba Musa Al-Ash’ary R.A akasema: Ni haramu kwako, Ibn Masoud akaenda kwa Aba Musa Al-Ash’ary R.A na kumuambia: Hivi umefahamu kuwa kunako haramisha kutokana na kunyonya ni unyonyaji unaotesha nyama, Abu Musa akasema: Msiniulize kitu madamu habari hii ipo kwenu” ([14]).

Hadithi imepokewa kutoka kwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kunyonyesha baada ya kuacha kunyonya” ([15]).

Imepokelea kutoka kwa Abdillah Ibn Omar kuwa mtu mmoja alikuja kwa Omar R.A akasema: Nilikuwa na mtoto mdogo wa kike basi mke wangu akaenda kwa mjakazi na akamnyonyesha, kisha nikaingia akasema: Nimemnyonyesha, Omar R.A akasema: Ukweli huyo ni mjakazi wako lakini kunyonya ni wakati wa utoto ([16]).

Madhehebu ya Dhwahiriyah:

Madhehebu ya Dhwahiria wamesema kuwa kunyonya ukubwani na utotoni kote kunapelekea uharamu wa kunyonya ([17]), nayo ni kauli ya Bi Aisha Mola awe radhi naye, imepokelea na Atwaai, Allaithy na Daud ([18]). Na Ibn Hazmi akainasibisha kwa Imamu Ally ([19]), nao ni unasibishaji usio sahihi kwa maelezo yafuatayo:

Na wakachukuwa dalili nyingi juu ya hilo – kama alivyozitaja Ibn Hazmi ndani ya kitabu cha Al-Muhilly ([20]):

Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abi Musa – na kisa chaka kilichopita kimetajwa na Abdillah Ibn Masoud R.A pamoja na kuwa amefuta yale aliyoyatolea Fatwa. Na haya hayahitaji mjadala ya Abi Musa kufuta Fatwa aliyoitoa.

Maelezo yaliyopokelewa kuwa Salimu Ibn Abi Al-Jaad – Mtumishi wa Al-Ashjaii – alimpa habari kwamba baba yake alimueleza kuwa alimuuliza Ally Ibn Abi Twalib akasema: Mimi nilitaka kumuoa mwanamke niliwahi kunywa maziwa yake nikiwa mkubwa kwa ajili ya tiba. Ally akasema: Usimuoe na kumkataza.

Nikasema maelezo haya ni dhaifu yamepokelewa na Abdulrazik katika kitabu chake ([21]), na AbdulKareem ni mtoto wa Abi Al-Makhaarik. Nayo ni maelezo dhaifu kama alivyoeleza Al-Hafidh katika kitabu cha Taqriib ([22]), kama vile Hadithi ya Salimu mfanya kazi wa Ibn Abi Al-Jaad kutoka kwa Ally R.A ni Hadithi amekosekana mpokezi mmoja, kama ilivyotajwa na Abu Hatim kutoka kwa Abi Zara ([23]).

Kunasibishwa na Imamu Ally si sahihi kama alivyosema Ibn Abdulbarr ([24]) na Abu Zaraa Al-Iraqy ([25]), kama vile Abdulrazaq amepokea ndani ya kitabu chake kinyume na madhehebu haya kutoka kwa Imamu Ally, ambapo amesema kutoka kwa Ally pia, alikuwa anasema: Mke wake alimnywesha maziwa ya mjakazi wake, au mjakazi wake maziwa ya mke wake, ili kumuharamisha naye, basi hakuna uharamu katika hilo ([26]).

Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Shihab kuwa aliulizwa kuhusu kunyonya mkubwa akasema: Amenieleza Urwatu Ibn Zubeir Hadithi Mtume S.A.W alimuamuru Sahla bint Suhail kumnyonyesha Salimu mfanya kazi wa Abi Hudhaifa minyonyesho mitano – akiwa ni mkubwa – na akamnyonyesha,  akawa anamuona ni mtoto wake, Ur’watu amesema: Akafanya hivyo Bi Aisha kwa mtu aliyependa aingie nyumbani kwake kwa upande wa wanaume, hivyo alikuwa anamuamrisha ndugu yake Ummu Kulthuum na mabinti wa kaka yake kumnyonyesha mtu anayetaka aingie nyumbani kwake kwa upande wa wanaume.

Imepokewa kutoka kwa Ibn Jariih amesema: Nimemsikia Atwaa Ibn Abi Riyaah aliulizwa na mtu akasema: Mwanamke alininywesha maziwa yake nikiwa mkubwa je naweza kumuoa? Atwaa akasema: Hapana, Ibn Jariir amesema nikamuuliza: Huo ni mtazamo wako? Akasema: Ndio, kwani Bi Aisha alikuwa anaamrisha hivyo watoto wa kike wa ndugu yake.

Dalili hizi mbili hazifai kuthibitisha madai, ambapo zote mbili hazizingatiwi kuwa kielelezo cha mtazamo na rai ya watu wake katika masuala haya.

Wana dalili mbili zingine zitaelezwa na kujadiliwa katika majibu yao kuhusu dalili za Jamhuri, nazo ni:

Hadithi ya Sahla na Salimu mfanya kazi wa Abi Hudhaifa.

Kauli ya Mola Mtukufu: {Na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya} An-Nisaa: 23.

Wakajibu baadhi ya dalili za Jamhuri kama ifuatavyo:

Hadithi ya Mama wa Waumini Ummu Salama Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwake amesema: Mtume S.A.W amesema: “Si haramu kutokana na kunyonya isipokuwa kwa kufungua utumbo kwa maziwa, na ikawa kabla ya kuachishwa kunyonya”. Wakasema: Hadithi hii imekatika wapokezi, kwa sababu Fatuma bint Al-Mundhir hakusikia kutoka kwa Ummu Salama Mama wa Waumini, kwa sababu alikuwa mtu mzima zaidi ya mume wake Hishaam kwa kupishana miaka kumi na miwili, na Hishaam alizaliwa mwaka wa 60H, Fatuma alizaliwa mwaka 48H, na alifariki Mama wa Waumini Ummu Salama mwaka 59H, na Fatuma akiwa mdogo hakukutana naye, basi ni vipi apokee kutoka kwake na wala hakusikia kutoka kwa shangazi wa baba yake Bi Aisha Mama wa Waumini kitu chochote, bali kusikia kwake ni kwa bibi yake Asmaa bint Abi Bakri Swiddik – R.A

Mjadala huu unasikitisha, hakuna ulazima wa kukatika Hadithi kwa sababu ya Fatuma bint Al-Mundhir alikutana na Ummu Salama akiwa mdogo, kwani mtoto mdogo kuna uwezekano wa kazingatia sana vitu na kuvihifadhi, na mlisema: Fatuma wakati wa kufariki kwa Ummu Salama alikuwa bint wa miaka kumi na moja, huu ni umri mzuri hasa kwa mwanamke kwani inafaa kuolewa katika umri huu, ni nani huyo katika umri wa kuoelewa inasemwa kuwa hana akili ya kusikia wala kufahamu yanayotokea? Huu ni mtazamo batili ambao haujibiwi pamoja na Ummu Salama alikuwa mkweli kwa bibi yake Asmaa, na nyumba yao ilikuwa moja, Fatuma huyu alikulia mikononi mwa bibi yake Asmaa pamoja na shangazi wa baba yake Bi Aisha R.A na Ummu Salama, na Bi Aisha alifariki mwaka wa hamsini na saba, na ikasemwa pia alifariki mwaka hamsini na nane, inawezekana Fatuma kamsikia, ama bibi yake Asmaa alifariki mwaka wa sabini na tatu na Fatuma wakati huo alikuwa binti wa miaka ishirini na tano hivyo alisikia mengi kutoka kwake ([27]).

Kama vile haijifichi kuwa usahihishaji wa Tirmidhy na Hakimu wa Hadithi hii kunaondoa kasoro ya kukatika kwa wapokezi, kwani Maimamu hao wawili hawasahihishi kilichokuwa kimekatika wapokezi isipokuwa inakuwa sahihi kwao muunganiko wake, kama ilivyoelezwa kwenye elimu ya Hadithi kuwa Hadithi iliyokatika wapokezi wake ni katika kundi la Hadithi dhaifu ([28]).

