Karama na Muujiza.

Egypt's Dar Al-Ifta

Karama na Muujiza.

Question

Nini maana ya karama? Ipi mipaka yake? Na ipi tofauti kati ya karama na muujiza? 

Answer

Karama ni kitendo cha tofauti na kawaida Mwenyezi Mungu huipitisha mikononi mwa mja mwema, na karama haikutani na madai ya Utume, mtu mwenye karama huwa hadai kuwa ni Mtume, bali ni kwa upande wa ukirimu wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wema pamoja na mawalii wake waliokirimiwa, kama vile kukunjika kwao ardhi au kufanya tasbihi (Utakaso) pamoja na vitu visivyo na uhai, na yasiyokuwa hayo katika karama zilizoahidiwa kwa mawalii na kupitia kwa baadhi ya Maswahaba na watu waliofuata baada ya Maswahaba, na hasa kwa waja wema wa Umma wa Muhammad, na mipaka yake ni kufanya jambo lisilowezekana kwa kawaida si kiakili, kwa kawaida maji kwa mfano mtu huzama anaposimama juu yake, hivyo inafaa kwa Mwenyezi Mungu kufanya tofauti na kawada kwa mja wake ili kuonesha wema wa mja wake na uwalii wake kwa maji hayo kumbeba mja huyo, hilo ni jambo lisilowezekana kwa kawaida, ama kisichowezekana kiakili ni kile kisichofikiriwa kutokea kwake, kama vile kukifanya kitu kipo lakini wakati huo hakipo.

Tofauti kati ya karama na muujiza ni kuwa muujiza ni jambo lisilo la kawaida Mwenyezi Mungu hupitisha mikononi mwa mwenye kudai Utume, ikiwa ni kuaminisha madai yake kuwa yeye ni Mtume kutoka kwa Mola wa viumbe, na karama ni jambo lisilo la kawaida lisilofungamana na madai ya Utume, hivyo inafaa kutokea kwa mja yeyote aliyetakiwa na Mwenyezi Mungu.

Share this:

Related Fatwas