Hukumu ya kujiua

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kujiua

Question

Ni ipi hukumu ya mtu anayejiua?

Answer

Kujiua ni haramu kwa mujibu wa Sharia ya Kiislamu, na ni moja ya madhambi makubwa. Kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.} na kauli yake Mtume (S.A.W) isemayo: “Na mwenye kujiua kwa kitu basi ataadhibiwa nayo Siku ya Kiyama” (Imeafikiwa) Japokuwa mtu aliyejiua amefanya dhambi kubwa, lakini haijuzu kumueleza kuwa ni kafiri na ametoka katika dini, bali huoshwa na kuvikwa sanda na kuswaliwa, na kuzikwa katika makaburi ya Waislamu, anaombewa rehema na msamaha. Hata hivyo, dhambi ya uhalifu huu mkubwa isipunguzwe, wala isitengenezwe uhalali wake. Yeyote anayehisi dalili zake, kama vile mgonjwa wa moyo aliyezidiwa, hana budi kuharakisha kwenda kwa madaktari wataalamu kumsaidia apate matibabu na kuondokana na matatizo ya ugonjwa huo.

Share this:

Related Fatwas