Ama Hadithi inayosema: “Hakuna kunyonyesha baada ya kuacha kunyonya” yenyewe ni katika upokezi wa Muammar kutoka kwa Juwaibar kutoka kwa Dhihhak kutoka kwa Nizaal Ibn Sabra kutoka kwa Ally kutoka kwa Mtume S.A.W, nayo ni Hadithi iliyokatika mpokezi, kwa sababu Juwabara amedondoka na Dhihhaku ni dhaifu.

Na Hadithi: “Hakuna kunyonyesha baada ya kuacha kunyonya” nayo ni kwa upokezi wa Muammar pia kutoka kwa Haram Ibn Othman kutoka kwa Abdilrahman na Muhammad Ibn Jabir Ibn Abdillah kutoka kwa baba zao kutoka kwa Mtume S.A.W yakatajwa maneno mengi ndani yake Hadithi iliyopita, nayo pia amedondoka mpokezi, kwa sababu Hiraam Ibn Othman amekosekana mara moja.

Ama kauli ya Mola Mtukufu: {Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini} Al-Ahkaaf: 15. Na kauli ya Mola Mtukufu: {Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha} Al-Baqarah: 233. Na kauli yake: {Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili} Luqman: 14. Wakasema – kwa maana ya Jamhuri – Mwenyezi Mungu Mtukufu amekata kuwa kumwachisha kunyonya mtoto ni miaka miwili, na kunyonyesha miaka miwili kamili kwa mwenye kutaka kukamilisha kunyonyesha, wakasema: Hakuna kabisa kunyonyesha baada ya miaka miwili, kwa sababu kunyonyesha kumekamilika, kukikatika unyonyeshaji inakuwa pia hukumu yake imekatika ya kuharamisha na yasiyokuwa hayo, jibu lake – kama anavyosema Ibn Hazmi – Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema ni wajibu wetu kusimama alipoainisha Mola Mtukufu, lau kusingekuwa na Aya kwenye hili basi ingekuwa maelezo haya yanaelea, lakini zimekuja Aya katika hilo: Tuliyopokea kwa Imamu Muslimu kuwa Amru Naakid na Ibn Abi Omar wote wamesema: Mimi Sufyani Ibn Ayiina kutoka kwa Abdilrahman Ibn Kassim Ibn Muhammad Ibn Abi Bakri Swadik kutoka kwa baba yake kutoka kwa Bi Aisha Mama wa Waumini R.A amesema:

 “Sahlah bint Suhail alikuja kwa Mtume S.A.W akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mimi ninaona uso wa Abi Hudhaifa kuingia kwa Salimu naye ni kijana wake wa kazi, Mtume S.A.W akasema: “Mnyonyeshe” Sahla akasema: Ni vipi nimnyonyeshe hali ya kuwa ni mkubwa? Mtume S.A.W akatabasamu na akasema: Nimeelewa kuwa ni mtu mkubwa”, na kuendelea katika njia za Hadithi zingine, Hadithi hii inaondoa shaka na kubainisha kusudio la Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya zilizotajwa kuwa kunyonyesha ambako kunakamilika ni kwa kukamilika miaka miwili, au kwa kuridhia wazazi wawili kabla ya miaka miwili ikiwa wataona katika hilo kuna masilahi kwa mtoto kwa kumlipa mnyonyeshaji, Aya ya Qur`ani ilitosheleza katika hili kwa sababu Mola Mtukufu amesema:

{Na wazazi wanawake wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada} Al-Baqarah: 233. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamrisha wazazi wa kike kunyonyesha watoto kwa kipindi cha miaka miwili, na katika hili hakuna uharamu wa kunyonya baada ya muda huo kwa sababu uharamu kwa kunyonya unakatika kwa kukamilika miaka miwili, na imekuwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya} An-Nisaa: 23, wala Mwenyezi Mungu hakusema miaka miwili wala baada ya miaka miwili kwenye Aya zingine, kwa ujumla ni kuwa haifai kuhusisha isipokuwa kwa Aya inayobainisha kuwa ni wakati maalum na wala si kwa kudhani wala kukadiriwa kusiko na ufafanuzi wake.

Hivyo katika jibu hili la Ibn Hazmu kuna mambo mawili:

Jambo la Kwanza: Dalili ya Jamhuri katika Aya hizi kuwa kunyonyesha kuliko haramu ni kipindi cha miaka miwili katika utoto, imejibiwa na yaliyokuja ndani ya kisa cha Sahla na Salimu kijana wa kazi wa Abi Hudhaifa.

Jambo la Pili: Aya hizi zinazungumzia muda wa kunyonyesha uliowajibu wa kumlipa mnyonyeshaji, na wala hakuna maelezo ya uharamu baada ya huo muda, wala uharamu unakatika kwa kukamilika miaka miwili, bali kauli yake Mola Mtukufu: {Na mama zenu walio kunyonyesheni na dada zenu kwa kunyonya} hakuna ndani yake kuainisha miaka miwili wala wakati pasi ya wakati wa kuongezeka kidogo kwenye Aya zengine, kwa ujumla haifai kuhusisha isipokuwa kwa Andiko linalobainisha kuwa muda huo umehusishwa na wala si kudhani, wala kuchukuliwa bila ya ufafanuzi.

Jambo la kwanza linajadiliwa kuwa Hadithi ya Sahla na Salimu ni maalumu kwao, na kutokea kwake ni tukio maalumu wala si kwa wote – maelezo haya ni moja ya majibu ya Jamhuri kuhusu Hadithi – ambapo wamesema: Ama Hadithi ya Salimu jibu lake lina sura mbili:

Sura ya Kwanza: Imepokeswa na Mama wa Waumini Ummu Salama mke wa Mtume S.A.W alikuwa anasema: Wake wengine wa Mtume S.A.W wamekataa kuingia kwao yeyote kwa sababu ya kunyonya – kwa maana ya kunyonya ukubwani – na wakasema kumwambia Bi Aisha: Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu hatuoni hili isipokuwa ni ruhusa aliyoitoa Mtume wa Mwenyezi Mungu maalumu kwa Salimu, wala haikuwa ruhusa kwa yeyote kuingia kwetu kwa sababu ya huku kunyonya ([29]), hii inaonesha kuwa Salimu alikuwa ni maalumu kwa hilo, na wala haikuwa maalum kwa watu wengine, haikubali ulinganishi, wala hatuachi asili iliyokubalika katika Sharia.

 Sura ya Pili: Imefutwa, kwa maana: Kunyonya ukubwani kulikuwa kunapalekea uharamu kwa kunyonya kisha ikafutwa kwa Hadithi iliyopita ([30]).

Al-Hafidh Ibn Hajar amesema: Wamejibu kuhusu kisa cha Salimu kwa majibu mengi miongoni mwayo ni kuwa hukumu imefutwa, na wengine wakasema kuwa kisa cha Salimu kilikuwa mwanzoni mwa kuhama Mtume S.A.W, na Hadithi zinaonesha juu ya mazingatio ya miaka miwili kutokana na mapokezi ya Maswahaba, ikaonesha juu ya kuchelewa kwake, nao ni upokezi dhaifu: Ambapo kuchelewa kusilimu kwa mpokeaji na udogo wake hakupelekei kutokubalika alichokipokea hapo mwanzo, katika kisa cha Salimu kinaonesha kutangulia hukumu ya miaka miwili, kwa kauli ya mke wa Abi Hudhaifa katika baadhi ya njia zake za upokezi ambapo Mtume S.A.W alimuambia: “Mnyonyeshe” akasema: Ni vipi nimnyonyeshe hali ya kuwa ni mkubwa? Mtume S.A.W akatabasamu na akasema: “Nimefahamu kuwa ni mtu mkubwa”, na katika upokezi wa Muslimu alisema mke wa Abi Hudhaifa: Ni mtu mwenye ndevu, akasema: “Mnyonyeshe”, hii inaonesha kuwa mke wa Hudhaifa alikuwa anafahamu mtoto mdogo ndiyo mazingatio katika uharamu unaotokana na kunyonya.

Pia madai ya umaalum wa Salimu na mke wa Hudhaifa, asili ni kauli ya Ummu Salama na wake wa Mtume S.A.W: Hatujaona hili isipokuwa ni ruhusa aliyoitoa Mtume S.A.W maalumu kwa Salimu, na kukubalika na Ibn Swaiyagh na wengine kuwa asili ya kisa cha Salimu ni kutokana na yaliyotokea katika ubini ambao umepelekea kuchanganyika Salimu na Sahla, ilipoteremka amri ya kujizuia ndani na kuondolewa mtoto wa ubini hilo likawa zito kwa Sahla ndipo ikatolewa ruhusa kwake katika hilo ili kuondoa shaka na tabu aliyonayo, katika hili kuna mtazamo, kwa sababu linapelekea kukutana na anayelingana na Sahla katika tabu uzito na kujizuia ndani, kutaondoa umaalum na kuthibiti madhehebu ya kinyume, lakini inapingika, na Maimamu wengine wakasema: Asili ni kuwa kunyonya hakupelekei haramu, wakati linathibiti hilo utotoni inakuwa kinyume na asili na kubakia mengine kwenye asili, kisa cha Salimu ni tukio maalum lina uwezekano wa umaalum hivyo inapaswa kusimamisha kulipinga hilo ([31]).

Imamu Al-Kasany amejibu kuhusu maelezo ya Bi Aisha kwa Hadithi ya Salimu kwa kusema: “Ama maelezo ya Bi Aisha R.A imepokelewa kwake yanayoonesha juu ya kufuta kwake, kwani imepokewa kwake kuwa amesema: Hakuna uharamu wa kunyonya isipokuwa kunyonya kunakootesha nyama na damu, imepokewa kuwa Bi Aisha alikuwa anamuamrisha binti wa kaka yake Abdulrahman Ibn Abi Bakri R.A kunyonyesha watoto wadogo ili waweze kuingia kwake pindi wanapokuwa wakubwa, pamoja na maelezo yake hayo yalipingwa na wake wengine wa Mtume S.A.W kwani wao walikuwa hawataki kuingia kwao mtu yeyote kwa sababu za kunyonya, na lenye kupingwa haliwi hoja” ([32]).

Nikasema: Ambalo linaonekana ni kuwa Bi Aisha ametenganisha kati ya kusudio kuwa ni lishe na kati ya haja ya kunyonya, ni wakati gani kusudio la lishe linakuwa haliharamishi isipokuwa ni kabla ya kuacha kunyonya, na huu ni unyonyeshaji wa watu wote. Ama jibu la pili ni inafaa ikiwa utahitajika ulazima wa uharamu, na kwa sababu ya kuhitajika kinafaa kisichofaa kwa upande mwengine, nayo ni ijitahai ya Mama wa Waumini R.A kwa maana masuala hayazingatiwi kuwa tofauti Kifiqhi ni kama yalivyo masuala mengine ya Kifiqhi yaliyotofautiana, aliyepatia ana malipo ya aina mbili na mwenye kukosea ana malipo ya aina moja.

Jibu la pili la Ibn Hazmu linajadiliwa kwa kauli yetu: Ikiwa tutakubali hilo lakini dalili ya kukatika uharamu kwa kutimia miaka miwili limechukuliwa kwenye Hadithi – ya kuwa kunyonya kunakoleta uharamu ni kule kunakuwa kwa mtoto mdogo, na katika kukata njaa – ni katika maneno ya Mama wa Waumini wote – ukiondoa Bi Aisha – na ni kauli za Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe kwao wote.

Ama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya} An-Nisaa: 23, hakuna kuainisha miaka miwili wala muda pasi ya muda unaongezeka kidogo kwenye Aya zingine, jibu lake ni kuwa: Kusudio lake sio kunyonya mtu mkubwa, kwa sababu Mtume S.A.W amefasiri kunyonya kunakopelekea haramu ni kule kunako ondoa njaa kuotesha nyama kuzalisha mifupa na kufungua utumbo, na hii ni sifa ya kunyonya utotoni na wala si ukubwani, hivyo Sunna imejengea asili ya yaliyomo kwenye Kitabu ([33]).

Ama Hadithi: “Kwa hakika kunyonya ni kukata njaa”, ni hoja ya wazi kwetu, kwa sababu mtu mkubwa katika kunyonya ili kuondoa njaa ni kama mtoto mdogo, huo ndio ujumla wa kunyonya pindi inapofika mifyonzo mitano kama alivyoamrisha Mtume S.A.W.

Linajibiwa hili kuwa tafasiri ya Hadithi pamoja na mliyoyataja kwa umbali wa lengo la tamko, hayakimbiliwi haraka na akili za wenye kuambiwa, bali kauli katika maana yake ni aliyoyasema Abu Ubaida: Ambaye pindi anapokuwa na njaa chakula chake kinachomshibisha maziwa ni mtoto mdogo wa umri wa kunyonya, ama ambaye njaa yake anashiba kwa chakula basi kunyonya kwake sio kunyonya, kama vile hazingatiwi kabisa mwenye ndevu kunamshibisha kunyonya maziwa ya mwanamke na kumuondolea njaa, tofauti na mtoto mdogo ambapo hana kinachochukuwa nafasi ya maziwa, kwani yenyewe ndio yenye kumuondolea njaa, lakini mkubwa si mwenye njaa ya kuhitaji maziwa ya mwanamke, ambalo linafafanua hili ni kuwa Mtume S.A.W hakuelezea ukweli wa njaa bali alichoelezea taswira yake na muda wake, hakuna shaka huyo ni mtoto mdogo, ikiwa mutapinga kuwa amelezea ukweli wake kutawalazimu kuto haramisha kunyonya mtu mkubwa isipokuwa pindi akiridhia akiwa mwenye njaa, na kama ataridhia akiwa mwenye kushiba hakuathiri chochote ([34]).

Kama vile hakuna kinachojificha katika haya wala kuleta shaka kuwa kuondoa njaa kwa kunyonya maziwa ya mwanamke kwenye chuchu za mnyonyeshaji ni kunakuwa kwa yule asiyekuwa na chakula wala kinywaji zaidi ya hayo, ama mwenye kuwa anakula na anakunywa basi huyo njaa yake haiondoki wakati wa kuhitaji zaidi ya kula na kunywa, na kunyonya kuwa kunaweza kuondoa njaa ya mkubwa ni jambo lisilo na ushindani, kwani hakuna ushindani kwa anayeweza kuondoa njaa yake kwa maziwa, lakini ushindani ni kwa asiyeweza kuondoa njaa yake kwa maziwa ([35]).

Hivyo kama maelezo yalivyotangulia ni wazi kuwa majibu ya Ibn Hazmu kuhusu dalili za Jamhuri si zenye kukubalika kwa ujumla wake, hata kama kuna udhaifu katika Hadithi chache ambazo Jamhuri wamezitumia kama dalili isipokuwa Hadithi hizi hazichukuliwi sawa na dalili zengine, kama ilivyosemwa: Kujibu dalili maalumu hakumaanishi ni jibu la dalili fulani.

Pingamizi lingine amelitaja Ibn Hazmu na akajibu kwa kusema:

Msemaji anaweza kusema: Hadithi hii ni maalum kwa Salimu kama walivyosema baadhi ya wake wa Mtume S.A.W kisha akajibu kwa kusema: Anapaswa kufahamu mwenye kuielezea Hadithi hii kuwa ni dhana ya mwenye kudhani hivyo miongoni mwao, kama hivi imekuja katika Hadithi kuwa wake wa Mtume wanasema: Hatuoni hili isipokuwa ni maalum kwa Salimu, na wala hatufahamu huenda ni ruhusa maalumu kwa Salimu, hiyo ni dhana bila ya shaka yeyote, kwani dhana haipingi Sunna, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Hakika ya dhana haisaidii chochote mbele ya haki} An-Najmi: 28, ni pande mbili kati ya kupinga kwa Ummu Salama R.A na kati ya kupinga Bi Aisha Sunna iliyothibiti, na kauli yake: Una nini kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kigezo chema? Kunyamaza kwa Ummu Salama kunaonesha kurudi kwake kwenye haki.

Linajadiliwa jibu hili – kuongezea na maelezo yaliyotangulia – na Hadithi iliyopokelewa na Baihaqy kutoka kwa Shafi ambapo amesema: Ametueleza Abu Said, ametuambia Abu Al-Abbas, ametuambia Rabii amesema: Shafy amesema: Hili Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua zaidi kwa Salimu kijana wa Abi Hudhaifa ni maalumu kwake, ikiwa atasema mwenye kusema: Ni ipi dalili juu ya ulichoelezea? Nitasema….Hadithi ya Ummu Salama yenyewe imetaja Hadithi ya Salimu kutoka kwa Mtume S.A.W na akasema katika Hadithi: Ilikuwa ni ruhusa maalum kwa Salimu, Shafi amesema: Tumechukuwa maelezo haya kwa uyakini na wala si dhana ([36]).

Akabainisha Imamu Shafi kuwa Hadithi iliyopokelewa na Ummu Salama haikuwa ijitahadi yake bali kauli yenye nguvu ni kuwa imenukuliwa kutoka kwa Mtume S.A.W ambapo katika mapokezi haya hayakuja maneno mawili: “Hatuoni Hadithi hii ni maalumu kwa Salimu” na “Wala hatufahamu huenda ni ruhusa kwa Salimu” ikawa kuichukua ni kwa upande wa kuwa kwake yakinifu na wala si dhana, na Ummu Salama R.A hazingatiwi kuwa mpokezi mwenye kunukuu yale aliyoyabainisha Mtume S.A.W. na kunyamaza kwa Ummu Salama peke yake hakumaanishi kurejea kwake.

Madhehebu ya Ibn Taimia na Ibn Al-Qayyim:

Ibn Taimia na mwanafunzi wake Ibn Qayyim wamesema kuwa Hadithi ya Sahla haijafutwa wala sio maalumu wala si ya yote, bali ni ruhusa kwa haja ya asiyeweza kuachana na kuingia kwa mwanamke na kupata tabu ya kujizuia naye, kama vile hali ya Salimu na mke wa Abi Hudhaifa, ni kama huyu mtu mkubwa pindi anaponyonyeshwa kwa haja maalum kuna athari ya kunyonya kwake, ama asiye kuwa yeye hakuna athari isipokuwa kunyonya kwa mtoto mdogo.

Wakasema: Hadithi inakanusha kunyonya katika ukubwa: Ima moja kwa moja na kuambatanishwa na Hadithi ya Sahla, au katika hali zote na kuhusishwa hali hii katika ujumla wake.

Wakasema: Hii ni bora zaidi kuliko kufutwa na madai ya kuhusishwa na mtu maalum, ni karibu zaidi ya kufanyia kazi Hadithi zote kwa pande mbili, na kanuni ya Sharia inashuhudia hilo.

Ibn Taimia amesema: “Inafaa kwa haja kile kisichofaa kwa kitu kingine, na hii ni kauli inayoelekewa” ([37]).

Kwa mtazamo huu ameelezea Shaukany na akasema: Haya ndio marejeo yangu, marejeo haya yanakusanya kati ya Hadithi zote, na hilo ni kwa kufanya kisa kilichotajwa cha Salimu kimehusisha kwa wote: “Hakika kunyonya ni katika kukata njaa”, “Wala hakuna kunyonya isipokuwa ndani ya miaka miwili”, “Hakuna kunyonya isipokuwa ni kufungua utumbo na inakuwa kabla ya kuacha kunyonya”, “Hakuna kunyonya isipokuwa ni kunakozalisha mifupa na kuotesha nyama”, hii ni njia ya kati na kati baina ya njia ya mwenye kuzifanya Hadithi hizi ni dalili ya hakuna hukumu kabisa ya kunyonya ukubwani, na baina ya mwenye kufanya kunyonya ukubwani ni kama tu kunyonya utotoni ([38]).

Kauli zingine katika masuala haya:

Kuna kauli zingine katika masuala haya – tofauti na kauli tatu maarufu zilizotangulia – katika kuainisha muda ambao unathibiti ndani yake uharamu, miongoni mwake:

Kunyonya kunakopelekea uharamu ni kule kabla ya kuacha kunyonya, haya ndiyo yaliyosemwa na Ummu Salama, na kupokelewa na Ibn Abbas, na pia ameyasema Al-Hassan, Az-Zahry, Al-Auzaii, Akrama na Qatada.

Kunyonya katika hali ya utoto kunapelekea uharamu, msemaji pasi ya kuweka mpaka, yamepokewa hayo kutoka kwa wake wa Mtume S.A.W tofauti na Bi Aisha Mungu amuwie radhi, na kutoka kwa Ibn Omar na Saidi Ibn Al-Musayyab. 

Kunyonya kunakopelekea uharamu ni umri wa miaka mitatu, nayo yamepokewa na kundi la watu “Kuufa” pia amepokea Al-Hassan Ibn Saleh.

Kunyonya kunakopelekea uharamu ni wa umri wa miaka saba, yamepokelewa hayo kutoka kwa Omar Ibn Abdilaziz.

Kunyonya kunakopelekea uharamu ni unyonyaji wa miaka miwili na siku kumi na mbili, yamepokelewa hayo kutoka kwa Rabiia ([39]).

Sifa ya mkubwa kunyonya:

Miongoni mwa yaliyoleta tatizo katika Hadithi ya Sahla na Salimu ni Mtume S.A.W kumuamrisha kumnyonyesha, kutokana na kukutana kwa ngozi mbili, nako ni haramu kabla ya kukamilisha kunyonya kunakozingatiwa, na mwisho kuwa ni haramu kwake kumuoa.

Jibu la hilo ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Maana halisi ya kunyonya ni kufika maziwa kwenye utumbo wa mtoto mdogo, ama namna ya kufika hakuna sura ya Kisharia inayopaswa kufuatwa na kuzingatiwa, kinachozingatiwa ni kufika maziwa ndani ya utumbo wa mtoto wa kunyonya.

Na kunyonya kwa maana ya kilugha: Ni jina litokanalo na kunyonya ([40]), nalo ni jina la kunyonya chuchu na kunywa maziwa yake ([41]), kwa upande wa Kisharia: Ni jina la kupata maziwa au linalopelekea kupata maziwa ndani ya utumbo wa mtoto mdogo au kulisha akili yake ([42]), na Al-Jarjany amesema: Ni kunyonya mtoto mdogo chuchu za mwanadamu katika umri wa kunyonya ([43]), na baadhi ya Wanachuoni wakaelezea kuwa: Kunyonya mtoto wa chini ya miaka miwili maziwa yaliyojitengeneza kutokana na ujauzito au akayanywa na mfano wake ([44]).

Imeonekana kwa maelezo yaliyotangulia kuwa makusudio ya kunyonya chuchu ni kwa mtoto mdogo wa kunyonya au aliye na umri wa chini ya miaka miwili hivyo hapa hakuna nafasi wala sehemu kwa mtu mkubwa, na kwa mtazamo huu kunywa maziwa bila ya kutumia chuchu za mwanamke kunafaa kuwa kunyonya.

Kisha tunajiuliza swali: Je mtoto mdogo ambaye anakunywa maziwa bila ya kuyanyonya moja kwa moja kwenye chuchu ya mwanamke ([45]) kunathibiti hukumu ya kunyonya au hapana? Jibu: Ni kuwa inathibiti kwake hukumu ya kunyonya kwa kauli ya Jamhuri, hakuna aliyekwenda kinyume na kauli hiyo isipokuwa ni Al-Dhwahiriya, wakaweka sharti la kunyonya kwenye chuchu za mwanamke moja kwa moja.

Jamhuri ya Wanachuoni wamekubaliana kuwa lishe kwa kutumia maziwa ya mama mnyonyeshaji kunapelekea uharamu, ni sawa sawa ikiwa kwa kunywa au kula kwa sifa yeyote itakayokuwa, hata kwa kutumia sindano au kupitishia puani kwa kutumia mipira na zisizokuwa njia hizo, pindi zinapotumika kwa njia inayotakiwa, ikiwa itaondoa njaa uharamu upo kwa njia zote hizo, ukiacha watu wa Abu Hanifa wao wameondoa matumizi ya sindano.

Pili: Kadhi Ayyadh amesema: Huenda Sahla aliyakamua kisha Salimu akayanywa pasi ya kugusa chuchu za Sahla wala kugusana ngozi zao, Imamu An-Anawawy amesema: Haya ambayo ameyasema Hassan, amesema: Inachukuliwa kuwa aliruhusiwa kumgusa kwa haja iliyopo, kama alivyohusishwa kunyonya pamoja na kuwa mkubwa. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi ([46]).

Ikiwa patasemwa kuwa imepokelewa katika Hadithi kauli ya Sahla: Ni vipi nimnyonyeshe naye ni mtu mkubwa? Tunasema: Sahla wala haulizi kuhusu kumnyonyesha kwake, bali huku ni kushangazwa kwake, kwa kile anachokifahamu kuhusu kunyonya hakuwi isipokuwa kwa mtoto mdogo.

Yanayounga mkono maelezo haya ni yaliyopokewa na Ibn Saad katika kitabu chake na kutajwa na Ibn Hajar katika kitabu cha Al-Iswaba kutoka kwa Muhammad Ibn Abdillah Ibn Akhy Az-Zahry kutoka kwa baba yake amesema, Sahla alikuwa anakamua kwenye chombo matone ya maziwa yake na kumnywesha Salimu kila siku mpaka akanyonya ndani ya siku tano, baada ya hapo ikawa anaingia Sahla akiwa kichwa wazi na mikono wazi, ni ruhusa Sahla aliyoipata kutoka kwa Mtume S.A.W ([47]).

Ufupisho wa Utafiti

Kauli iliyopitishwa na kukubaliwa katika masuala haya ni kauli ya Jamhuri ya Wanachuoni kuwa kunyonya ukubwani hakupelekei uharamu, na Hadithi ya Sahla na Salimu – Kijana wa kazi wa Hudhaifa – ni tukio maalumu na wala si kwa wote.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Imeandikwa Na: Mustafa Abdulkareem Muhammad

29/07/2007.

Imepitiwa Na: Muhammad Al-Sayyid.

Ndoa ya Misyaar

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Ndoa ni mkataba wa maneno baina ya watu wawili; mwanamume na mwanamke ambao hawana vizuizi vya kisheria, hali yake kama mkataba wowote ambao unasihi kisheria kwa kupatikana sharti na nguzo zake na kutokuwepo vizuizi vyovyote. kadhalika mkataba katika Fiqhi ya Kiislamu kimsingi unaweza kuwa kwa maneno.

Basi kama likifanywa katika upande wa kuanza kutoka kwa aliye na sifa kamili za kutenda, masharti na nguzo zake zikiwa zimekamilika bila vizuizi, basi huzingatiwa kuwa mikataba ni sahihi, inafuata athari zake na hukumu zinazofuatia.

Katika ndoa ya Misyaar, mkataba wa ndoa unafungwa, sharti na nguzo zinatimizwa, ila mwanamke anakubaliana na mumewe ili aiche haki yake ya kulala naye na kumpa matumizi au mojawapo ya mawili hayo.

Na "Misiyar" silo neno la kiajemi –kama anavyosema Sheikh Al Qaradhawiy- lakini ni neno la kawaida katika lahaja za nchi za Ghuba, labda maana yake ni kupita na kutokaa muda mrefu, basi inadhihirika ndoa ya Misiyar ilichukua maana yake kutokana na  maana hiyo. [Fatawa Muasweraha 291/3]. Kwani mwanamume katika ndoa hiyo anamtembelea mke wake katika nyakati mbalimbali, na hakai naye muda mrefu.

Kimsingi aina hiyo ya ndoa ni halali ikiwa mkataba umetimiza sharti na nguzo zake zinazotakikana kisheria, nazo ni: ijaabu (makubaliano ya kuoana), kuwepo kwa walii, mashahidi na kutokuwepo vizuizi vya kisheria kwa wanandoa.

Mkataba huo ukitimizwa sharti na nguzo zake, basi unakuwa na haki zinazoambatana na mkataba wa kindoa kama vile Nasaba, Urithi, Eda, Talaka, kuingiliana, kukaa na matumizi na wajibu na haki nyingine ziambatazo na ndoa, lakini wanandoa wakiafikiana kwamba mke aache haki ya kukaa au kupata matumizi, basi mwanamke akiacha haki yake au baadhi yake inajuzu kisheria kwani yeye ndiye mwenye haki hiyo naye anaweza kuiacha bila ya kuathiri hali ya kusihi mkataba wa ndoa.

Ibn Qudama alisema katika kitabu chake “Al Mugh-niy” alipozungumzia aina za masharti ya ndoa: “Sehemu ya pili: yanayobatilisha sharti na yanayohahikisha mkataba, kama vile ikishurutishwa kutokuwa na mahari kwa mke au kutompa matumizi au mke ashurutishe asiingiliane na mumewe au mumewe atumie kinga ya kuingiliana (kinga za mimba) au mumewe ampe siku zaidi ya mke mwenza au mumewe ashurutishe asimtembelee zaidi ya siku moja kila wiki au amtembelee mchana tu bila ya usiku au mumewe amshurutishe mkewe ampe matumizi au ampe kitu angalau hata kidogo, basi masharti hayo yote ni batili; kwani hayaafikiane na maana inayotakikana na mkataba tena kwa kuwa yanamaanisha kuondosha yaambatanazo na mkataba hata kabla ya kufungika, kwa hiyo haijuzu kama ilivyo haki ya wamiliki wawili, mmoja hana haki ya kumshurutisha mwenzake aiache haki yake kabla ya mauzo.

 Ama mkataba wenyewe, basi unakuwa ni sahihi; kwani masharti yale yanaambatana na vitu vya ziada ambavyo havilazimishwi kuvitaja tena haidhuru kutovitaja kwa hiyo havibatilishi mkataba kama ikishurutishwa mahari ambayo asili yake ni haramu”. [Al Mughniy 72/7]

Suala la kujuzu kwa mwanamke aache baadhi ya haki zake wakati wa kufunga mkataba wa ndoa yake linarejea maneno ya Mwenyezi Mungu: {Na mwanamke akichelea kutupwa na kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekwa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamungu basi hakika Mwenyezi Mungu Anazo khabari za yote mnayoyatenda} [AN-NISAA, 128].

Ilisimuliwa kutoka kwa Mama wa Waumini Bi. Aisha R.A. ya kwamba sababu ya kushuka kwa Aya hiyo ni: “Mume anakuwa na mke hali ya kuwa amemchukiza hamtaki anataka kuachana naye, na mkewe amwambie: “nakupa uhuru wa kuniacha”, basi Aya hiyo ilishuka katika suala hilo”. [Sahihi Al Bokhariy 2318]

Na Kutoka kwa Ibn Abass R.A. alisema: “Bi. Sauda aliogopa Mtume s.a.w. amwache akamwambia: usinipe talaka niache niishi nawe na siku yangu mpe Bi. Aisha, basi Mtume S.A.W. akafanya na hiyo Aya ilishuka: (basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora)”. [Sunan At Tirmiziy 3040]

Ndoa ya Misyaar siyo mpya katika Fiqhi ya Kiislamu lakini jina lake ndilo jipya na aina hiyo ni ya zamani ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la ndoa ya “NAHARIYAT AU LAYLIYAT (ndoa ya kukutana mchana au usiku)”, na mazingatio hapa yanakuwa katika hukumu siyo majina.

Ilitajwa katika kitabu cha Fat-h Al Qadir kilichotungwa na Al Kamal bin Al Hamam Al Hanafiy: “Si vibaya kuwaoa AL NAHARIAT nao ni: kuwaoa wanawake sharti kukutana nao mchana sio usiku”. [Kitabu cha Fat-hu Al Qadeer 249/3]

Imamu Ahmad alisema - kama ilivyotajwa katika kitabu cha Al Mughniy - katika suala la mwanamume ambaye kamwoa mwanamke akamshurutisha akae naye mara moja kila wiki halafu mkewe akarejea na kusema: sikubali ila siku baada ya siku, akasema Imamu Ahmad: Ana haki ya kuachana na ombi lake kwa hiari yake na hiyo inajuzu ama akisema: Sikubali ila baada ya kugawanya masiku, basi ni haki yake anaweza kuiomba muda wowote akitaka. Aidha ilisimuliwa na Al Athram katika suala la mwanamume anayemwoa mwanamke akamshurutisha aende kwake siku maalumu kwamba inajuzu lakini mkewe akifuta maneno yake akirudi kuomba haki yake basi anakuwa na haki ya kuomba, kadhalika alisema katika suala la mwanamume anayemwoa mwanamke sharti ampe matumizi ya derham tano au kumi kila mwezi ya kwamba ndoa hiyo inajuzu kisheria, naye mkewe ana haki ya kufuta maneno yake. Naye Al Maruzi alirejea aliyoyasema Imamu Ahmad katika suala la Al Nahariat na AL Layliyat akasema: Aina hiyo ya ndoa haiafikiani na ndoa ya watu wa Uislamu. Naye Hamad bin Abi Sulaiman na Ibn Shubruma ni miongoni mwa waliochukizwa na  suala la kuwaoa AL NAHARIYAT. Na Al Thauriy alisema: Hapa sharti ni batili. Ingawa Al Hassan na A’twaa walikuwa haoni vibaya katika ndoa ya AL NAHARIYAT, naye Al Hassan alikuwa haoni vibaya kwa mtu amwoe mwanamke sharti aainishe kwake siku maalumu kukutana naye kila mwezi. Hapa uchukizo wa wanaochukizwa na suala hilo unarejea kubatilisha sharti na kujuzu kwa wanaojuzu kunarejea asili ya ndoa, kwa hiyo maoni yao yanaafikiana juu ya usahihi wa ndoa na kubatilisha sharti. [Al Mughniya kwa Ibn Qudamah 72/7 kwa mageuzi madogo]

Maana ya kauli ya Imamu Ahmad: Aina hiyo ya ndoa haiafikiani na ndoa ya watu wa Uislamu; si ndoa kamili, kama unavyosema: Si Muumini asiyependa ya nduguye, kwa anayoyapenda ya nafsi yake. [Kitabu cha Fatawa Muaserah kwa Sheikh Al Qaradhawiy 294/3] Na maana inayotakikana hapa: Si Muumini mwenye imani kamili asiyependa ya nduguye kwa anayoyapenda ya nafsi yake.

Ingawa baadhi ya Maulamaa wameelekea kutojuzu aina hiyo ya ndoa, wakapata dalili kuthibitisha kauli yao, na miongoni mwa dalili hizo ni:

Mkataba katika aina hiyo ya ndoa unakuwa unaambatana na baadhi ya masharti yanayohitalifiana na lengo “maana” la mkataba, kama sharti la mwanamke kuachana na haki yake katika kugawanya siku za wiki na mke mwenza, matumizi n.k., masharti hayo ni mabaya yanaweza kubatilisha mkataba.

Ilitangulia kujadili dalili hizo kutokana na kauli ya Imamu Inb Qudama kuhusu sehemu ya pili ya masharti ya ndoa, ambayo ilitajwa kwamba mkataba unajuzu kisheria lakini unakuwa na sharti baya.

Ndoa kwa aina yake hiyo inahitalifiana na makusudio ya Sheria ya Kiislamu yanayoelekeza kuleta pahala pa kukaa, mapenzi pamoja na ulezi kwa watoto.

Kiufupi: sisi hatusemi kwamba aina hiyo ya ndoa haiafikiani na ndoa sahihi ya Kiislamu inayotakikana, [[Kitabu cha Fatawa Muaserah kwa Sheikh Al Qaradhawiy 295/3]. Bali tunasema kwamba aina hiyo inalifikia lengo kuu la ndoa nalo ni kujizuia na machafu kama ilivyokuja katika Hadithi ya Mtume S.A.W,  “Enyi vijana yeyote anayekuwa na uwezo wa ndoa, basi aoe kwani inamwondolea tamaa na kulinda tupu”. [Imeafikiana nayo, Sahihu Al Bokhariy 4779, na Sahihi Muslim 1400]

Ndoa ya Misyaar kimsingi inategemea hali ya usiri na kufichika na asili ya ndoa katika Sheria ya Kiislamu ni kutangazwa.

Hapa baadhi ya watu walijibu kauli hiyo kwamba suala la usiri silo kitu cha msingi katika aina hiyo ya ndoa, bali aina hiyo inaweza kuwa na aina ya tangazo na rekodi katika masjala ya kiserikali (rasimu) aidha suala la kuficha ndoa baada ya kukamilika masharti na nguzo zake hakuifanyi kuwa ni batili kwa mujibu wa maoni ya wengi wa Maulamaa wa kifiqhi.

Na yaliyonakiliwa na Wamaliki kuhusu suala la kushurutishia hali ya usiri kwa mashahidi ili wafiche habari ya ndoa, basi hayo yanajibiwa kwamba mashahidi wakishurutishwa wawe na usiri wakati wa kufunga mkataba, ama ikitokea bada ya kufunga mkataba basi haidhuru. [Kitabu cha Fatawa Muaserah kwa Sheikh Al Qaradhawiy 300/3- pamoja na As Sharhu Al Kabeer Sheikh Ad Dardier 236/2]

Ndoa hiyo inakuwa na aina nyingi za marufuku za kisheria, kwani baadhi ya wanawake wanaweza kuchukua aina hii ya ndoa kama ni njia ya kufanya machafu wakadai kwamba wameolewa kwa njia ya ndoa ya Misyaar, kwa hiyo inalazimika kukataza aina hiyo ya ndoa ili kujiepusha na mambo ya shaka.

Ingawa kauli hii inajibiwa kwamba inapindukia mipaka katika suala la kujiepusha na mambo ya shaka, kwani aina hiyo ya ndoa inaweza kusaidia katika kuilinda nafsi na mambo machafu.

Ndoa ya aina hiyo inaletea madhara kwa mke wa kwanza; kwani mumewe atatembelea mkewe wa pili kukaa nae na kufanya mapenzi naye bila ya mke wa kwanza kujua, jambo ambalo linapuguzia haki ya mke wa kwanza.

Rai hiyo inajibiwa kwamba, si lazima ndoa hiyo ya Misyaar iwe ya pili, bali inaweza kuwa ya kwanza au ya pili tena mke anaweza kuwa na taarifa nayo.

Tena mume akiwa na mke wa pili lakini analificha suala lake kwa mke wa kwanza, basi haidhuru ikiwa anaangalia kwa uangalifu haki za mke wa kwanza katika kukaa naye na matumizi yake n.k.

Aina hiyo ya ndoa inavunja heshima ya mwanamke, licha ya kuwa haina mwelekeo wa hali ya jambo baadaye kwa talaka akiomba mke haki yake kugawanya siku za wiki au akiomba haki yake ya kupata matumizi, aidha aina hiyo ya ndoa inakuwa kama njia ya kumkandamiza mke kutokana na hali yake ilivyo; kwani yeye akipata mume kwa mujibu wa ndoa ya kawaida hatakubali kwa namna hiyo ya ndoa ya Misyaar.

Rai hiyo inajibiwa kwamba, hakuna uhusiano wa karibu kati ya hali ya kuomba mke haki yake katika kugawanya siku za wiki na mke mwenza au kupata matumizi na kuachika “kutalikiwa”; kwani talaka inaweza kutokea kwa sababu yoyote nyingine mbali na kuomba mke haki yake ya kupata matumizi au kugawanya siku za wiki na mke mwenza.

Mume kwa mujibu wa ndoa hiyo anaweza kumkandamiza mkewe akiona ana mali na utajiri hali ya kuwa mke ana shida naye, basi anaweza kumkandamiza ili apate manufaa yoyote.

Rai hiyo inajibiwa kwamba, kumkandamiza mke kunaweza kutokea hata katika ndoa ya kawaida, bali jambo hilo linatokea mara nyingi, mume anamkandamiza mkewe halafu anamwacha au anampa talaka, na jambo hilo linaambatana zaidi na imani na tabia na halina uhusiano na aina ya ndoa.

Aina hiyo ya ndoa haiafikiani na yaliyotajwa na Mwenyezi Mungu kuhusu mume na haki yake ya kuwa mlinzi wa mkewe; kwani katika aina hiyo ya ndoa hatobeba jukumu la kutoa matumizi wala pahala pa kukaa, naye Mwenyezi Mungu Amefanya mume awe mlinzi wa mkewe kwa mambo mawili;

La kwanza: Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine kwa sababu ya sifa ambazo Mwenyezi Mungu Amewapa ili wawe na uwezo wa kuvumilia na subira.

 La pili: kwa wanazozitoa; mahari na matumizi.

Rai hiyo inajibiwa kwamba kukubali kwa mume suala la mkewe kuacha haki yake ya kupata matumizi hakumaanishi mume aache haki yake ya kuwa mlinzi wa mkewe; hakuna uhusiano baina ya masuala hayo mawili.

Upambanuzi katika tofauti zilizopo kati ya ndoa ya Misyaar na ndoa ya Mutaa’ “ndoa ya muda maalumu”

Ndoa ya mutaa inakuwa kwamba mwanamume anamwambia mwanamke: nakupa kadhaa niingiliane nawe kwa siku moja, mwezi mmoja au mwaka n.k. akiainisha muda kama ilivyotangulia katika mifano au akiuacha bila ya kuainisha yote ni sawa, kama kwamba anasema: nakupa kadhaa niingiliane nawe msimu wa Hija au kwa muda nitakaobaki nchini au mpaka Zaidi arudi hali ya kwamba muda ukiisha talaka inatokea.

Ndoa ya mutaa ni aina mojawapo wa ndoa za kijahiliya, nayo ilikuwa halali mwanzoni mwa Uislamu halafu ikaharamishwa tena ni haramu kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya Maulamaa kwa ujumla; Imamu abu Hanifa, Maliki, Shafii na Hanbali. [Al Mausu'ah Al Fiqhiyah Al Kuwaitiyah 233-334/41

Baadhi ya wapinzani wa ndoa ya Misyaar waliuelekea mtazamo wa Qiyasi kulinganisha baina ya ndoa ya mutaa na ndoa ya Misyaar ili kupata dalili za kisheria za kuharamisha ndoa ya Misyaar, ingawa kuna tofauti kubwa baina ya aina hizo mbili.

Kwani ndoa ya mutaa inakuwa na muda maulumu unaosawazisha ujira au mahari maalumu tena muda huo mara nyingi unaainishwa kwa mujibu wa ujira au mahari tofauti na ndoa ya Misyaar ambayo haiainishiwi muda maalumu tena inakuwa na sifa ya kudumu na inaendelea mpaka itokee talaka.

Halikadhalika mwanamke hapati talaka katika hali ya ndoa ya mutaa lakini anaachana na mumewe wakati wa kuisha muda walioafikiana, hali ya kuwa anapata talaka yake katika ndoa ya Misyaar ikitokea talaka.

Upambanuzi katika tofauti zilizopo kati ya ndoa ya Misyaar na ndoa ya Muhalalishaji

Baadhi ya wapinzani wa ndoa ya Misyaar walielekea kulinganisha baina ya ndoa ya Misyaar na ndoa ya Muhalalishaji ambayo Mtume S.A.W. aliilaani na akamlaani mwenye kuifanya.

Mtazamo huo unajibiwa kwamba. Lengo la mwanamume hapa ni tofauti; maana katika ndoa ya Misyaar mwanamume anakuwa na haja ya kumwoa mwanamke, lakini katika ndoa ya Muhalalishaji, Muhalalishaji anakusudia tendo lake la kumrudisha mwanamke kwa mume wake wa kwanza; katika hali ya ndoa ya Muhalalishaji maana inayotakikana hasa katika ndoa haipatikani.

Lakini ndoa ya Misyaar, maana inayotakikana na ndoa inakuwepo ambapo mwanamume na mwanamke wanaafikiana wawe pamoja, nayo ni ndoa yenye sifa ya kudumu kama kila Muislamu anayekusudia kumwoa mwanamke Muislamu; asili katika ndoa ni nia ya kudumu katika ndoa. [Fatawa Mo'aswerah kwa Sheikh Al Qaradhawiy 298/3]

Kwa ufupi ni kwamba, Misyaar ni ndoa sahihi na inajuzu kisheria ikiwa na nguzo za ndoa na masharti yake yanayotakiwa kisheria, aidha mwanamke akiacha baadhi ya haki zake za kukaa au kupata matumizi ya nyumbani au mojawapo ya hayo ni jambo ambalo halibatilishi mkataba wa ndoa, ingawa mwanamke ana haki ya kuomba baadaye haki yake ya kukaa na kupata matumizi ya nyumbani wakati wowote akitaka, naye mumewe analazimika kulitekeleza ombi lake.

Tena aina hiyo ya ndoa licha ya kuwa ni sahihi ila ikipatikana khofu ya kuwepo madhara au uovu katika jamii kuenezwa – kama kwamba watu waache ndoa ya iliyozoeleka inayokubalika wakaelekea ndoa ya Misyaar – hapo kiongozi anaweza kuizuia kwa sababu hiyo, na hilo linaingia katika mlango wa siasa ya kisheria kama alivyofanya Omar R.A. alipomwamrisha Huzaifa R.A. amwache mke wake myahudi akisema: “ninachelea kuwa mtawaacha wanawake Waislamu  na kuwaoa wanawake ambao hawakutulia”. Ingawa asili katika ndoa hiyo ni sahihi. [Moswanaf Abdulrazaq 176/7]

Naye Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi.

Imeandikwa na  Mustafa Abdul Karim Muhammad

6/8/2007

 

[1] Sahihi Muslimu: 1453.

[2] Kitabu cha Al-Muhilly bil-aathar 10/210.

[3] Kitabu cha Naili Al-Autwar 7/71.

[4] Kitabu cha Badaai Swanaaii cha Al-Kaasaany 4/5, 6.

[5] Kitabu cha sherehe mukhtasar Khalil 4/178.

[6] Kitabu cha Asnaa Al-Matwalibu cha Sheikh Zakari Al-Answary 3/416 na kitabu cha Mughny Al-Muhtaaj cha Sheikh Sharibiny 5/127, 128.

[7] Sherehe ya kitabu cha Muntaha Al-iraadat cha Bahuuty 3/215, na kitabu cha Kashaf al-Kinaai 5/455.

[8] Kitabu cha Al-Mughany cha Ibn Qudama 8/142.

[9] Kitabu cha Kifaayatu Twalib Rabbany cha Abi Hassan Ally Ibn Khalaf Al-Munuufy Al-Maliky 2/115/116. Na kitabu cha ASnaa Al-Matwaalib cha Sheikh Zakari Al-Answary 3/41, na kitabu cha Mughny Al-Muhtaj cha Sheikh Al-Khatwib Sharbiny 5/128, sherehe ya kitabu cha Muntaha Al-Iradaty cha Al-Bahuty 3/215, na kitabu cha Kashaf Al-Qinaai 5/455.

[10] Kitabu cha Badaii Swanaii cha Al-Kaasaany 4/5, na kitabuha sherehe Muntaha Al-Iradaaty 3/215 – na Hadithi imekubaliwa na Maimamu wote wa Hadithi: Kwenye kitabu cha Sahihi Bukhary ni Hadithi ya 4814, Sahihi Muslim Hadithi nambari 1455 na tamko la Imamu Bukhary.

[11] Kitabu cha Badaaii Swanaaii cha Al-Kasaany 4/5, na kitabu cha Asnaa Al-Matwalibu cha Sheikh Zakaria Al-Answary 4/416, sherehe Muntaha Al-Iraadaat cha Bahuty 3/215, na kitabu cha Kashshaf Al-Qinaa 5/455, na Hadithi imo katika kitabu cha Sunani Tirmidhy Hadithi nambari 1152, na Abu Isa amesema: Hadithi hii ni nzuri na sahihi, yamefanyiwa kazi na Wanachuoni wengi miongoni mwa Maswahaba wa Mtume S.A.W na wengine: Kuwa kunyonya hakupelekei uharamu isipokuwa kwa umri wa chini ya miaka miwili, na baada ya miaka miwili kamili hakuna uharamu wowote.

[12] Kitabu cha Asna Matwalibu cha Sheikh Zakaria Al-Answary 3/416, na kitabu cha Mughny cha Sheikh Al-Khatwib Sharbiny 5/128, 215, kitabu cha Al-Kashshaf Al-Qinaii cha Bahuty  5/455 – Al-Hafidh Ibn Hajar amesema katika kitabu cha Talkhiiswu Al-Hubair 4/8 Hadithi: “Hakuna kunyonyesha isipokuwa kwa mtoto wa miaka miwili” imepokelewa na Dar Al-Qutwny 4/174 ni katika Hadithi ya Amru Ibn Dinar kutoka kwa Ibn Abbas.

[13] Kitabu cha Badaai Swanaaii cha Al-Kaasany 4/5 – Al-Hafidhi Ibn Hajar amesema katika kitabu cha Talkhiisw Al-Hubair 4/8 Hadithi: “Kunyonyesha ni kunakojenga nyama na mifupa” Abu Daud Hadithi nambari 2059 kutokana na Hadithiya Abi Musa Al-Hilaly kutoka kwa baba yake kutoka kwa Masoud kwa tamko: “Hakuna kunyonyesha isipokuwa….” Na kuna kisa chake na Abi Musa katika kumnyonyesha mtu mkubwa, na Abu Musa pamoja na baba yake.

[14] Kitabu cha Badaaii Swanaaii cha Al-Kaasany 4/5 – Hadithi hii inapatikana katika sunani ya Dar Qutwny 4/173 na katika Sunani Baihaqy 7/460/461.

[15] Kitabu cha Badaaii Swanaaii cha Al-Kaasany 4/5 – Zailaii amesema katika kitabu cha Naswbi Raya 3/416. 417. Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kunyonyesha baada ya kuacha kunyonya”. Nimesema: Imepokewa Hadithi kutoka wa Ally, Hadithi inayotokana Jabir imepokelewa na Twabrany katika muujamu yake ndogo 2/158: kutoka kwa Ally amesema: Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kunyonyesha baada ya kuacha kunyonya, wala hakuna uyatima baada ya kubaleghe”. Kwa njia nyengine imepokelewa na Abdilrazak katika kitabu chake 6/416 kutoka kwa Ally kutoka kwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kunyonya baada ya kuacha kunyonya” kisha ikapokewa na Thawry, amesema Al-Uqaily katika kitabu chake cha Dhuafaa 4/428: Nayo ni kauli sahihi – lakini sikuwa na shahidi wa Hadithi – na imepokelewa na Ibn Ady katika kitabu cha Al-Kaamil 1/362, 363 kwa tamko: “Hakuna kunyonya baada ya kuacha kunyonya” ni Hadithi inayotokana na Ayubu Ibn Suweid kutoka kwa Thawry. Ama Hadithi inayotokana na Jabir imepokelewa na Abu Daud katika musanadi yake 1/ 243 ametuambi Kharijah Ibn Muswabu kutoka kwa Haram Ibn Othman kutoka wa Abi Atiiq kutoka kwa Jabir kutoka kwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kunyonya baada ya kuacha kunyonya, wala hakuna uyatima baada ya kufika baleghe”.  

[16] Kitabu cha Badaaii Swanaaii cha Al-Kaasany 4/5 – maelezo haya yanapatikana kwenye kitabu cha Muutwaa cha Imamu Maliki 2/578 na katika Sunani Baihaqy 7/461.

[17]  Kitabu cha Al-Mahally Bil-Aathaar 10/205.

[18] Kitabu cha Al-Mughny cha Dudama 8/142.

[19] Kitabu cha Al-Mahally Bil-Aathaar 10/205.

[20] Kitabu cha Al-Mahally Bil-Aathaar 10/205, 206.

[21] Kitabu cha Abdulrazak 7/461.

[22] Angalia kitabu cha Taqriib Al-Tahdhiib 361.

[23] Angalia kitabu cha Tahdhiibu At-Tahadhiibu 3/373.

[24] Kitabu cha Tamhiide 8/256, na kitabu cha Al-Istinkaar 6/255.

[25] Kitabu cha Twarhu Tathriib 7/135.

[26] Kitabu cha Abdulrazik 7/461.

[27] Kitabu cha Zaadul-Maad katika uongofu wa mbora wa waja 5/524.

[28] Kitabu cha Naili Al-Autwal cha Shaukany 2/72.

[29] Kitabu cha Sahihi Muslimu Hadithi nambari 1454.

[30] Kitabu cha Badaaii Swanaaii 4/5, 6. Na kitabu cha Asnaa Al-Matwaalib 3/416. Na kitabu cha Mughny Al-Muhtaaj 5/129. Na kitabu cha Kashaaf Al-Qinaai 5/445.

[31] Kitabu ch Fat’hul-Bary sherehe ya Sahihi Muslimu 9/149.

[32] Kitabu cha Badaaii Swanaaii 4/6.

[33] Marejeo yaliyopita 4/5.

[34] Kitabu cha Zaadul-Maad 5/522 na kurasa zinazofuata.

[35] Kitabu cha Naili Al-Autwar cha Shaukany 2/72.

[36] Kitabu cha Maarifatul-Sunan cha Baihaqy 11/263, 264.

[37] Kitabu cha Majmuui Fatawa 34/60. Na kitabu cha Fatawa Al-Kabiir 5/515. Na kitabu cha Zaadi Al-Maadi cha Ibn Qayyim 5/527.

[38] Kitabu cha Nailil-Autwar 7/71.

[39] Marejeo yaliyopita, pamoja na kwenye kitabu cha Zaad Al-Maad 5/513.

[40] Kitabu cha An-Nihaaya fii ghariibil-Hadithi, cha Ibn Al-Athiir 2/259.

[41] Kitabu cha Al-Iqnaa cha Khatibu Sharbiny2/364, na kitabu cha Alrawdhu Al-Marii sherehe ya Zaad Al-Mustaknaa cha Mansour Al-Bahuuty 3/218.

[42] Kitabu cha Al-Iqnaa cha Khatibu Sharbiny2/364

[43] Kitabu cha Taarifaat cha Jarjany 1/36.

[44] Kitabu cha Salsabiil fii maarifatil-Daliil cha Balbahiy 3/95, pia kitabu cha Rawdhu Al-Muriii 3/218.

[45] Na hilo ni kama vile kutumia chombo cha kukamulia ambacho kinakamua maziwa kutoka kwenye chuchu za mnyonyeshaji, kisha yanawekwa kwenye chombo na kunywa mtoto pasi ya kugusa chuchu za mama.

[46] Sherehe ya Sahihi Muslimu ya An-Nawawy 10/31.

[47] Kitabu cha Twabakatul-Kubraa 8/271. Na kitabu cha Al-Swaba fii tamyiizi Swahaba 7/716. Na kitabu cha Al-Mis’atwu cha Khalil Inb Ahmad.

Share this:

Related Fatwas